Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA RAIS ZUMA NA RAIS KABILA ZIMBABWE

$
0
0
 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini pamoja na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwa ajili ya viongozi wa SADC wanaohudhuria mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe .Picha na Freddy Maro

*MAULID KITENGE AACHA KAZI ITV NA RADIO ONE LEO.

$
0
0

MTANGAZAJI machachari wa habari za michezo kupitia kituo cha Televisheni cha ITV na Radio One, Maulid Baraka Kitenge (pichani) leo kupitia akaunti yake ya Twitter ametangaza rasmi kubwaga manyanga (kuacha kazi) katika Kampuni hiyo aliyokuwa akiifanyia kazi baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 14. chini ni ujumbe wake aliouandika kupitia akaunti yake ya Twitter.

*JAJI LEWIS MAKAME AFARIKI DUNIA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia hivi punde,inaeleza kuwa aliewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini,Jaji Mstaafu Lewis Makame (pichani) amefariki dunia mchana huu katika hopitali ya Hospital ya AMI Trauma Center, Masaki jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

taarifa kamili itakuja baadae.

*MAULID KITENGE ATIMKIA KWA 'MKUDE SIMBA' E FM 93.7

$
0
0
TAARIFA  KWA VYOMBO VYA HABARI.


18/August 2014.


MtangazajimahiriwamichezowasikunyingiMaulidi Baraka Kitengeamejiunganakituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopoKawejijini Dar Es salaam.


Kutokananatafitiyaipsosyamwaka 2013,inasemekana kuwamtangazajihuyowazamaniwakituo cha redioone,ndiemtangazaji bora wamichezonchini Tanzania.


Mkurugenziwavipindiwa  RadioEFM,DicksonPonela,ameelezakufurahishwakwakwekwamtangazajihuyokinarakuhamiakatikakituohicho.


“MpakasasaMaulidiKitengeameshasignmkatabanakituochetunaanatarajiakusikikahivikaribunikatikakipindi cha michezohapa EFM”, alisemamkuregenzihuyo.


MaulidiKitenge au jezinambaritisamgongoni, amejiunganamagwijiwaliobobeakatikafanihiyoakiwemoDizoone,DennisSebo,SosB,KankyMwaigomolenaDjMajay.




---------------------------------------END-----------------------------------------

*FAINALI YA TANZANIA MOVIE TALENTS NDIO HABARI YA MJINI KWA SASA

*GARI INAUZWA

$
0
0
 Nissan Patrol ipo sokoni.
Nissan Patrol, Engine TD42, 4200CC,Diesel, Manual, Make 1997.

