Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA BALOZI WA UHOLANZI NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
***************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itazidi kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Uholanzi hasa katika sekta ya kilimo, elimu na uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji ili kufikia lengo la Tanzania ya Viwanda.
Aidha, Mhe.Balozi aliahidi kuwa mjumbe mzuri wa Tanzania na atarejea mara kwa mara kuja kutembea kwani Tanzania ina watu wema na vivutio vingi vya utalii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA MISRI PIA AKUTANA NA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Rais huyo wa Misri ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza nyimbo za kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

BAADA YA SIMBA, YANGA, EVERTON. Sport Pessa wamekuja na hii hapa.

$
0
0




Rafiki Bonus ilivyokuja na mkakati wa kusaidia masikini. 
*************************************************************
Unatamani Kuvuna Buku Mbili Kwa Kila siku? Kampuni inayojishughulisha na soka ya Sport Pesa itakusaidia kufanya hivyo kupitia mchezo wake mpya wa Rafiki Bonus.
Rafiki unayemualika kucheza na Sportpesa? Hizi Ndizo Hatua Zenyewe. Huenda ukawa umesikia au kuona kuhusu promosheni ya RAFIKI BONUS kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa na ukawa umeshajiuliza sana kuhusiana na promosheni hii na jinsi inavyofanya kazi lakini mwisho wa siku ukaishia kukosa majibu sahihi au majibu ya kukidhi.Hakuna haja ya kuumiza kichwa tena kwani Makala hii ina lengo lakukuelewesha hatua kwa hatua kuhusiana na promosheni na RAFIKI BONUS hivyo twende sambamba.
Rafiki Bonus ni nini? Rafki Bonus ni promosheni kutoka kampuni ya SportPesa ambayo ina lengo la kukuzawadia Shilingi 2000 za kitanzania wewe mteja wa SportPesa kwa kila rafiki yako unayemualika kujisajili na kucheza na SportPesa.
Hii ni sawa sawa na kusema kuwa kwa kila rafiki unayemualika kujisajili na SportPesa halafu rafiki yako huyo akaweka ubashiri wake basi wewe uliyemualika utakuwa umejipatia Sh 2000.
Hivyo kwa mahesabu ya harakaharaka kuwa kama ukiweza kualika marafki 10 kwa siku moja wakajiunga nakuweka ubashiri wao utakuwa ina maana utakuwa umepata Sh 20,000/=Sasa umeshajua Ra)ki Bonus ni nini hivyo bila shaka utakuwa na shaukukubwa ya kutaka kujua jinsi ya kumualika rafiki yako ili uweze kujivutiamkwanja huo. Wala usiwe na haraka, twende sambamba.
Jinsi ya Kumualika rafikiKama wewe ni mteja wa SportPesa ambaye unaweka utabiri wako mara kwamara angalau mara moja ndani ya mwezi mmoja basi ni rahisi sana kwakokwasababu unachotakiwa kuanza kufanya ni kumshawishi rafiki yako kujisajili na akikubali kufanya hivyo basi unachotakiwa kufanya ni:1.
Hakikisha ra)ki yako anajisajili na kuwa mteja wa SportPesa kamaulivyo wewe kwa kuingia kwenye uwanja wake wa SMS na kutumaneno RAFIKI kwenda 15888 ambapo atatumiwa ujumbe mfupi kutoka SportPesa utakaomtaka atume neno KUBALI likifuatiwa na namba yako wewe ya simu kwenda 15888.

