Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live

*BREAKING NEEEEWZ!!! - BUNGE LAWASIMAMISHA WABUNGE 7 KWA KUFANYA VURUGU BUNGENI JANUARY 27 MWAKA HUU

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati  ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe.George Huruma Mkuchika akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu uchunguzi wa vitendo vya baadhi ya wabunge kufanya vurugu.
****************************
 Na. Aron Msigwa -Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge limepitisha azimio la  kuwasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliohusika katika kufanya vitendo vya vurugu ndani ya ukumbi na kudharau Mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Mhe.Kabwe Zubeiri Ruyangwa Kabwe, Mhe.John Heche, Mhe.Halima Mdee,Mhe.Tundu Lissu, Mhe.Halima Mdee, Mhe.Pauline Gekul  na Mhe. Ester Bulaya.
 Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Akisoma adhabu hizo Mwenyekiti wa kamati hiyo yenye wajumbe 15 Mhe.George Huruma Mkuchika amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo kwa kuwaita na kuwahoji wahusika ulibaini kuwa wabunge hao walitenda kosa kwa kukiuka kanuni zinazoliongoza bunge hilo.
 Imebainishwa kuwa Mhe.Zitto Kabwe alivunja masharti ya Kifungu cha 24(c), (d) na (e) cha Sheria ya Haki na Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 60(2) na (12) , 74(1) na (b) kwa kusimama na kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau mamlaka ya Spika. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Kamati hiyo ilibaini kuwa Mhe.Godbless Lema, Mbunge wa Arusha alivunja Masharti ya kifungu cha 24 (c),(d) na (e) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 pamoja na Kanuni ya 74(1) (a) na (b) ya kanun hiyo Kudharau Mamlaka ya Spika.

Kwa upande wa Mhe.John Heche alivunja kanuni ya 72 (1) na 68(10) ya kanuni za Bunge kwa kuendelea kusimama na kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa mwongozo na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilivuruga shughuli za Bunge.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati hiyo Mhe.Halima Mdee, Mhe.Tundu Lissu,Mhe Pauline Gekul  na Mhe.Ester Bulaya walivunja masharti ya kifungu cha 24 (c), (d) na (e) cha sheria ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 72 (1)68 (10), 60(2) na 12 na 74(1) (a) na (b) kwa kusimama na kuendelea kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi, kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau Mamlaka ya Spika.

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Mhe. Ester Bulaya na Mhe.Tundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Spika.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.

 adhabu hizo Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja na pia kwa kuwa alitoa ushirikiano kwa kamati kwa kufika na kujibu maswali yote kama alivyoulizwa pamoja na kuheshimu vikao vya kamati na Mwenyekiti aliyeongoza vikao hivyo.

Pamoja na adhabu hizo Kamati hiyo imetoa maoni na mapendekezo kuwa Bunge liandae mafunzo ya kutosha kwa wabunge wote kuhusu matumizi ya uzingatiaji sahihi wa kanuni sahihi wa kanuni za Kudumu za Bunge hasa kanuni za majadiliano ndani ya Bungeni.

Aidha, Kamati hiyo imesema kuwa ipo haja ya kutungwa kwa kanuni za maadili kwa wabunge wote kama kifungu cha 12 A Cha Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kinavyoelekeza ili kuweza kudhibiti nidhamu kwa wabunge kwa kuhakikisha heshima na hadhi ya Bunge inadumishwa.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wakichangia kwa nyakati tofauti kuhusu suala hilo wamesema kuwa ipo haja ya Bunge kurudisha heshima yake kwa wabunge wote kuheshimiana na kutoa michango yenye staha kwa kuzingatia nafasi walizonazo katika jamii.

Wamesema kuwa michango wanayoitoa ndani ya Bunge hilo lazima ijikite katika masuala yanayowahusu wananchi wanaowawakilisha badala ya mambo yanayochochea vurugu na kulifanya Bunge lipoteze heshima yake katika jamii.

Aidha, wabunge hao wamekubali kwa kauli moja kuanza upya kuzingatia kanuni zinazoendesha vikao vya Bunge huku wakimtaka Spika wa Bunge au Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutosita kuchukua hatua za haraka kwa mbunge yeyote atakayekiuka utaratibu na kanuni zilizowekwa.

