↧
*TAMASHA LA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015
↧
*WATAKAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA DART KUPIGWA FAINI YA SHILINGI LAKI TATU
Mkurugenzi wa Mifumo Junn Mlingi kutoka Taasisi ya Mabasi yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transport) akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo katika kituo cha Kivukoni jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakipanda gari la Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jana jijini Dar es Salaam katika ziara ya kukagua Miundo Mbinu ya Mradi wa DART kabla ya kuanza kutumika .
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakikagua kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Afisa wa Tanroads akikagua kibanda cha kukatia tiketi kilichopo ndani ya kituo cha Kimara katika mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads wakiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka walipokuwa wakifanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam. Picha na Anitha Jonas –MAELEZO.
************************************
Na Ally Daud- MAELEZO.
Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam (DART) Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa miundo mbinu ya mradi huo.
Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35 kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika tano.
“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.
Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.
Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.
Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.
Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden Dragon kutoka Japan.
↧
↧
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA MAUNGUMZO NA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO NCHINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Jasem Najem wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Jasem Najem, baada ya mazungumzo yao Ikulu Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Katarina Rangnitt, wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo kwa ajili ya kujitambulisha rasmi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Pekka Hukka, wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka, baada ya mazungumzo yao Ikulu Dar es Salaam, leo.
↧
*MASHEIKH WA TANZANIA WAWASILI SALAMA MJI MTAKATIFU WA MAKKA KUTEKELEZA IBADA YA HIJA
Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeiry (kushoto) Sheikh Mkuu wa Mtoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa (kulia) na Sheikh Sayd Hassan, kutoka Kenya. wakiwa katika picha ya pamoja, katika mji mtakatifu wa Makka, walikokwenda kutekeleza Ibadaa ya Hija. Sikukuu ya Eid El Haj inatarajia kuwa Septemba 24.
↧
*LIGI KUU KUENDELEA TENA LEO NA KESHO, VIWANJA NANE KUWAKA MOTO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Leo Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports kutoka Tanga, katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
*U15 WALIOKWENDA MAZOEZI ORLANDO PIRATES WAREJEA
Kufuatia safari ya vijana watano wa U15 Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias, Athumani Maulid waliokwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando Pirates kufuatia mwaliko uliotolewa na TFF na klabu hiyo, safari hiyo ilikamilika na vijana wamerejea nyumbani. Fuata link chini kwa taarifa zaidi
*FDL KUTIMUA VUMBI KESHO
Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao. KUSOMA ZAIDI BOFYA LINK HIYO CHINI
↧
↧
*WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AENDELEA KUPOKEA MISAADA YA VIFAA MBALIMBALI KUSAIDIA SHULE MSINGI KAKUNI MKOANI KATAVI
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa kompyuta mpakato zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi leo jijini Dar es salaam. Shule hiyo ya kisasa imeanzishwa kufuatia wazo la Wazo la Waziri Mkuu, Mhe.Mizengo Pinda la kuwa na shule Bora na ya kisasa katika kijiji hicho na inajengwa kupitia michango na misaada ya wadau mbalimbali.
Mwakilishi wa Kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania Bw. Jimmy Liguo Jin (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda sehemu ya msaada wa Tabuleti 100 zilizotolewa na kampuni hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi ya Kakuni iliyo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi.
Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kikundi cha Ushonaji cha Vijana Sokoine (SYG) kilichopo mkoani Dodoma Bw. Salehe Mustapha akimkabidhi Waziri Mkuu Mizengo Pinda msaada wa Sare uliotolewa na kikundi hicho kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni iliyopo katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi .
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya HUAWEI nchini Tanzania mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni hiyo kusaidia elimu katika shule mpya ya msingi Kakuni mkoani Katavi, ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Bw. Waziri Barnabas akimkabidhi Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Tanzania sehemu ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na NMB kusaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Benki hiyo kusaidia wanafunzi wa shule mpya ya Msingi Kakuni katika kijiji cha Kibaoni mkoani Katavi. Picha/ Aron Msigwa-MAELEZO.