TONY ELUMELU: HUMAN TRAFFIC IS EVIL,IT STRIPS OUR OUR YOUTH OF DIGNITY AND DENIES THEM OPPORTUNITY

$
0
0
Group CEO, United Capital Plc. Oluwatoyin Sanni (left); Founder, The Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu; and Director General of NAPTIP, Julie Okah-Donli during the visit of DG to the foundation in Lagos on Thursday; 
Tony Elumelu: Human Trafficking Is Evil, It Strips Our Youth Of Dignity And Denies Them Opportunity
***********************************************
Tony Elumelu Foundation commits to support National Agency for the Prohibition of Trafficking in Persons (NAPTIP).
In recognition of the growing concerns around human trafficking in Africa, The Tony Elumelu Foundation (TEF), an African founded and funded 21st century philanthropic organization committed to youth empowerment and entrepreneurship development, hosted the Director General of Nigeria’s National Agency for the Prohibition of Trafficking in Persons (NAPTIP), Julie Okah-Donli.
According to Okah-Donli, UNESCO ranks human trafficking as the third most lucrative criminal enterprise in Nigeria. Thus, agencies like NAPTIP need good laws, sustained funding and equally important, critical support from local and global stakeholders to execute the urgent war against human trafficking. “We can no longer wait for government alone to fight this war. Many victims are on standby, anxious to be fully reintegrated into society. At the agency, we are desperate for assistance to empower and rehabilitate these millions of victims in need. Thus, we are identifying and approaching organizations like the Tony Elumelu Foundation (TEF) for support.”
She continued: “We need to refurbish and rehabilitate our existing shelters, facilitate periodic provision of food, clothing and medical consumables and shelter for victims. We also need assistance in the development of standard skills’ acquisition centres in strategic locations for the training of vulnerable persons, as well as rescued victims.”
In response, Mr. Tony Elumelu CON, Founder, Tony Elumelu Foundation, commended Okah-Donli for her accomplishments at the agency, including the conviction of over 325 persons, and successful rehabilitation of more than 12,000 victims. He also added that she was a former staff of leading pan-African bank, United Bank for Africa (UBA). “She is an alumna of the United Bank for Africa (UBA), Africa’s global bank, thus we are not surprised at what she has become. We predicted that she will attain such great heights because of the passion she has always had for human trafficking,” he said
On behalf of the Foundation, he pledged commitment to the war against human trafficking. “We support what you are doing and we stand behind you. The Tony Elumelu Foundation believes in the empowerment of our youths and as we all know, they cannot be empowered if they are not free.” “We stand with you in eradicating human trafficking in Nigeria and will engage extensively with you as you work to restore dignity to mankind, protect the dignity of our youth and ensure no one can take undue advantage of them.”
He also made an appeal to the government to increase budgetary funding to the cash-strapped agency. “I call on the Federal Government to make more resources available to support you. As private companies, we pay taxes to the Federal Government and we want to see a more judicious use of the taxes paid.”
Elumelu also urged other private sector players to join the agency to fight human trafficking, assuring them of the credibility and competency of NAPTIP and its DG whom he could vouch for. “If she succeeds, we will all succeed. Let us come together to make sure our youth, our future leaders, are not trafficked.”

KESI YA WEMA SEPETU KUJULIKANA AGOSTI 18 MWAKA HUU

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imweka wazi kuwa Agost 18 mwaka huu itatoa uamuzi kama kielelezo cha msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vipokelewe mahakamani hapo kama kielelezo vya kesi inayomkabiri Wema Sepetu ama la. 
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya majibishano makali kuhusu kielelezo kutoka upande wa utetezi na ule wa mashtaka.
Kielelezo hicho cha bangi kinataka kutolewa katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kumuongoza shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima kuendelea kutoa ushahidi wake.
Katika ushahidi wake, shahidi huyo amidai kuwa alipima msokoto huo na vipisi hivyo vya bangi vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi.
Mbali na mambo mengine, shahidi Mulima kupitia Kakula aliomba kuitoa kielelezo cha bangi kikiwa ndani ya bahasha iliyofungwa ikiwa na muhuri juu, na kama kielelezo cha ushahidi lakini wakili wa utetezi Tundu Lissu alibisha vikali na kusema, upande wa mashtaka ulisema unataka kutoa bangi lakini sasa wanatoa bahasha.
Wakili Lissu alipinga na kusema, ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.
Alidai Lissu vipisi viwili vyenye majani ukiviangalia kwa makini ni vipisi vya sigara za kienyeji ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua ambavyo kwao vinaitwa twagooso.
Baada ya mabishano makali baina ya pande hizo mbili, Hakimu Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18, kwa ajili ya uamuzi kama bangi hiyo ipokelewe au la.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA

$
0
0

           Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi hilo.
************************************
 


RAILA ODINGA ATANGAZA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

$
0
0

Na: Shisia Wassilwa, DW, Nairobi


Kiongozi wa upinzani Kenya, Raila Odinga, asema upinzani hautakubali haki za Wakenya kukandamizwa na kwamba wataonyesha jinsi uchaguzi ulivyochakachuliwa. Upinzani utafungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.
Zikiwa zimepita siku nane tu baada ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Kenya, Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya - NASA, umetoa tamko lake kwa vyombo vya habari jana.
Muungano huo tangu mwanzo ulikuwa ukishikilia msimamo wake kuwa uchaguzi huo haukuwa huru, haki na wazi. Tume ya kusimamia uchaguzi bado inasubiri kupokea fomu za uchaguzi juma moja baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.
Muungano mkuu wa upinzani unadai kuwa tume hiyo imechelewesha kuwakabidhi karatasi hizo kwa sababu inazichakachua ili zionekane ni sambamba na matokeo iliyotangaza kuwa Rais Kenyatta alimshinda Odinga kwa kura milioni 1.4. Muungano huo ukikataa kumtambua Kenyatta kuwa rais mteule. Odinga amesema kuwa hawatakubali matokeo hayo hadi tume ya kusimamia uchaguzi iyajibu masuala ambayo wameyaibua.
NASA imeelezea kuwa wangekubali uhalali wa matokeo hayo iwapo wangepatiwa fomu za uchaguzi za kuonesha kuwa matokeo yale ni sawa na yale yaliyotangazwa na tume ya kusimamia uchaguzi. Tume hiyo bado haijatoa fomu 34A elfu 10 za uchaguzi huo kwa umma. Odinga aliyeonekana mtulivu amewasuta wote ambao wamekuwa wakitaka akubali ushinde wakiwemo waangalizi wa kimataifa.