*MAHAKAMA KUU KUANZISHWA KATIKA MKOA WA MARA

$
0
0
Na Lydia Churi- Musoma
Mahakama ya Tanzania inakusudia kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wa Mara ambapo ujenzi wa jengo la mahakama hiyo unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu.
Akizungumza leo mjini Musoma katika ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman alisema mkoa wa Mara unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu kwa kuwa nia ya Mahakama ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. 
Alisema mahakama hiyo itajengwa kwa haraka na itamalizika katika kipindi cha mwaka moja kwa kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi huo tayari imeshatengwa ambapo nyingine imetokana na msaada waliopewa kutoka Benki ya Dunia.
Alisema kuanzishwa kwa mahakama hiyo katika Mkoa wa Mara kutawapa fursa wananchi wa Mara ya kupata huduma kwa karibu zaidi na pia itasaidia kupunguza kesi zilizoko mahakamani kwa haraka.
Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake alipomtembelea, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo alimwomba Jaji Mkuu kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wake kwa kuwa asilimia 55 ya kesi zote za mauaji katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinatoka katika mkoa wa Mara hivyo mkoa huo unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu.
Pamoja na mkoa huo kuwa na kesi nyingi za mauaji, Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa wa Mara pia unakabiliwa na kesi nyingi zinazohusu masuala ya ardhi kwa kuwa ni asilimia 38.3 tu ya eneo zima la mkoa huo ndiyo eneo linalotuwa kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli za maendeleo
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Mkoa wa Mara una wakazi zaidi ya milioni 1.3.
Alisema Mkoa wa Mara una eneo lenye kilometa za mraba 30,150 ambapo asilimia 36 ya eneo hilo ni maji wakati asilimia 25.7 ni eneo lenye mapori na hifadhi za Taifa ikiwemo mbugaya wanyama ya Serengeti.
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa aliisifu Mahakama ya Tanzania kwa kufanya kazi yake kwa weledi ya kuzimaliza kesi zilizohusu mapigano ya koo zilizokuwepo katika siku za nyuma mkoani humo kwa kuwa zimesaidia maeneo ya mkoa huo kuwa salama hivi sasa na hayaonyeshi dalili za kujirudia. Aliongeza kuwa eneo la haki likitulia hata masuala ya utawala yakuwa rahisi. 

Jaji mkuu Leo amehitimisaha ziara yake katika kanda ya Mwanza yenye mikoa ya Mara, Geita na Mwanza ambapo alikuwa akikagua shughuli mbalimbali za kimahakama katika kanda hiyo.

*SERIKALI YAJADILI RASIMU YA KISWAHILI YA MPANGO WA KUKABILIANA NA MAAFA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akitoa neno la ufunguzi katika mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mei 30, 2016. 
Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Christopher Chusi akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa uliofanyika Mei 30, 2016 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia mada ya Menejimenti ya Maafa kutoka kwa Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. John Kiriwai (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. 

Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya maafa katika zoezi la ukakamavu katika kujiandaa na kukabili maafa wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa Wilayani Kilosa tarehe 30 Mei, 2016.
Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Fadhili Mtengela akiwasilisha mada ya kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika mkutano wa kujadili mpango huo uliofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. 
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo Wilayani kilosa Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
********************************************************
Na. Mwandishi Wetu
Ofisi ya Waziri Mkuu imejadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wilayani Kilosa Mei 30, 2016.
Rasimu hiyo imejikita katika kutoa miongozo ya uratibu katika kukabili dharura za aina zote za majanga yanapotokea katika ngazi zote za Kitaifa.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maafa Wilayani Kilosa Mkurugenzi wa Tafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Naima Mrisho alieleza kuwa muongozo huo ni sehemu ya kuisaidia jamii katika kupata mbinu bora za kujiandaa, kukabili, na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea ili kuzisaidia jamii zetu.  
“Ni muhimu kuwa na mpango huo kwa kuzisaidia Halmashauri zetu katika kupambana na maafa yanayotukabili,”alisema Bi. Naima 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele alibainisha umuhimu wa Mpango huo ikiwa ni sehemu ya kuanzia na inayotoa muongozo mzuri unaosaidia katika Halmashauri yake katika kukabiliana na Maafa. 
 “Tangu mpango kuanza kutumika Desemba 2013 Wilaya ya Kilosa imeweza kuwa na mbinu za kuyakabili maafa yanapotokea hususani yale ya mafuriko” Alisema Mkuu wa Wilaya. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bw. Idd Mshili aliipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona umuhimu wa kuitembelea Halmashauri yao kwa kuupitia Mpango na kuuboresha ili kusaidia kurahisisha uelewa kwa kua lugha ya Kiswahili inaeleweka kwa urahisi hususani ngazi ya chini na kwa wanavijiji wanaokumbana na maafa pindi yanapotokea.
 “Nichukue fursa hii kuwapongeza Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuona umuhimu wa kuubadili mpango kutoka lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili ili kufikia makundi yote ya jamii kwa urahisi.”
AWALI: Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa ulianza kutumika mwaka 2013 ikiwa na lengo la kuziwezesha Halmashauri kujiandaa na kuyakabili maafa yanapotokea, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kufanya Tathimini kwa Halmashauri za baadhi ya Mikoa kwa kuangalia ubora wa mpango tangu uanze kutumika katika Mikoa ya Mtwara, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Singida na Shinyanga kuanzia Mei 23 hadi 30, 2016.

