Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

TFDA YATUMIA MAONESHO YA VIAWANDA KUTOA ELIMU KWA UMMA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akitoa maagizo kwa Meneja Uhusiano kwa Umma wa TFDA, Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda la TFDA katika viwanja vya sabasaba jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda hilo katika viwanja vya sabasaba jana jijini Dar es Salaam. 
 
Wananchi wakipata huduma katika banda la majani ya chai katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Picha na Emmanuel Massaka.
***********************************
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema vijana ndiyo wanaweza kuleta mapinduzi ya sekta ya viwanda vinavyojengwa. 

Dk.Mpango ameyasema hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ameseama vijana lazima wachangamkie fursa ya viwanda pamoja na ujasiriamali. 

Amesema nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaohitaji hivyo sekta binafsi ndiyo inaajiri sehemu kubwa ikiwemo kujiajiri. Dk. Mpango amesema sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu ambao ni vijana wa kufanya hivyo kwa ujuzi wao. 

Aidha amesema kila mtu anatakiwakulipa kodi ili serikali iweze kutoa huduma kwa wananchi na kodi isipotumika kwa malengo wananchi wanaweza kuhoji kodi i yao.

Dk. Mpango amesema serikali haitaki kuibana sekta binafsi ishindwe kupumua kutokana na kodi kinachofanyika kuangalia uwezo wa ulipaji kodi kwa kilakinachozalishwa. 

Waziri huyo ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Chakula Dawa (TFDA), kuwatembelea wajasiriamali ili kuweza kupata changamoto zao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>