*UN yasema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki

Muungano huo wa upinzani sasa unadai kuwa serikali inaharamisha na kuyatisha mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini ili kuyazuaia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi. Mashirika hayo yanadai kuwa mchakato mzima wa uchaguzi huo ulikosa uwazi na haki. Maafisa wa polisi walivamia shirika la uongozi bora la AFRICOG leo asubuhi, japo lengo la uvamizi wake halifahamiki. Hata hivyo, serikali imeyapa mashirika hayo siku tisini kutimiza masharti ya kisheria.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema kuwa uchaguzi huu uliendeshwa kwa njia huru na haki na kusema kuwa rais Kenyatta alimshinda Odinga. Ombi la Odinga la kutaka Umoja huo kutathmini matokeo ya uchaguzi wa tarehe nane, lilikataliwa. Matamshi kama hayo yakitolewa na Rais wa Marekani Donald Trump aliyewataka Wakenya kudumisha amani utulivu na kusuluhisha utata wao mahakamani.
Uamuzi huo umeafikiwa na kikao cha muungano huu kilichojumuisha vinara wake, wataalamu wa kifundi, wataalamu wa masuala ya sheria, katiba na uongozi pamoja na viongozi wa kada mbali mbali wa muungano huo.
Hata hivyo muungano wa NASA haukutoa ushahidi uliokuwa nao kwa wanahabari kwa hofu ya kumwaga mtama mbele ya kuku wengi. Tamko la leo la Odinga ni nafuu kwa Wakenya wengi ambao walidhani kuwa angeitisha maandamano. Yeyote anayepanga kupinga matokeo ya urais ana hadi siku ya Ijumaa kufanya hivyo kwa mujibu wa katiba. Macho yote sasa yanaelekezwa katika idara ya mahakama kuona jinsi itakavyoamua. Mwaka 2013, Mahakama ya Juu ilitupilia mbali kesi iliyowasilishwa na upinzani kupinga matokeo ya urais ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUBADILIKA

$
0
0
 Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chote ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi,Rukwa na Kigoma akisisitiza  jambo kwa washiriki hao wakati akifunga mafunzo hayo.
 Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka PS3 bw. Desderi Wengaa akizungumza wakati wa hafla ya Kufunga mafunzo hayo.
 Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akizungumzia umuhimu wa mfumo huo katika kuleta mageuzi ya kiutendaji kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi,Rukwa na Kigoma.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza muda mfupi kabla ya Hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika Mjini Kigoma. Picha na Frank mvungi-Maelezo
**********************************************
Frank Mvungi - Maelezo
Serikali imewataka watumishi wa umma katika mikoa na Halmashuri kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mabadililko ya mifumo yanayofanywa kwa kushirikina na wadau wa maendeleo.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuandaa mipango,bajeti na kutoa ripoti yaliyowashirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Katavi, Rukwa na kigoma ,Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Dkt. Paul Chote amesema dhamira ya serika ni kuwawezesha watumishi wake kutekelza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika kuwahudumia wananchi.
“Mfumo huu sio wa majaribio hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kurudi katika mkoa na halmashuri na kuhakikisha kuwa anajenga uwezo kwa watumishi ambao hawakushiriki katika mafunzo haya kwa kuwa mfumo huu unahitaji uwajibikaji wa pamoja” alisisitiza Chote.
Akifafanua Dkt. Chote amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa lakutumia weledi na ujuzi waliopata kuleta mageuzi chanya katika maeneo yao ili azma ya serikali kutoa huduma bora itime.
Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Lisa Rwamiago amesema kuwa vituo zaidi ya elfu 22,000 vya kutolea huduma vitaunganishwa katika mfumo huo wa Kitaifa hali itakayofanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika kwa kuwa na mifumo bora yakutolea huduma.
“Nashukuru PS3 kwa ushirikiano uliopo kati yake na TAMISEMI na umewezesha kutekelezwa kwa miradi yenye tija hasa kwa wananch”.Alisisitiza Rwamiago
Akifafanua Rwamigo amesema kuwa watumishi katika Mikoa na Halmashuri lazima waoneshe kwa vitendo namna tofauti ya kutekelza majukumu yao kwa kutumia mfumo huo wa kielektroniki ulioboreshwa ambao ni (web based).
Mradi wa PS3 unalenga kushirikiana na Serikali katika kuboresha matumizi ya rasilimali zilizopo ikiwemo fedha, rasilimali watu na mifumo katika ngazi ya kutolea huduma kama vile vituo vya Afya,Zahanati,Hosipitali na katika sekta ya elimu.

Kutokana na maboresho na kurahisishwa kwa Teknolojia,mfumo huu mpya wa PlanRep umefanywa kuwa ‘web based’ hivyo utawezesha Halmashuri kuingiza taarifa za Mipango na Bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kuweza kutumwa kwenye mfumo mmoja uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI na hatimaye kuingizwa kwenye bajeti kuu ya mwaka husika.