Wasiliana kwa namba 0752 753 309

*BALOZI IDDI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA MAAFA KUWEKA MIKAKATI YA KUJILINDA NA EBOLA

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya kukabiliana na maafa  Zanzibar akikiongoza kikao hicho kuweka mikakati maalum ya kupambana ya ugonjwa wa Ebola endapo utaingia katika Visiwa vya Zanzibar.
Wajumbe wa Kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar wakiendelea kujadili mikakati mbali mbali itakayosaidia kujikinga na ugonjwa wa Ebola ambao tayari umeshaziathiri nchi kadhaa za Afrika Magharibi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
***********************************
Zanzibar imeanza mikakati maalum ya kujiweka tayari kupambana dhidi ya  janga la Kimataifa la kuibuka kwa maradhi ya Ebola endapo yataingia ndani ya visiwa vya unguja na Pemba maradhi ambayo tayari yameshazikumba nchi kadhaa za Afrika magharibi.
Mikakati hiyo imechukuliwa kutokana na mazingira halisi ya Visiwa vya Zanzibar kufungamana pamoja na maingiliano ya mara kwa mara kwa wageni kutoka nchi mbali mbali duniani kupitia sekta ya utalii inayoingiza wageni wengi.
Kikao cha Kamati ya Taifa ya kukabiliana na maafa Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kilikutana kwa dharura Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kupanga mikakati itakayosaidia kukabiliana na janga hilo.
Wajumbe wa kikao hicho kilichotoa baraka ya kuundwa kwa kamati ndogo itakayoratibu mikakati hiyo chini ya uwenyekiti wa Wizara ya Afya wameelezea umuhimu wa kuendelea kutolewa  elimu kwa wananchi itakayosaidia kujikinga na maradhi hayo hatari.
Walisema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na shirika la Bandari, mamlaka ya Viwanja vya ndege, Idara ya Uhamiaji pamoja na taasisi nyengine ziendeleze uchunguzi na ufuatiliaji wa wageni wote wanaotoka katika nchi ambazo tayari ugonjwa huo umeshaathiri.
“ Utaratibu wa kutolewa elimu maalum kupitia vyombo vya Habari pamoja na magari ya sinema kwa kamati za maafa kuanzia Taifa hadi shehia juu ya ugonjwa huo unafaa kupewa msukumo wa dharura pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye bandari bubu “. Walisema wajumbe hao.
Baadhi ya wajumbe hao walishauri kujumuishwa kwa wawekezaji vitega uchumi mbali mbali waliopo hapa nchini ambao wana taaluma wa fani tofauti inayoweza kusaidia mikakati hiyo.
Walieleza kwamba  utafiti ufanywe kuangalia sifa za wawekezaji hao ambao huziainisha kwenye mikataba yao wakati wanapoomba uwekezaji  vitega uchumi vyao hapa nchini.
“ Tumeshuhudia baadhi ya wawekezaji  hao wakati wa maafa ya kuzama kwa meli ya M.V Spice Island kwenye mkondo wa Nungwi walivyotusaidia kitaalamu pamoja na mawasiliano “. Alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya watembezaji watalii Zanzibar { ZATI } Simai Mohammed.
Kuhusu suala la ushiriki wa vyombo vya Habari katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo wa ebola Wajumbe hao walishauri watendaji wa vyombo hivyo kupatiwa semina maalum zitakazosaidia katika kutoka elimu hiyo kwa wananchi.
Walifahamisha kwamba wapo Wahariri  na hata baadhi ya mitandao ya kijamii inaopenda kutumia matukio kama haya kueleza mambo  yaliyo tafauti na uhalisia wa matukio yenyewe.
Ugonjwa wa Ebola uliogundulika mwaka 1976 Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo { DRC } na Sudan ni miongoni mwa ugonjwa hatari wa mripuko unaoenea kwa kasi na kusababisha vifo vingi kwa wakati mmoja.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na homa, kuumwa kwa kichwa, kuumwa kwa misuli na viungo vya mikono na miguu, koo, kukosa nguvu za mwili na baadaye kufuatiwa na vipele katika ngozi, macho kuwa malegevu, kwikwi na hatimae kutokwa na damu katika tundu mbali mbali za mwili ikiwemo pua, masikio, mdogo na ngozi.
Ugonjwa huu wa Ebola hujichomoza baada ya virusi vyake kuenezwa kwa kupitia mnyama kwenda kwa binaadamu na binaadamu kwenda kwa mwengine mnyama popo akithibitika kuwa ndie chanzo kikuu cha ugonjwa huo.
Hadi sasa hakuna dawa wala chanjo maalum inayoweza kutibu ugonjwa wa Ebola lakini kinachofanyika kwa hivi sasa ni mgonjwa husika kupatyiwa matibabu ya kusaidiwa kutokana na dalili zilizojitokeza.
Mripuko wa ebola unaoendelea hivi sasa ulianza kugundulika mara ya kwanza nchini Guinea mnamo Tarehe 21 Marchi mwaka huu wa 2014 na baadae kuenea kwa kasi katika nchi jirani za Liberia, Siera Leone na Nigeri.
Hadi kufikia Tarehe 11/8/2014 jumla ya wagonjwa 1,975 wamegunduliwa kuambukizwa ugonjwa huo wakiwemo wafanyakazi wa afya 140 ambapo kati yao wagonjwa 1,069  na wafanyakazi 80 wa afya wamefariki dunia.
 Shirika la Afya Ulimwenguni { WHO } Tarahe 8/8/82014 lililazimika kutangaza mripuko huo kuwa ni janga la Kimataifa la Afya la Kijamii.

*MAANDALIZI YA UTOAJI MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.

Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

**********************************************
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 

MCHAKATO WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015


1.0        MAANDALIZI YA UTOAJI MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitangaza mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 kupitia magazeti na tovuti yake mnamo wezi Aprili 2014. Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine, uliainisha sifa za waombaji mikopo na ruzuku, vipengele vya Mikopo, programu za vipaumbele kwa waombaji wa shahada ya kwanza, shahada za uzamili na uzamivu waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu zinazotambulika. Maombi ya mikopo kwa waombaji wapya yalifanyika kwa njia ya mtandao kwa anuani ya http://olas.heslb.go.tzau kupitia anuani ya tovuti ya Bodi ya Mikopo ambayo ni: www.heslb.go.tz

Kulingana na Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa mwaka wa masomo 2014/2015, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilifungua maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS) kuanzia Aprili 23, 2014 na kuendelea kupokea maombi hayo hadi Julai 31, 2014.


Mabadiliko machache yamefanyika, kubwa likiwa ni kwa wanufaika wanaoendelea na masomo, tofauti na ilivyokuwa miaka iliyopita, hawakutakiwa kujaza tena fomu kuthibitisha uhitaji wao wa mikopo kwa mwaka unaofuatia, isipokuwa kwa wale ambao waliopenda kusitisha kuendelea kupokea mkopo kutoka Bodi. Wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo wataendelea kupata mikopo yao kulingana na viwango walivyopangiwa awali.


1.1        Maombi yaliyopokelewa


Jumla ya maombi 58,037 yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2014.  Kati ya maombi hayo, jumla ya maombi 37,689 ni ya waombaji wa kiume na maombi 19,592 ni ya waombaji wa kike.  Uchambuzi zaidi wa waombaji wa mikopo unaonyesha kuwa Waombaji wa kundi la diploma ya ualimu wa sayansi ni 480 (Me – 324, Ke – 156), Waombaji wa shahada ya uzamili/uzamivu (kwa vyuo vya ndani ya nchi) ni 276 (Me – 194, Ke – 82), Waombaji wa shahada ya kwanza (kwa vyuo vya ndani ya nchi) ni 56,922 (Me – 37,460, Ke – 19,462), Waombaji wa shahada ya uzamili/uzamivu (nje ya nchi) ni 126 (Me- 88, Ke – 38) na Waombaji wa shahada ya kwanza (nje ya nchi) ni 233 (Me – 141, Ke – 92).


1.2  Uchambuzi wa Maombi

Baada ya kufungwa rasmi kwa kipindi cha kupokea maombi ya mikopo, hatua inayoendelea kwa sasa ni uhakiki (verification) wa taarifa za waombaji, kwa kuzipitia nyaraka mbalimbali zilizoambatanishwa na waombaji mikopo ambazo ni cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, vielelezo vya mdhamini, saini ya mwombaji na mdhamini wake na ushuhuda wa Mwanasheria au Hakimu kwamba vivuli vya nyaraka zilizowasilishwa kwenye Bodi ni halisi.


1.3   Upangaji wa mikopo

Mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo utakamilika baada ya majina ya wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kujiunga na vyuo mbalimbali yanapowasilishwa rasmi kwenye Bodi ya Mikopo. Udahili wa wanafunzi unafanywa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) unaotumiwa na vyuo takribani vyote vya elimu ya juu nchini. Kwa vyuo ambavyo havimo katika mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) hutuma TCU majina ya wanafunzi ambao vimewadahili ili waweze kuthibitishwa kabla ya kupatiwa mikopo.   Taarifa za udahili ni muhimu katika zoezi la upangaji wa mikopo kwa kuwa zinatoa mwongozo wa gharama halisi za programu za mafunzo. Wanafunzi wanaostahili na waliotimiza masharti na vigezo vya ukopeshaji ndio hupangiwa mikopo kulingana na bajeti iliyotengwa na Serikali.


1.4   Kutangazwa kwa majina ya wanafunzi waliopata mikopo

Majina ya wanafunzi waliopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi na taarifa hiyo pia itatangazwa katika vyombo vya habari ili kuwataarifu wadau wote ikiwa ni pamoja na wanafunzi, vyuo vya elimu ya juu, wazazi na umma kwa ujumla. Nakala za majina ya wanafunzi waliopangiwa mikopo zitatumwa kwenye vyuo husika.


2.0        WANAFUNZI WA MASOMO YA STASHAHADA YA UALIMU


Kwa kutambua umuhimu wa masomo ya Sayansi na kukabiliana na upungufu

wa walimu wa masomo hayo katika ngazi ya shule za  Msingi na Sekondari, mwaka huu serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya Stashahada maalum ya Ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.


Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na Stashahada hii maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma na wote watanufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.


3.0        HITIMISHO


Kwa Taarifa hii, Bodi inapenda kuwataarifu wadau wote kuwa mchakato wa utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 unaendelea vema.


Aidha, Bodi inawasisitizia waombaji wa Mikopo, wazazi/walezi na umma kwa ujumla kutambua kuwa Mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya juu na hivyo iwapo kuna waombaji wanaoweza kujigharamia, wasiombe mikopo ili kutoa nafasi kwa wahitaji wengi zaidi kunufaika.
                  

Imetolewa na:

KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


*KARIBU KATIKA BLOG MPYA YA UJENZI ZONE

$
0
0
Habari Mdau, Pole na kazi za kujenga Taifa, Nilikuwa naomba msaada wako wa kunitambulishia Blog ambayo nimeianzisha kwa sababu ya Ujenzi, kusaidiana maswala mbalimbali yanayohusu ujenzi nina ambatatinisha kila kitu hapa chini.
Asante sana
Jackqueline 
**************************************
Karibuni wadau wote  katika Blog yenu  mpya ya wanaujenzi, hapa tutakuwa pamoja  kushirikiana kwa mawazo, ushauri,  ujuzi tulioupata wenyewe na kwa ujuzi wa wataalamu waliosomea fani ya ujenzi. Kama wewe unajenga nyumba yako mwenyewe, kama umewahi kujenga, kama unajipanga kujenga na hata kama una ndoto kwamba siku moja utajenga nyumba,  Basi karibu sana katika blog Hii kujua mengi.

Toa mchango wako wa mawazo, tujulishe umefanikiwa vipi kutatua matatizo uliyokabiliana nayo kwenye ujenzi, wako mshauri mwenzio ambae anatafuta njia ya kufanikisha azma yake na anatamani nae akae kwenye nyumba yake mwenyewe, uliza swali kwa jambo linalokutatiza au toa ushauri kuhusu kitu chochote unachoona unaweza kuchangia na wanaujenzi tukanufaika nacho, hakuna mtu mmoja anayejua kila kitu, ila kwa kushirikiana pamoja tunaweza.

Familia ya wanaujenzi inamjumuisha kila mmoja wetu, iwe umejenga ghorofa, iwe umejenga chumba kimoja, iwe ndiyo kwanza unajinyima ili ukanunue kiwanja, hapa ni mahala pako.

Mwisho
Changamoto ni nyingi kwenye safari ya ujenzi wa makazi yetu, tupo hapa kuelimishana, kupeana moyo na zaidi kurahisisha zoezi zima la ujenzi, kushirikiana uzoefu ndio hasa lengo la Blog hii ya Ujenzi Zone. Chochote kinachohusu ujenz kwa mtazamo chanya kitafaniakisha zaidi lengo la Blog hili kutimia.

TEMBELEA SASA BOFTYA HAPA : www.ujenzizone.blogspot.com

*HABARI KUTOKA TFF LEO, MTIBWA, POLISI MORO KUCHEZA MECHI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI

$
0
0

 MTIBWA, POLISI MORO KUCHEZA MECHI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI

Timu za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitacheza Jumamosi (Agosti 23 mwaka huu) mechi ya majaribio ya mfumo wa tiketi za elektroniki.

Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.

Tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho (Agosti 20 mwaka huu) kupitia mtandao wa M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa Morogoro Mjini.

Washabiki 100 wa kwanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.

Tayari mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons na Mbeya City zilipambana na kutoka sare.

Mechi nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30 mwaka huu. Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.

Septemba 6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga itakayofanyika Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

*WAAMUZI KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
Waamuzi wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) mwezi ujao.

Mtihani huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo pia wale wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mbali ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu, pia kutakuwa na semina kwa makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na FDL.

Hivyo waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya mtihani huo.

*MAKOCHA COPA COCA-COLA KUNOLEWA DAR
Makocha wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja na waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.

Kozi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa itakayochezwa Septemba mwaka huu.