↧
*WANAFUNZI WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YA SAYANSI.
Na. Jovina Bujulu –MAELEZO, Dar es salaam.
Wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi kote nchini wameshauriwa kuongeza bidii katika kujifunza masomo hayo ili kuendana na juhudi zinazofanywa na Serikali za kuwawezesha wanafunzi hao kujifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samweli Manyele kwenye sherehe ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2013 na 2014.
“Kama wachunguzi wa Serikali ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya Kemia na Biolojia tumeona ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa hili kupenda masomo ya Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.
Amesema Zoezi la kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na Biolojia limeanzishwa kutoakana na Wakala ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani.
Aidha, amesema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze kuimarisha vipaji vyao vya masomo na matumizi ya kompyuta .
Amefafanua kuwa Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule mbalimbali za Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali zikiwemo Fedha, Vyeti na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya Sayansi kwa upande wa wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za kufundisha masomo hayo.
Kwa upande wa Wanafunzi waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za Feza, Marian, Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanoro iliyoko jijini Mwanza.
Sherehe za kuwazawadia na kuwapa tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi zilianzishwa mwaka 2007 chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na utoaji wa zawadi na tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Bioloji.
↧
*TPB YAKABIDHI JENGO LA KITUO CHA AFYA PEMBA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud (Wanne kushoto waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Litice Rutashobya, (watatu kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanakijiji, mbele ya jengo la Kituo Cha Afya, Ungi, Shehia ya Msuka Mashariki, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya TPB kukabidhi jengo hilo kwenye hafla iliyofanyika Sptemba 17, 2015. Kituo hicho kimekamilishwa ujenzi wake na TPB.
Waziri Abloud, akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa kituo hicho. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Letice Rutashobya, (katikati mwenye miwani) na Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya shirika wa TPB, Noves A. Moses
Waziri Aboud, (wapili kulia), Profesa Letice Rutashibya, (wapili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (kulia) na Mbunge wa jimbo la Konde, Khatib Suleiman Haji, wakibadilishana mawazo mara baada ya ufunguzi wa jengo hilo la Kituo cha Afya
↧
*BALOZI IDDI AZINDUA JENGO JIPYA LA SHULE YA KIJIJI CHA MOGA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Moga mara baada ya kuzindua jengo Jipya la Skuli ya Kijiji hicho la madarasa Manne lililojengwa kwa nguvu za wananachi wenyewe.
Balozi Seif akipokea Risala ya Wananchi wa Kijiji cha Moga Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la skuli ya Moja. Picha na –OMPR – ZNZ.
*******************************************
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza wanafunzi Nchini kuongeza bidii katika kujifunza masomo yote na kutilia mkazo zaidi masomo ya Sayansi na Teknolojia ambayo ndio yenye nafasi kubwa katika harakati za kila siku kwenye karne hii ya Sayansi.
Alisema katika kuhakikisha juhudi hizo zinafanikiwa, walimu nao wana jukumu kubwa la kujiendeleza kwa kuwa tayari kujifunza mambo mbali mbali yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Wazazi, Walimu na Wanafunzi wa Kijiji cha Moga baada ya kulifungua jengo jipya la Madarasa Manne la Skuli ya Msingi Moga iliyopo Wilaya ya Kaskazini “ A ” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema Walimu wanahitaji kupatgiwa msaada mkubwa kutoka kwa Wazazi pamoja na wadau wa Maendeleo katika Sekta hiyo ili skuli zote za hapa Nchini ziweze kupata mafanikio makubwa zaidi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba juhudi zaidi zitaendelea kuchukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuzipatia Skuli vifaa na nyenzo za Kisasa za kufundishia kama vitabu, vifaa vya Maabara, Komyuta na walimu waliobobea katika fani tofauti ili wanafunzi wawe na uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.