MSIPOTUMIA FURSA ZILIZOPO TANGA WAGENI WATAZITUMIA: DKT. MWAKYEMBE

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongeza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Martin Shigela akitoa neon la utangulizi wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga
 Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers Dkt. Jim Yonaz akielezea kuhusu malengo ya kongamano la Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
******************************************
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakazi wa na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kuanza mapema kuzitumia fursa zilizopo katika mkoa huo kabla ya wageni hawajazitu,ia na kuwaacha wenyeji kuwa watazamaji.
Waziri Mwakyembe ametoa rai hiyo leo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la siku moja la Fursa za Biashara ambalo lina lengo la kufungua fursa za biashara zilizopo katika mkoa na hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga unatarajiwa kuanza.
“Tusipojipanga leo na kuzitumia vizuri hizi fursa nyingi zilizopo basi tujue fursa hizi zitatumiwa na wageni ili hali Watanzania tunaauwezo”, alisisitiza Waziri Mwakyembe.
Alieleza kuwa kama kuna changamoto zozote zinazowakabili watu wa Tanga na Watanzania kwa ujumla katika kutumia fursa zilizopo basi ni vema Serikali ya Mkoa, wafanyabishara na wawekezaji waliopo mkoa wa Tanga wakazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili zigeuke kuwa fursa ili Watanzania wazichangamikie.
Aidha Mwakyembe amewasisitiza Watanzania kuwekeza katika biashara ya huduma na viwanda vya uzalishaji bidhaana bidha ambapo vitakuwa vikihudumia ujenzi wa miradi mbalimbali hususani bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanga, Tanzania.
Ameeleza kuwa hivi sasa kasi ya wageni kutaka kutumia fursa za bomba la mafuta imekuwa kubwa ambapo ameeleza kuwa kuna baadahi ya wafanyabiashara kutoka nchi jirani wamekuwa wakifanya ushawishi ili wafanyakazi na wataalamu watakaokuwa katika mradi wa bomba la mafuta wawe wanatumia huduma za hoteli za nchi hiyo.
Akiongea awali, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alieleza kuwa wananchi wa Mkoa wa Tanga wameendelea kujipanga kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa zilizopo Tanga kwa ajili ya kukukuza kipato na uchumi wa mkoa wa Tanga.
“Tumejiandaa vya kutosha na wakati ni sasa na hatuna sabababu za kuchelewa kutumia fursa zilizopo”, alieleza Mkuu wa Mkoa huku akitaja baadhi ya uwekezaji unaotarajiwa kufanywa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya cha Saruji, ujenzi wa hoteli, kilimo, upanuzi wa uwanja wa ndege na uimarishaji wa miundombinu ya reli na bandari.
Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Dkt. Jim Yonaz aliwataka wananchi na wafanyabiashara wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanakuwa na haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa za ukuaji wa uchumi wa mkoa ili wawe sehemu ya fahari ya kuirudisha Tanga ya viwanda kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Dkt. Yonaz alieleza kuwa kuwa TSN wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inashirikiana na Serikali ya mkoa kwa kutoa elimu kupitia magazeti ya Daily News na HabariLeo kutangaza fursa mbalimbali zilizopo mchini ili wananchi waweze kuzifahamu na kuzifanyia kazi.

Jukwaa la Fursa za Kibiashara linaloandaliwa TSN ni la kwanza kufanyika katika mkoa wa Tanga na la tatu kufanyika hapa nchini ambapo la Jukwaa la kwanza lilifanyika mkani Simiyu na lile la pili lilifanya mkoa wa Mwanza. Aidha kwa mujibu wa waandaji, jukwaa kama hili linatarajiwa kufanyika hivi karibuni Visiwani Zanzibar na baadae katika mkoa wa Arusha.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI AFRIKA YA KUSINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Mawasiliano wa Afrika ya Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo ambaye alimpokea mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pretoria.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika Kusini tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ( SADC) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 
**************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika ya Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaoaanza tarehe 19 na 20 ambapo kesho tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit). 
Mheshimiwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amepokelewa na Waziri wa Mawasiliano wa Afrika Kusini Mhe. Ayanda Dlodlo.
akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.
 Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augastine Mahiga amesema Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.   
Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi.  
Dkt. Mahiga amesema katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit)  Tanzania itakabidhi nafasi ya  Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.
Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam

DAWASCO KUANA ZOEZI LA KUKATA MAJI MWEZI HUU AGOSTI 14-19, 2017

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA JUU YA 
UBORESHAJI WA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI 
BAGAMOYO MKOANI PWANI. 

Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wateja wake wote wa Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Chini utakuwa kwenye maboresho kwa wastani wa siku 5, kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 14/08/2017 hadi 19/08/2017, hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo kuwa na upungufu wa kiwango cha huduma ya Majisafi. 
Sababu ya upungufu wa Majisafi: Maboresho ya Mtambo na mabomba makuu ya usafirishaji na usambazaji Maji. 
Maeneo yatakayoathirika: Mji Wa Bagamoyo Vijiji Vya Zinga, Mlingotini, Kilomo na Mapande. 
Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha kuepuka adha itakayojitokeza. 
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia: 
Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) au 
Dawati la huduma kwa wateja Dawasco Bagamoyo 0743 451 887 
www.dawasco.go.tz 