Makocha watakaoshiriki kozi hiyo na mikoa yao kwenye mabano ni Ahmed Simba (Mwanza), Ally Kagire (Kagera), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Anthony Mwamlima (Mbeya), Athuman Kairo (Morogoro), Bakari Ali (Kaskazini Pemba) na Charles Mayaya (Shinyanga).

Fidelis Kalinga (Iringa), Gabriel Gunda (Singida), Hafidh Muhidin Mcha (Kusini Pemba), Hamis Mabo (Kigoma), John William (Geita), Joseph Assey (Shinyanga), Joseph Haley (Manyara), Jumanne Ntambi (Kilimanjaro), Leonard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara), Mohamed Muya (Dodoma), Nicholas Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).

Osuri Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha), Ramadhan Abdulrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja (Lindi), Seif Bakari (Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Sheha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Tigana Lukinjo (Njombe), Yusuf Ramadhan Hamis (Kusini Unguja), Zahoro Mohamed (Tanga) na Zakaria Mgambwa (Rukwa).

Waamuzi vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix Tangawarima wa Zimbabwe ni 33. Kwa upande wa ukocha Mkufunzi ni Ulric Mathiott kutoka Shelisheli.

*KOZI YA UKOCHA LESENI A KUFANYIKA SEPTEMBA 4
Kozi ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika mara ya kwanza nchini, jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 4 mwaka huu.

Mkufunzi wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF, na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh. 300,000.

Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF. Fomu kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya TFF.

*WAZIRI WA VIWANDA AFUNGUA MAONESHO YA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI CHINA

$
0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia pikipiki  aina ya SWAN inayotengenezwa na kampuni ya Honda ambayo inayotumia mafuta ya Petrol na Umeme wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini China.  Kulia kwake ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na kushoto ni  Juwes Wang ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia viatu vinavyozalishwa nchini China wakati wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini humo ambayo yamefunguliwa leo na kumalizika jumapili ya tarehe 24/8/2014.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia vitenge vinavyozalishwa nchini China wakati wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini humo.
 Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing  akimkabidhi zawadi  Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda wakati wa  ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini humo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akimsikiliza Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing  wakati wa  hafla fupi ya ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini humo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda na  Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini China.
 Baadhi ya wageni aliohudhuria  sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini China wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (hayupo pichani) .
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Shenzhen Yingli New Energy Resources Honglin Hui (Kulia) akimueleza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (kushoto) jinsi Solar Panel  inayotengenezwa na kampuni hiyo  inavyofanya kazi wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa  nchini China yaliyofunguliwa leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es Salaam. Picha na Anna Nkinda- Maelezo

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA UHOLANZI IKULU ZANZIBAR LEO.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw.Jaap Frederiks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw.Jaap Frederiks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw.Jaap Frederiks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada ya mazungumzo leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

*RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI NA AFUNGUA KITUO CHA AFYA KIBAONI, MOROGORO VIJIJINI

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea akikagua wodi mpya ya  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa maeneo mbali mbali ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini baada ya kukifungua Agosti 22, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazazi baada ya kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. PICHA NA IKULU

*RAIS KIKWETE ASAFIRI KWA TRENI YA TAZARA KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini  Mhe Innocent Kalogeris na KAtibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki mkoani Morogoro.
 Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri (kulia) na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri zawadi ya picha ya jengo la makao makuu ya TAZARA akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa  Morogoro.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumlaki Rais.
 Rais Jakaya, akipunga mkono kuwasalimia wananchi....
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na umati mkubwa wa watu baada ya kuwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika mkoa wa Morogoro. PICHA NA IKULU

*LUIS FOGO, CALEMBEU, SANZ WAZUNGUMZIA MTANANGE WAO NA TANZANIA ELEVEN STARS KESHO UWANJA WA TAIFA

$
0
0
 Mchezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid, ambaye pia ni Kiongozi wa Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid,Luis Figo, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mchezo wao wa kirafiki na timu ya Tanzania Eleven inayoundwa na wachezaji wa zamani wa timu za Yanga, Simba na Taifa Stars, utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia mchezo huo Figo amesema kuwa wao wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya kuonyesha uwezo na kutoa burudani kwa mashabiki wao wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kujenga ushirikiano baina ya wachezaji wa Hispania na Tanzania. Kulia ni Christian Calembeu, na Mkurugenzi wa TSN Frank Baghoza na Kocha wa timu ya Madrid.
 Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven Stars, Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati) akizungumzia namna Timu yake ilivyojiandaa kuwakabili magwiji hao soka,  wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Luis Figo na kulia kwake ni Fernando Sanz Duran ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
 Fernando Sanz Duran, akiwapiga picha ya kumbukumbu wenzake wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwa bize kunasa matukio. 