Alisema Serikali inatambua kuwa mafanikio ya kweli katika utekelezaji wa Mipango ya Taifa inategemea jitihada za pamoja kati ya Serikali nyenyewe na washirika wa maendeleo wakiwemo Wananchi katika kuimarisha Elimu Nchini.
Alisema kwamba Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali itaendeleza kutekeleza dhamira yake ya kuifanya Elimu inayotolewa ianzie katika ngazi ya maandalizi hadi Sekondari.
Balozi Seif alifahamisha kwamba lengol ni kuihakikisha kuwa wanafunzi wote wanaweza kupata elimu ya lazima ya miaka 12 kuanzia maandalizi hadi Kidato cha Nne sambamba na kuongeza upatikanaji wa nafasi za kusomea.
Alieleza kuwa Wazazi na walezi hawana budi kuendeleza kwa pamoja utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo katika kuimarisha Taasisi za Uongozi na uendeshaji wa sekta ya Elimu pamoja na kuona rasilmali zilizotengwa kwa ajili ya Sewkta ya Elimu zinatumika kwa ufanisi na kwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza juhudi zinazochukuliwa na Kamati za Skuli Nchini kwa kazi kubwa zinazofanya za kusimamia na kusaidia shughuli za uendeshaji wa Skuli zao.
Balozi Seif aliahidi kwamba Serikali itaendelea kuziimarisha Kamati za Maskuli ili zitekeleze majukumu yake inazojipangia kwa ufanisi mkubwa zaidi kwa vile Maendeleo yoyote ya elimu yanahitaji msukumo wa pamoja kati ya Serikali na wadau wake.
Aliiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuweka mpango wa kuajiri walimu walio katika maeneo wanayoishi hatua ambayo mbali ya kupunguza gharama za nauli kwa walimu lakini pia itawapa utulivu wanafunzi kuwa karibu na walimu wao kwa muda mrefu.
Katika kuunga mkono juhudi za Wananchi hao wa Kijiji cha Moga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliahidi kusaidia matofali elfu 2,000 kuchangia ujenzi wa jengo jipya lililoanza kujengwa kwa nguvu za Wananchi wenyewe.
Balozi Seif pia akaahidi kusaidia Kompyuta moja na Printa yake kwa lengo la kuwajengea mazingira bora wanafunzi wa skuli hiyo ya msingi ya Moga kusoma katika mfumo wa kisasa wa sayansi na teknolojia.
Akitoa Taarifa za ujenzi wa jengo hilo Diwani wa Wadi ya Gamba Ndugu Machano Fadhil Babla alisema uamuzi wa Wananchi wa Kijiji cha Moga wa kuongeza jengo jengine la Skuli umekuja kufuatia matatizo mbali mbali yaliyokuwa yakiwapata Watoto wao kufuata elimu masafa marefu ya Mkwajuni.
Nd. Babla alisema watoto wa Kijiji cha Moga walikuwa waki9ata elimu chini ya Miembe, Madrasa za Quran pamoja na Majengo ya Chama cha Mapinduzi jambo ambalo lilikuwa haliwapi utulivu watoto hao katika masomo yao.
Diwani huyo wa Wadi ya Gamba ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A” aliishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kusaidia ujenzi huo katika hatua za awali licha ya kwamba Wizara hiyo ndio mkamilishaji wa majengo yote ya skuli yanayoanzishwa na Wananchi.
Ndugu Babla alisisitiza kwamba katika kwenda na wakati Kamati ya Skuli, Walimu na Wazazi wa Kijiji cha Moga wameamua kuendelea na ujenzi wa jengo jengine Jipya litakalokuwa na madarasa Manne, Maktaba pamoja na Ofisi ya Mwalim Mkuu.
Akitoa salamu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Mwanaid Saleh aliwapongeza Wananchi wa Wadi ya Gamba kwa uamuzi wao wa kuiunga mkono Wizara ya Elimu katika ujenzi wa Majengo mbali mbali ya Skul.