Imetolewa Na: 
Ofisi Ya Uhusiano 
Dawasco-Makao Makuu. TAARIFA KWA UMMA UBORESHAJI WA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI BAGAMOYO MKOANI PWANI. Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wateja wake wote wa Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Chini utakuwa kwenye maboresho kwa wastani wa siku 5, kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 14/08/2017 hadi 19/08/2017, hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo kuwa na upungufu wa kiwango cha huduma ya Majisafi. Sababu ya upungufu wa Majisafi: Maboresho ya Mtambo na mabomba makuu ya usafirishaji na usambazaji Maji. Maeneo yatakayoathirika: Mji Wa Bagamoyo Vijiji Vya Zinga, Mlingotini, Kilomo na Mapande. Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha kuepuka adha itakayojitokeza. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia: Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) au Dawati la huduma kwa wateja Dawasco Bagamoyo 0743 451 887 www.dawasco.go.tz Imetolewa Na: Ofisi Ya Uhusiano Dawasco-Makao Makuu.

WANA CCM WA KATA YA MZINGA KUKUTANA JUMAPILI

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzinga, Majaliwa (kulia) akipongezwa na mmoja wa Wanachama wa CCM baada ya kutangazwa kuchaguliwa kuwa nwenyekiti wa Kata hiyo, hivi karibuni
******************************************
Na Ripota wa Mafoto Bolg, Dar
MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mzinga wilayani Ilala, Dar es Salaam, unatarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii.

Katibu Mwenezi wa CCM wa kata hiyo Paul Kapotele, amesema wajumbe wameshataarifiwa kuhudhuria mkutano huo wa kuwatambulisha viongozi wapya pamoja na kuwashukuru wapigakura.

Alisema mkutano huo umepangwa kuanza saa 5:00 asubuhi katika ukumbi wa Mkwabi, ambapo pia viongozi wa zamani wa CCM na makada mbalimbali wamealikwa.
"Viongozi wapya tulichaguliwa Agosti 5 mwaka huu kwa hiyo tumeona ipo haja ya kuita tena Mkutano Mkuu ili kuwashukuru wapigakura kisha hapo tuanze kuchapakazi," alisema Kapotele.
Alisema malengo ya uongozi mpya ni kukipa ushindi Chama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2019 na uchaguzi mkuu.
"Baada ya kumalizika uchaguzi tuliangalia namna ya kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na wanachama ndio maana tumeandaa mkutano huu kwa lengo la kujenga," alifafanua Kapotele.
Alisema kuwa ana imani baada ya mkutano huo, CCM Mzinga itakuwa imara kufuatia upendo na umoja utakaojengeka miongoni mwa wanachama, viongozi na wapenzi wa Chama.
Katika uchaguzi huo, Kaimu Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mzalendo na Uhuru Wikiendi, Fred Majaliwa, alichaguliwa kuwa mwenyekiti kwa kuzoa kura 59 dhidi ya 28 alizopata Ignas Agustino ambaye alikuwa anatetea kiti hicho, huku Guruneti akipata kura tatu katika jumla ya kura 90 zilizopigwa.
Pia, wajumbe 37 wa Halmashauri Kuu walimchagua kwa kura 24 Emmanuel Ryoba Mkunyi kuwa katibu kata na kumwangusha Twaha Kisogo aliyepata kura 13, wakati Kapotele alirejea madarakani baada ya kuzoa kura 29 dhidi ya nane za Gaudencia Malongo.
Wajumbe waliochaguliwa kwenye Kamati ya Siasa ni Mayasa Subeya, Said Ndembo na Amos Chandala wanaoungana na wengine kwa nafasi zao katika chama na jumuia zake.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na  Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
******************************************************
Na Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amewaasa maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kuamsha ari ya kufanya kazi kwa wananchi ili kujiletea maendeleo.
Ameyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mkoani Iringa alipokuwa akifanya ziara kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii nchini.
Bibi Sihaba Nkinga ameongeza kuwa viongozi wa Halmashauri na Mikoa nchini wanatakiwa kuwapa nafasi Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kurejesha ari ya wananchi kujitolea katika kutekeleza shhughuli za kimaendeleo katika maeneo yao.
“ Nawaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mtimize majukumu yenu ipasavyo ili kuamsha ari ya ufanyaji kazi kwa wananchi ili kuleta maendeleo katika maeneo yao” alisema Bibi Sihaba.
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga pia amesisitiza matumizi ya rasilimali zilizopo ili kuendelea kuhimiza wananchi kujitolea katika kujitolea na kufanya kazi zitakazowaletea maendeleo katika maeneo yao.
Aidha kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub  amemuakikishia Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kuwapa ushirikiano Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili waweze kutimkiza majukumu yao.
“Sisi viongozi wa mkoa tupo tayari kutoa ushirikiano kwa Maafisa hawa ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa wakati na katika ufanisi” alisema Bibi Waumoja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amefanya ziara mkoani Iringa kwa lengo la kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii na kuamsha aerinya wananchi katika kujitolea kufanya kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla. 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub akisistiza jambo kwa  kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akifafanua jambo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Kikundi cha Sanaa cha Malezi na Uhamasishaji wa Ulinzi kwa Mtoto Wilaya ya Iringa wakiimba wimbo wa kumshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kwa kuendelea kuhamasisha Maafisa Maendeleo ya Jamii na ustawi wa JAmii kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Jamii. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(kulia) akijadiliana jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub  mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Katibu Mkuu huyo na Maafisa Maendeleo ya jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa. Picha na Erasto Ching’oro WAMJW. 

