Mchezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid, ambaye pia ni Kiongozi wa Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid,Luis Figo, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mchezo wao wa kirafiki na timu ya Tanzania Eleven inayoundwa na wachezaji wa zamani wa timu za Yanga, Simba na Taifa Stars, utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia mchezo huo Figo amesema kuwa wao wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya kuonyesha uwezo na kutoa burudani kwa mashabiki wao wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kujenga ushirikiano baina ya wachezaji wa Hispania na Tanzania. Kulia ni Christian Calembeu, na Mkurugenzi wa TSN Frank Baghoza na Kocha wa timu ya Madrid.
Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven Stars, Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati) akizungumzia namna Timu yake ilivyojiandaa kuwakabili magwiji hao soka, wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Luis Figo na kulia kwake ni Fernando Sanz Duran ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
Fernando Sanz Duran, akiwapiga picha ya kumbukumbu wenzake wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwa bize kunasa matukio.