Bibi Mwanaid alisema hatua hiyo ya maendeleo inayofaa kuigwa na Wadi nyengine hapa Nchini imelenga katika kuwaondoshea changamoto za kupata elimu watoto wa Taifa hili.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu alilishukuru shirika la Maendeleo la Sweden { SIDA } kwa juhudi zake za kusaidia gharama za kukamilisha ujenzi wa jengo hilo licha ya kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Sekta ya Elimu hapa Zanzibar.
Ujenzi wa Jengo jipya la madarasa Manne la Skuli ya Moga lililojengwa kwa nguvu za Wananchi na kuunga mkono na washirika wa maendeleo wa sekta ya elimu hadi kukamilika kwake limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 50,000,000/-
↧
↧
*KUTOKA UWANJA WA TAIFA, YANGA WANAONGOZA MABAO 2-1, SASA NI KIPINDI CHA PILI
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, akiruka kushangilia bao lake alilofunga katika dakika ya 30 kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi ya JKT Ruvu kwenye mchezo unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa,
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, akimiliki mpira katikati ya wachezaji wa JKT Ruvu.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga.....
↧
*YANGA YAENDELEZA DOZI YAWAHENYESHA MAAFANDE WA JKT RUVU 4-1 TAIFA
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga ya jijini Dar es Salaam na JKT Ruvu, umemalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, huku wakiibuka na ushindi wa mabao 4-1. Mabao ya Yanga yalifungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 30, Amis Tambwe dakika ya 48 na 60, Thaban Kamusoko, dakika ya 87. Bao la kufutia machozi la JKT Rubu lilifungwa na Naftali Nashon katika dakika ya 50.
Huko katika viwanja vingine, MBEYA CITY 0- TANZANIA PRISONS 1- Uwanja wa Sokoine Mbeya
STAND UNITED 2- AFRICAN STARS 0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga
MGAMBO JKT 2- MAJIMAJI 0 - Uwanja wa Mkwakwani
Thaban Kamusoko, akipongezwa na kocha wake baada ya kufunga bao la nne, katika dakika ya 87
Simon Msuva wa Yanga, akiruka daruga la beki wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhan
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akimenyana na beki wa JKT Ruvu, Napho Zuber
Beki wa JKT akiruka kuokoa hatari
Mshambuliaji wa Yanga, Godfrey Mwashiuya, akiruka kukwepa kwanja la beki wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhan
Msuva wa Yanga (kulia) na beki wa JKT Ruvu wakiwania mpira
Mshambuliaji wa Yanga, Godfrey Mwashiuya, akiwakimbiza mabeki wa JKT Ruvu.
Kipa wa JKT Ruvu, Tony Kavishe, akigagaa chini huku akiuangalia mpira ukitinga wavuni, na kufungwa bao la Nne lililofungwa na Thaban Kamusoko katika dakika ya 87.
Kocha wa Yanga, akitoa maelekezo kwa Nahodha wake, Nadir Haroub 'Canavaro'.
↧
*LOWASSA ALIVYOPOKELEWA MJINI BUKOBA
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mmoja wa wadau wa Mabadiliko, Prof. Azaveli Rwaitama, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015. Mjini Bukoba, Mkoani Kagera jana Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimpongeza Mke wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Bukoba.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza na baadhi ya vingozi, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi, Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera.
Wananchi wa Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera wakimshangilia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye eneo la Mkutano.
↧
*MGOMBEA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU (CCM) YUSUF MANJI AZINDUA KAMPENI ZAKE DAR ES SALAAM
Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia (kulia), akimtambulisha Yusuf Manji katika uzinduzi huo.
Kiongozi wa Kamati ya Ushindi kwa CCM kutoka Kigoma, Nicholaus Zacharia, akihutubia katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Mchumi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Urio akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Kada wa CCM, Godbertha Kinyondo akisalimia wananchi kwenye uzinduzi huo.
Makada wa CCM wakiserebuka
Vijana wa hamasa wa CCM wakiwa kazini.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Michango mbalimbali ikitolewa.
Umati ukimsikiliza Yusuf Manji.