VIDEO: KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO, SIHABA NKINGA AKUTANA NA MAAFISA MAENDELEO, USTAWI WAJAMII MKOANI IRINGA

TCCIA YAANDAA MKUTANO WA PILI WA KIBIASHARA 2017

$
0
0
Makamu wa Rais wa TCCIA Octavian Mshiu akimkabidhi nyaraka ya shukrani Afisa mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Joseph E Haule
*************************************
Chama cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo (TCCIA) kimeandaa mkutano maalumu (Business Breakfast) uliowakutanisha wafanyabiashara na taasisi mbalimbali za serikali wakiwemo TRA, EWURA, BRELA na TBS katika kujadili maswala mbalimbali na muhimu ya kibiashara ikiwemo kuboresha na kukuza ufanisi kwa wanachama wa TCCIA.Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu wa Rais wa TCCIA Octavian Mshiu alisema TCCIA inatambua umuhimu wa ufanyaji kazi wa pamoja na ushirikiano kati ya TCCIA na taasisi za Serikali ili kuleta tija katika biashara hapa Tanzania.
Jackson Lohay kaimu Meneja Mwandamizi huduma za kibenki rejareja Azania BankTukio hilo pia lilimshirikisha mwambata wa biashara wa Uturuki nchini Tanzania Bwana Onur Tekyildiz ambaye alieleza fursa kubwa za biashara kati ya uturuki na Tanzania pia ukuzaji na uvutiaji wa wakezaji na wabia kutoka Uturuki.
Mwambata wa biashara wa Uturuki nchini Tanzania Bwana Onur Tekyildiz
*****************************************
Awali mwakilishi wa Benki ya Azania ilitoa mada juu ya njia za ukuzaji wa baishara na jinsi ya kupata mitaji na fedha za uanzishaji wa viwanda na pia jinsi ilivyojikita katika kuhudumia wateja wa kawaida na wafanyabiashara.Shirika la nyumba la Taifa (NHC) ambao pi walishiriki kikamilifu katika mkutano huo walieleza fursa zilizopo za miradi yake Tanzania kwa wafanyabishara kuweza kumiliki nyumba na ofisi.
Baadhi ya wanachama walishiriki katika mkutao huo 
************************************
TCCIA Business Breakfast imeandaliwa na TCCIA pamoja na EAG Group kwa udhamini wa Azania Bank na Shirika la Nyumba la taifa(NHC)

KESI YA WEMA SEPETU NA WENZAKE YAPIGWA TENA KALENDA

$
0
0
Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu akiwaMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, alipofika kusikiliza Kesi yake ambayo imesogezwa tena mbele hadi Septemba 12 mwaka huu.
********************************************
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Kisutu, imesema uamuzi wa kupokelewa au kutokupokelewa kwa bangi iliyokutwa nyumbani kwa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili utatolewa Septemba 12.
Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba amesema hayo leo wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Katika kesi hiyo, Wema ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kete mbili za bangi na msokoto mmoja pamoja na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Akiahirisha kesi hiyo, hakimu Simba amesema, " nilitakiwa kutoa uamuzi mdogo leo kuhusiana na kielelezo kilichowasilishwa na shahidi wa upande wa mashtaka kama kipokelewe au la, lakini palitakiwa kufanya utafiti wa kutosha kutolea maamuzi, nilijipa muda mdogo sana, tumejadiliana na mawakili wa pande zote mbili na sasa uamuzi utatolewa Septemba 12 na kesi hii itaendelwa hadi Septemba 13.
Awali ilidaiwa, February mwaka huu, katika makazi ya Wema, Kunduchi Ununio washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vyenye uzito Wa gramu 1.08

