Beki wa timu ya Taifa ya Nigeria, Juwon Oshaniwa (kushoto) akiruka kuwania mpira na Paul Pogba, wakati wa mechi yao ya Kombe la Dunia 2014 hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa jana usiku. Katika mchezo huo Nigeria iliaga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa. Kwa matokeo hayo Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali za mashindano hayo.
Golikipa ya Ufaransa, Hugo Lloris, (kulia) akipangua mpira huku beki wake Olivier Giroud, (kushoto) akimvuta jezi mchezaji wa Nigeria, Peter Odemwingie's, wakati wa mchezo huo wa Kombe la Dunia hatua ya 16 Bora.
Golikipa wa Ufaransa, Hugo Lloris, akianguka baada ya kushindwa kuzuia mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Nigeria, Emmanuel Emenike, na kutinga wavuni na kuandika bal la kuongoza ambalo hata hivyo lilikataliwa na mshika kibendera aliyeinua kuashiria Emmanuel, alikuwa ameotea.
Mshambuliaji wa Ufaransa, Mathieu Valbuena (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa Nigeria, Juwon Oshaniwa, wakati wa mchezo huo.
Laurent Koscielny, wa Ufaransa (wa pili kulia) akikosa nafasi ya wazi mbele ya wachezaji wa Nigeria wakati wa mchezo huo.![]()

John Obi Mikel, akijaribu kumiliki mpira wakati wa mchezo huo.
Mikel John Obi, wa Nigeria (kulia) na Kenneth Omeruo, wakimdhibiti mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud (9), wakati wa mchezo huo.