*MISS TEMEKE 2014 KUJULIKANA KESHO UKUMBI WA TCC CLUB CHANGOMBE, JIJINI DAR

$
0
0


 NANI kati wa washiriki 17 ataibuka kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Temeke 2014, linalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa TCC Club Chang'ombe Dar es Salaam.

Jumla ya warembo 17 kutoka vitongoji vya Mbagala, Kurasini na Chang;ombe watapanda jukwaani kuwania taji hilo, huku washindi wa tatu watapata nafasi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2014.

Akizungumza Dar es Salaa jana Mkurugenzi BMP Promotions, Benny Kisaka, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika kama yalivyopangwa.

Kisaka alisema kuwa taji linaloshikiliwa na mrembo kutoka kanda ya kati, lakini mwaka huu Temeke imejizatiti kutoa si tu Miss Tanzania, mbali warembo watatu wa kwanza wa Taifa kutokana na viwango vya warembo wa mwaka huu.

Alisema kuwa mbali ya shindano hilo kubwa, kulifanyika shindano dogo la awali lililoandaliwa na Michuzi Media la Miss Photogenic ambalo mshindi wake atazawadiwa kitita cha Sh. milioni 1 taslimu, shindano ambalo lililsimamiwa na jopo la wapiga picha wa kampuni hiyo ambao watamtangaza na kumpa zawadi mshindi siku ya shindano.

Kisaka aliwataja Warembo wanaotarajiwa Subira Ally, Hellen Yughin, Catherine Alex, Dalina David, Winfrida Guntram, Salama Salehe, Grace John, Lilian Lothy, Amina Salim, Rebecca Mdamu, Sitti Mtemvu, Hellen Sule, Neema Mollel, Lucy Lewis, Esther Mnahi, Pauline Nkini na Patricia Ponsian ambao walikuwa chini ya ukufunzi wa Super Bokilo, Shadya Mohamed na Sweet Remmy.

Alisema mkali wa bongofleva, Khalid Mohamed TID almaarufu kama Top in Dar, sanjari na Wanne Star, Makirikiri wa Tanzania, Young Suma, Super Bokilo na wasanii mbalimbali wanatarajia kupamba shoo hiyo ambayo Dj John Peter Pantelakis atalisindikiza.

Wadhamini wa shindano hilo ni TBL Kupitia Redds wamedhamini shindano hilo sanjari na kinywaji cha Zanzi, Michuzi Media Group, Radio EFM 93.7 Cash & Carry Distributors, Kitwe General Traders, Rio Gym & Spa, CXC Africa, 88. 5 Clouds FM, City Sports Lounge, Gazeti la Jambo Leo, Kiwango Security na 100.5 Times FM.
BMP Promotions imeshakamilisha shindano hili la 19 tangu kuanzishwa Miss Temeke chini ya undaaji wake kwa asilimia kubwa, hivyo washabiki wa Kanda ya Temeke na vitongoji vyake watarajie mabadiliko makubwa katika aina ya shindano la urembo litakavyokuwa Ijumaa.

1996- Asela Magaka
1997- Miriam Odemba
1998- Khamisa Ahmed (Miss Temeke anayeendea kujiita hivyo huko Marekani)
1999- Ediltruda Kalikawe
2000- Irene Kiwia
2001- Happyness Sosthnes Magesse
super model Millen( Miss Tanzania)
2002- Regina Mosha
2003- Hawa Ismail ( Sylvia Bahame first runner up and Miss Tanzania same year)
2004- Cecylia Assey ( mrs Agrey Marealle), first runner up Miss Tanzania
2005- Seba Aggrey
2006- Jokate Mwegelo (Miss Tanzania fisrt runner up), Irene Uwoya 1st runner Temeke & 3rd runner up Miss Tanzania
2007- Queen David ( Miss Tanzania second runner up)
2008- Angela Lubala (top five Miss Tanzania)
2009- Sia Ndaskoy (top five Miss Tanzania)
2010- Genevieve Mpangala ( Miss Tanzania)
2011- Husna Twalib
2012- Edda Sylvester
2013- Svetlana Nyameyo ( Latifa Mohamedsecond runner Temeke and first runner up Miss Tanzania)

*WAZEE WA NGUO NYEUPE WAHINI ENEO HIKI NANI MWENYE KOSA???