Mkazi wa eneo hilo, Sharifa Ali akimueleza Manji kuhusu kero ya kutokuwa na soko.
Dogo akihubia kwenye uzinduzi huo. Dogo huyo alisema wana CCM wanapaswa kumchagua Magufuli kuwa Rais, Mbunge Mangungu na Diwani Manji.
Chipukizi wakifanya vitu vyao.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Yusuf Manji (kulia) akifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
↧
↧
*KUTOKA UWANJA WA TAIFA SIMBA WANAONGOZA BAO 2-1 SASA NI KIPINDI CHA PILI
Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza, akishangilia bao lake aliloifungia timu yake katika kipindi cha kwanza na katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili Kiiza ameipatia timu yake bao la pili. Katika dakika ya 48, Mbaraka Yusuph, anaipatia Kagera Sugar bao la kwanza
Wachezaji wa Simba, wakishangilia bao la Kiiza.
Hamis Kiiza akibanwa na mabeki wa Simba
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la timu yao....KAA NASI KWA MATOKEO KAMILI YA MECHI HII HAPO BAADAYE.
↧
*SIMBA WAIKALISHA KAGERA SUGAR 3-1, HAMIS KIIZA ANG'ARA
Beki wa Timu ya Kagera Sugar, Deogratius Julius, akiruka kuokoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Kiiza, katika dakika za 30, 46 na 90+, huku bao la kufutia machozi la Kagera Sugar likifungwa na Mbaraka Yusuph katika dakika ya 50.
Kutoka katika Viwanja vingine
AZAM FC, 1 (John Bocco) - MWADUI 0, Uwanja wa Mwadui Complex
MTIBWA SUGAR 2 (Salim Mbonde, Saidi Bahanuzi) - NDANDA FC 1 (Kigi Makasy), Uwanja wa Manungu
COASTAL UNION (0) - TOTO AFRICAN (0) Uwanja wa Mkwakwani Tanga
Beki wa Kagera Sugar, Said Hassan, akiwania mpira na Emery Nibomana...
Nahodha wa Simba, George Kavilla, akimiliki mpira kumdhibiti mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib.
Ibrahim Hajib, akipiga mpira katikati ya mabeki wa Kagera Sugar..
Ibrahim Hajib wa Simba, akiruka kukwepa kwanja la beki wa Kagera Sugar, Salum Kanoni...
Salum Kanoni wa Kagera Sugar (kulia) akiwania mpira na Peter Mwalyambi
Kocha wa Simba, akitoa maelekezo kwa Hamis Kiiza.
↧
*PRESIDENT KIKWETE BRIEFS MEMBER STATES IN NEW YORK
The Chairman of the UN High level panel on Global Response to Health Crises President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete briefs delegates of member states during a consultative session in New York over the weekend.
During the briefing President Kikwete told the delegates that the panel is progressing well in compiling the report that will be tabled in December this year and asked them to make relevant contributions that will be useful.
The Secretary-General has asked the Panel to make recommendations to strengthen national and international systems to prevent and manage future health crises, taking into account lessons learned from the response to the outbreak of Ebola virus disease.
In carrying out its work, the Panel will undertake a wide range of consultations, including with representatives from the affected countries and communities, the United Nations system, multilateral and bilateral financial institutions and regional development banks, non-governmental organizations, countries supporting the response effort, other Member States, health-care providers, academic and research institutions, the private sector and other experts. The Panel will be supported by a Resource Group of leading experts which is to provide advice to the Panel on technical and other issues.
The Panel held its first meeting in early May 2015 and is expected to submit its final report to the Secretary-General at the end of December 2015. The Secretary-General will make the report available to the General Assembly and undertake further action as appropriate.