MAKAMPUNI YA SIMU NCHINI YASAINI MKATABA WA KUPELEKA MAWASILIANO VIJINI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati), akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Bw. Le Van Dai (kulia) wakati wakisaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya simu kwa kujenga miundombinu maeneo ya vijijini, chini ya Mradi wa sita wa kufikisha mawasiliano kwa wote, kwenye makao makuu ya UCSAF barabara ya Bagamoyo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2017. UCSAF imesaini makubaliano kama hayo na makampuni mengine ya simu hapa nchini ikiwemo, Vodacom Tanzania PLC, Airtel, tigo na TTCL.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw.Ian Ferrao(kulia) wakisaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya simu kwa kujenga miundombinu maeneo ya vijijini. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mnyaa Mbarawa,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw.Ian Ferrao,akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kwaniaba ya makampuni yote ya simu nchini wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya simu kwa kujenga miundombinu maeneo ya vijijini. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
*****************************************
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Mawasiliano Kwa Wote Nchini, (UCSAF), umesaini mkataba na makampuni matano ya simu hapa nchini wa utekelezaji wa Mradi wa Sita wa Kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Manyaa Mbarawa.
Makampuni yaliyotia saini mkataba huo ambao utayawezesha, kujenga miundombinu ya kupeperusha mawasiliano ya simu kwenye mmbalimbali hususan vijijini ni pamoja na Halotel, Airtel, Vodacom Tanzania PLC, TTCL na TIGO.
Waziri Profesa Mbarawa alishuhudia Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF kwa niaba ya Mfuko, akisaini mikataba hiyo na Maafisa Watendaji Wakuu wa makampuni hayo mbele ya waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa maafisa wa UCASAF, kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza malengo makuu ya Mfuko ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu.
Lakini pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano hafifu.
Malengo mengine ni pamoja na Kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
Kutengeneza mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la kiushindani;
Maafisa hao wamesema lengo linguine ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amewahakikishia wawekezaji ushirikiano uklio dhahiri kutoka serikalini na kuwataka, waongeze kasi ya uboreshaji wa mawasliano ya simu ili wananchi hususan wa vijijiniwaweze kutumia teknolojia ya mawasiliano kuharakisha maendeleo yao.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akitoa hotuba yake
Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw. Joseph Kilongola, akizungumza kwabla ya kumkaribisha Profesa Mbarawa kutoa hotuba
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, akielezea lengo la kusainiwa kwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa Mradiwa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote.
Baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya simu
 Beatrice Singano Malya kutoka Airtel, akifurahia hotuba.
Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF
Afisa kutoka kampuni ya Halotel
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Ian Ferrao, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, wakisaini mkataba huo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Mhandisi Cecil Nkomola Francis, wakisaini mkataba huo.
Mhandisi Ulanga, akimpongeza Bw. Ferrao wa Vodacom
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, akiwa miongoni mwa maafisa wenzake wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri
Profesa Mbarawa, akipena mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw.Joseph Kilongola.
Wakuu wa makampuni ya simu za mikononi nchini.
Ferrao, akitoa hotuba ya shukrani kwa niaba ya wenzake

Profesa Mbarawa na Mhandisi Ulanga, wakionyeshana kitu
Profesa Mbarawa akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw.Joseph Kilongola
Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF

NEW HABARI (2006) LTD KUPITIA GAZETI LA DIMBA,YAANDAA ONESHO LA MUZIKI WA DANSI 'DIMBA MUSIC CONCERT'

$
0
0
  Meneja matukio wa Dimba Music Concert, Mwani Nyangassa, akizungumza na waandishi wa Habari jana kutambulisha wanamuziki watakaoshiriki katika tamasha hilo, litakalofanyika Septemba 2 kwenye ukumbi wa Travertine, Hotel Magomeni. Kushoto ni Mhariri wa Dimba Jimmy Chika na kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya New Habari (2006) LTD Michael Budigila. 
 Baadhi ya wanamuziki watakaoshiriki Dimba Music Concert, wakiwa na Kamati ya Maandalizi  jana mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi za New Habari (2006) LTD.
Wanamuziki Juma Kakere, Ally Choki, Hussein Jumbe na Juma Katundu, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutambulishwa kutumbuiza katika Tamasha hilo Septemba 2.
Mhariri wa Dimba, Jimmy Chika, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamuziki na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Dimba Concert .
********************************************
Kampuni ya New Habari (2006) LTD kupitia gazeti lake la DIMBA, imeandaa onesho maalum la muziki wa dansi DIMBA Music Concert litakaofanyika Septemba 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Traventine Magomeni jijini Dar es Salaam.
Onesho hilo lina lengo la kuukuza na kupromoto muziki wa dansi, ambao umekuwa ukielekea kupotea kila kukicha.
Katika onesho hilo kutakuwepo na mpambano wa wanamuziki wa dansi, ambapo bendi ya Msondo Ngoma Music (Baba wa Muziki), itachuana na mastaa mbalimbali wa muziki huo kutoka bendi mbalimbali nchini.
Kundi la mastaa ambao tumewapa jina la ‘Timu ya Taifa ya Muziki wa Dansi,’ litakalochuana na Msondo Ngoma, litaundwa na wanamuziki kama Kikumbi Mwanza Mpango' King Kiki', Hassan Rehani Bitchuka 'Stereo', Karama Regesu, Ally Choky, Juma Kakere, Nyoshi El-Saadat ‘Sauti ya Simba’ na Muumini Mwinjuma.
Kwa upande wa vyombo, watakuwepo wapiga vyombo Saadi Ally 'Machine' kwenye dramu, gitaa la solo likitekenywa na Aldofu Mbinga wakati besi litangurumishwa na Hosea Mhogachi.
Aidha, kinanda kitatekenywa Juma Jerry wakati tumba zitakung'utwa Salum Chakuku 'Kuku Tumba', ambapo ala za upepo watakuwepo Ally Yahaya, Hamis Mnyupe Tarumbeta na Shaabani Lendi kwenye Saksafoni.
"Utakua ni usiku wa mastaa wa dansi kuionyesha kazi Msondo Ngoma, kwani miaka ya hivi karibuni imekua ikikosa mbabe katika kila bendi inayoshindanishwa nayo lakini safari hii tumeamua tuwaonyeshe kazi."
Kiingilio katika onesho hilo litakaloanza kuanzia saa 2:00 usiku hadi majogoo, kitakuwa ni shilingi 10,000 kwa wote na 20,000/- kwa VIP.
IMETOLEWA NA MENEJA WA TUKIO ‘DIMBA MUSIC CONCERT’ MWANI NYANGASSA

BALOZI WA KUWAIT ATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA ECO VILLAGE MKOANI PWANI.