$
0
0
Magari yenye namba za usajili T 784 BUM na T 208 ASL, yakiwa yamegongana barabara ya Azikiwe mbele ya Benki ya CRDB, muda huu na kusababisha foleni kubwa eneo hilo.

*KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AWAAGA WANAFUNZI WA TANZANIA WALIOPATA UFADHILI WA MASOMO NCHINI UHOLANZI

$
0
0
 Makamu Mkuu wa Misheni ya Uholanzi, Bi. Hinke Nanta (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Kiongozi (katikati) wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa nasaha zake kwa wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks akitoa hotuba yake kwa wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO-DSM
**************************************************
Na Benedict Liwenga-MAELEZO

KATIBU Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amehudhuria hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata udhamini kwenda kusoma nchini Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo za mafuta na gesi, miundombinu, kilimo, maji, afya pamoja na Maendeleo ya sekta binafsi.
Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Balozi wa Uholanzi eneo la Oysterbay Jijini Dar es salaam ambapo Katibu Kiongozi ndiye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Katibu Kiongozi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa program ilianzishwa na nchi ya Uholanzi wa kuwasaidia watanzania kupata ufadhili kamili wa kwenda kusoma masomo mbalimbali nchini humo na ujuzi wanaoupata uweze kulisaidia Taifa pamoja na watanzania wengine kwa ujumla.
“Ninaamini kuwa wanafunzi hawa waliopata ufadhili huu wa masomo mbalimbali nchini Uholanzi watapata fursa kubwa ya kusomea mambo mbalimbali na ujuzi huu hawatakaa nao wenyewe binafsi, bali watalisaidia taifa na watanzania wengine, hivyo wajenge moyo huo wa kutokuwa wabinafsi”. Alisema Sefue. 
Naye Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks amesema kuwa amefurahi kwa muamko mkubwa wa watanzania wengi wa kuomba nafasi za masomo nchini kwake na amewaasa wengine kuiga mfano huo kwani nchi yake itaendelea na programu hiyo kulingana na bajeti pamoja na wataalam waliopo nchini Uholanzi.
“Nchi yangu inatoa fursa ya masomo kwa watanzania kwenda kusoma lakini tunaangalia maeneo ambayo tuna wataalam ambao wanaweza kuwasaidia watanzania kuwapa elimu, hivyo ni jukumu lao wenyewe watanzania kuaamua maeneo gani ya kusomea pamoja na kozi wazipendezo”. Alisema Frederiks

Katika kipindi cha miaka Hamsini iliyopita, zaidi ya watanzania Elfu tano wamepata udhamini wa kusoma katika sekta mbalimbali zikiwemo Utawala wa Fedha, Uhandisi, Miundombinu, Kilimo, Afya, Elimu na Utawala ambapo hii inaifanya Tanzania kuwa moja ya ya wanufaikaji wakubwa duniani wa programu hii ya udhamini wa masomo, ambapo wengi wa watanzania waliopata nafasi hizi wameshika nyazifa muhimu katika Jamii ya Tanzania kitu ambacho kinaendeleza ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

*MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU LEWIS MAKAME WAAGWA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame likiwa  mbele ya viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Viongozi mbalimbali wa Serikali wakilisikiza wasifu wa marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na nyuso za uzuni wakati wa  kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wafiwa akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakilisikiza wasifu wa marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 

Picha na Anna Nkinda- Maelezo

*SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA MISHAHARA YA WATUMISHI YA MWEZI JULAI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiongea na waandishi wa habari wakati alipokuwa akifafanua juu ya malipo ya mishahara ya watumishi yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu leo jijini Dar es salaam ambapo ameonya mamlaka husika ziwe na taarifa sahihi za idadi ya watumishi ili kuondoa makosa ya kulipa mishahara hewa, endapo kutatokea makosa ya ulipaji wa mishahara hewa watachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani.Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live




Latest Images