In the pictures President Kikwete with Other panel members include Celso Amorim from Brazil, Micheline Calmy Rey from Switzerland, Marty Natalegawa from Indonesia, Joy Pumaphi from Botswana and Rajiv Shah from the US.(Photo by Freddy Maro)
↧
*MAGUFULI ALIVYOITEKA CHATO JANA JIONI KATIKA MKUTANO WAKE WA KAMPENI
Wakazi wa Chato wakishangilia kuonesha kuwa watampa kura za ushindi Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato, mkoani Geita.![]()

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo mkubwa wakati akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mbele ya wakazi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato, mkoani Geita. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
Wakazi wa Chato ilkuwa ni shangwe tu kila kona ya uwanja.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ,Joseph Kasheku almaarufu King Msukuma akiwaomba ridhaa wananchi wa Chato ya kumchagua Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli ili aweze kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano.
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato, mkoani Geita.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, mkoani Geita.
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano,pichani kati anaeshuhudia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Chato mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato, mkoani Geita.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.
Sehemu ya maelfu ya wananchi katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari mkutano wa kampeni
Sehemu ya maelfu ya wananchi katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari mkutano wa kampeni. Picha na Ahmad Michuzi Jnr.
↧
↧
*MKUTANO WA NNE WA BARA LA AFRIKA KUJADILI MIPANGO ENDELEVU NA MAFUNZO KUANZA KUFANYIKA LEO HOTELI YA GIRRAFE JIJINI DAR
Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco Tanzania ,Celestine Kharkongor (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Don Bosco Oyterbay jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano huo na shughuli zinazofanywa na Don Bosco hapa nchini.
Meneja Mipango wa Ofisi ya Maendeleo Don Bosco Tanzania, Rosemarytery Njoki (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco Tanzania ,Celestine Kharkongor, Mratibu wa Don Bosco, Maika Denys na Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Don Bosco, Maika Denys (kulia), akichangia jambo.
Mwalimu wa Don Bosco, Hellen Jackson (kulia), akielezea mafanikio makubwa wanayopata wanafunzi katika shule hiyo.
Ofisa Mwezeshaji Aira wa Don Bosco Tanzania, Oswald Manyerere (kushoto), akielezea jinsi Don Bosco ilivyofanikiwa kuwatafutia ajira wanafunzi wao waliohitimu mafunzo mbalimbali. |
Mkuu wa Idara ya Utafuta wa ajira na Ofisa Masoko, Don Bosco Dar es Salaam, Nyerembe Yunus Nyampiga (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. |
Mmoja wa wanafunzi wa DonBosco akielezea mafanikio wanayopata shuleni hapo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanafunzi na walimu wao wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanafunzi wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Viongozi wa Don Bosco wakiwa meza kuu.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari na Wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo. |
Na Dotto Mwaibale, Dar
MKUTANO wa Nne wa Bara la Afrika wa kujadili mipango endelevu katika eno la mafunzo kwa vijana na wataalamu wasiojiweza na ushirikji wao katika soko la ajira, unatarajiwa kuanza kufanyika kesho Hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ambao utashirikisha nchi mbalimbali tisa unatarajiwa kuhudhuriwa na wageni 50 kutoka katika nchi hizo za Afrika.
Akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu Dar es Salaam jana kuhusu mkutano huo, Meneja Mipango wa Ofisi ya Maendeleo Don Bosco Tanzania, Rosemarytery Njoki alisema, mkutano huo utatoa nafasi kwa Mtandao wa Don Bosco Afrika kuchunguza njia ambazo zitaleta ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na umma ili kuleta maendeleo zaidi.
“Mkutano unatarajiwa kutafakari juu ya mipango inayoendelea katika eneo la mafunzo ya kijamii na wataalamu vijana wasiojiweza na ushiriki wao katika soko la ajira. Kama vile namna bora ya washirika wanaweza kufanya kazi na binafsi na ya umma sekta kuelekea maendeleo endelevu,” alisema Njoki.
Alisema mkutano huo pia utazungumzia masuala ya jinsia hasa kwa upande wa upatikanaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kuwafanya wanawake kuwa sawa na wanaume kwa kufanya kazi sawa.