$
0
0
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wanaoishi wanaoishi katika magumu cha Eco Village mkoa wa Pwani baada ya kuwakibidhi zawadi mbalimbali.
**********************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem ametembelea Kijiji cha Eco-Village kilichopo Kisemvule Mkoa wa Pwani. Eco-village ni eneo la kulelea na kuhudumia mayatima ambapo ndani yake kunafanyika shughuli za kilimo,ufugaji wanyama hasa kuku na ng'ombe, na hutegemea umeme wa jua kama chanzo cha nishati.
Katika ziara hiyo Mhe. Jasem alikabidhi msaada wa vyakula unga wa ngano,mchele,maharage,mafuta ya kula,majani ya chai na sukari kwa ajili ya watoto mayatima msaada ambao utatosheleza kwa kipindi cha miezi miwili. 
Pembezoni mwa ziara Mhe. Balozi alipanda mti ikiwa ni ishara ya kuunga mkoni juhudi za Eco-village ambacho ni kituo kinachoendesha mambo yake kisasa. 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem akipanda mti katika kituo cha watotot wanaoishi wanaoishi katika magumu cha Eco Village mkoa wa Pwani alipikwenda kutembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.

VETA NA UJERUMANI WATIA SAINI YA MAKUBALIANO YA KUENDELEZA UWAGENZI KWA VIJANA

$
0
0
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Moshi Kabengwe akisaini makubaliano ya uendelezaji wa mafunzo ya uwanagenzi kulia ni ni Mtendaji Mkuu wa Ujerumani , Reiner Nolte na wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter. 
**********************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetiliana saini makubaliano yenye thamani ya Euro 900,000 (zaidi ya shilingi bilioni 2.3) na Chemba ya Baraza la Ufundi Stadi ya Ujerumani (WHKT) kwa ajili ya mafunzo ya uwanagenzi yenye lengo la kuimarisha ufundi wa zana za kilimo na teknolojia ya mitambo ya ujenzi. 
Makubaliano hayo yalitiwa saini na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Moshi Kabengwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Leonard Akwilapo na Ujerumani aliyetia saini ni ni Mtendaji Mkuu wa Ujerumani , Reiner Nolte na kushuhudiwa na Barozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter, Mwenyekiti wa Board ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi,Peter Maduki, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk. Bwire Ndazi na Maafisa wengine waandamizi wengine wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, VETA na Ujerumani. 
“ujuzi wa mafundi na wakulima utaboreshwa kupitia kozi zitakazotolewa na VETA kwa mfumo wa uwanagenzi. Kozi hizo ni pamoja ufundi zana za kilimo, ufundi mitambo ya ujenzi na mafunzo ya vitendo katika teknolojia ya kupunguza upotevu wa mavuno ya mazao ya kilimo katika maeneo yatakayoainishwa,” inaeleza sehemu ya waraka wa makubaliano. 
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Balozi wa Ujerumani nchini Dk. Detlef Waechter alisema anatarajia kuwa ushirikiano katika mradi huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa Watanzania wengi, hususani vijana katika kupata ujuzi wa kuutumia kwenye kuongeza tija kwenye kilimo nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimani watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Moshi Kabengwe aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa msaada na ushirikiano na kusema kuwa utawasaidia vijana wengi kuajirika na kuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo. 
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa kuendelea kuiamini VETA na kuendeleza ushirikiano nayo katika utoaji mafunzo kwa mfumo wa uwanagenzi. Amesema, ushirikiano katika miradi ya nyuma umeendelea kuwanufaisha vijana wengi kupata ujuzi na kuweza kuajirika kwa urahisi. 
Mafunzo ya uwanagenzi uendeshwa kwa mfumo wa ngwe za mzunguko kati ya chuo cha ufundi stadi na sehemu ya kazi ambapo mwanafunzi hupata mafunzo ya ujuzi kwenye karakana za chuo na uzoefu wa hali halisi mahala pa kazi, hivyo kumwongezea umahiri pamoja na maarifa zaidi na utamaduni wa ya mazingira ya kazi husika. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza katika mkutano wa kutiliana saini ya makubaliano kati ya Ujerumani na VETA kwa ajili mafunzo ya uwanagenzi yenye lengo la kuimarisha ufundi wa zana za kilimo na teknolojia ya mitambo ya ujenzi. 
Picha ya Pamoja Balozi wa Dk. Detlef Waechter akipeana mkono Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimani watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Moshi Kabengwe pamoja na watendaji wa VETA Wawakilishi Ujerumani baada ya kusaini makubaliano ya kuendeleza wanagezi.
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>