“Pia tunatafuta kubadilishana uzoefu na washirika weu wa Afrika ambao wote tunafanya kazi ili kuboresha elimu, masuala ya mafunzio ya ufundi stadi na kuwaunganisha vijana na masoko ya ajira ya dunia,” alisema.
Alisema kwa mara ya kwanza mkutano huo unafanyika nchini kuanzia leo hadi Septemba 25, utakuwa ni kwa ajili ya ushirikiano wa sekta binafsi na umma. Alisema mkutano huo pia utawakutanisha shirikisha watu mbalimbali ikiwemo taasisi za serikali na chuo cha VETA.
Kwa upande wake Meneja Mipango wa Don Bosco, Bram Reekmans alisema, mkutano huo pia utatumika kuangalia njia ambazo Don Bosco inaweza kutumia kushirikiana zaidi na sekta binafsi kama sehemu ya mipango endelevu.
Alisema majadiliano mengine yatakuwa yanahusu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi namna ya kushirikiana ili kuboresha elimu.
Ofisa Mwezeshaji Aira wa Don Bosco Tanzania, Oswald Manyerere alisema, lengo la mafunzo yanayotolewa na tasisi hiyo ni kuhakikisha wanawawezesha vijana wasiojiweza kupiga hatua na hatimaye kufikia malengo waliyojiwekea.
Alisema vijana wanaopitia katika chuo hicho wamekuwa wakitafutiwa kazi baada ya kufanya mafunzo yao, ambapo kwa kipindi cha mwaka jana vijana waliomaliza walikuwa ni 322 na hadi sasa waliopatiwa kazi ni 220 huku idadi kubwa ikiwa ya wasichana sawa na asilimia 86.
Alisema wanafunzi hao ni kutoka katika shule zilizochini ya Don Bosco, Dodoma, Iringa na Oyterbay Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco,Celestine Kharkongor alisema Don Boscow ilianza hapa nchini mwaka 1996.
Alisema tangu kuanzishwa kwa chuo cha Don Bosco kimeleta mabadiliko ya tabia kwa vijana pamoja na kuwakwamua kiuchumi.
Mwalimu wa Don Bosco, Hellen Jackson alisema mafunzo yanayotolewa na chuo cha Don Bosco yatasaidia kutoa ajira kwa vijana na kuondoa changamoto zilizopo sasa za ukosefu wa ajira hapa nchini.
Alisema wazazi wenye watoto wa kike ni fursa kwao kuwapeleka katika chuo hicho.
↧
*WANAFUNZI WANUSURIKA KUFA KWA KUGONGWA WAKIWA NDANI YA BAJAJI DAR
Mwanafunzi wa Sekondary ya Loyola akipelekwa kwenye gari kuelekea Hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana mchana, baada ya Bajaj yenye namba za usajili MC 402 AWD waliokuwa wameikodi na wenzake Bandarini wakitokea Zanzibar kugongwa na Pickup Double Cabin yenye namba DFPA 826 katika makutano ya barabara ya Sokoine na Azikiwe jirani na Benki ya NBC. Katika ajali hiyo wanafuzi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali hiyo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakimfariji mwenzao Martha Silayo (katikati), aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Wananchi wakiangalia bajaj iliyogongwa. Imeelezwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali wa bajaj hiyo ambapo pia dereva wake alijeruhiwa.
Askari wa usalama barabarani na wananchi wakiwa eneo ilipotokea ajali hiyo.
Bajaj iliyogongwa ikiwa eneo ilipopatia ajali 'Kweli BOGOTI imegongwa'
↧
*DKT.BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA KUWEKWA WAKFU ASKOFU KENEN PANDA MBEYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani humo jana kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini, Mchungaji Kenan Salim Panja, zilizofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Wasanii wa kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenen Salim Panja iliyofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na kumpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim Panja, wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa hilo Mchungaji Kenan Salim Panja, iliyofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Kenen Salim Panja baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu huyo iliyofanyika katika Uwanja wa michezo Tukuyu Mkoani Mbeya.
↧