*IN LOVING MEMORY OF OUR BELOVED PROF. HELEN I. LUGINA

$
0
0
Helen, though it is five years today since God called you, the memories are still strong as the One pm Shining light.  Your unconditional love truly brightened our lives just like the meaning of your name.
Every day in some small way, memories of you come our way.
Living without you is the hardest part of all but with the peaceful memories you left us, you will walk with us forever.
Each one of us still remembers your infectious laugh, it keeps us going when the going gets tough.
Nothing can ever take away, the love you gave us and the family bond you built for us.
You are loved beyond words and missed beyond measure by your husband (Max), children (Emma, Mary, Richard, Roselinda and Kelvin) andgrandchildren (Gabriella, Nathan and Joanna)

*MDAU OTHMAN MANGUBE NA MKEWE BI MARIAM WAWASHUKURU WADAU,WASHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA NDOA YAO

$
0
0
Pichani Mdau Othman Mangube akiwa sambamba na mkewe Bi Mariam Swedy wakiwa katika nyuso za furaha,mara baada ya kufunga ndoa yao hapo mwaka jana,ambapo leo Wanamshukuru Mungu kwa kuvuka milima na mabonde mengi katika mazingira tofauti tofauti ya maisha na sasa Wanatimiza mwaka mmoja wa Ndoa yao,ambayo wao bado wanaamini ni changa,lakini kwa rehma na baraka za Mwenyezi Mungu atawasimamia na kuwaongoza katika mstari ulio nyoofu na kuwafikisha miaka mingi zaidi.
"Pia tunawakia heri ndugu jamaa na marafiki popote pale mlipo,tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mlioutoa wakati wa kuifanikisha ndoa hii,nawashukuru sana na tuendelee na ushirikiano huo,sina cha kuwalipa lakini Mwenyezi Mungu atawalipa zaidi."Asanteni sana
Bwana Othman Mangube akiwa na Mkewe Bi Mariam Swedy katika pozi la picha

*WANAHABARI WALIA NA UKOSEFU WA MIKATABA.

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Wamoja Ayubu (Kushoto) akipokea moja ya Ipad toka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel kwa msaada wa kampuni ya Star Times kwa ajili ya Maafisa Habari wa Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Iringa. 
Uwanja wa Kisasa uliojengwa na Kituo cha Michezo cha Iringa Footbal For Hope kwa ufadhili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa ajili ya kukuza vipaji vya watoto na kuwafikishia vijana kwa kuwapa elimu ya Afya kupitia michezo.

*MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMWAKILISHA RAIS DKT JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA, NCHINI PAPUA NEW GUINEA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe walipokutana Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil Alipowasili Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. 
 Viongozi wakiimba Wimbo wa Taifa
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa makini Hotuba ya Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil alipokua akifungua mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Guinea leo Mei 31,2016  Mkutano huo unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akichangia baadhi ya mada zilizowasilishwa kwenye mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Guinea leo Mei 31,2016.  Mkutano huo unaojadili kuhusu masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa.
Picha ya pamoja....

*TANROADS YAKANUSHA KUDAIWA FIDIA

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wamekanusha kudaiwa fidia na wananchi wa Kijiji cha Mazingira,Wilaya ya Handeni mkoani Tanga waliovunjiwa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa TANROADS Mhandisi Alfred Ndumbaro alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya malalamiko ya wananchi wa Kijiji hicho kuhusu kutolipwa fidia zao.

”Sheria iko wazi kuwa wanaojenga karibu na barabara wakivunjiwa hawalipwi fidia yoyote lakini wale ambao ujenzi wa barabara uliwafuata katika maeneo yao wana haki ya kulipwa fidia”, alisema Mhandisi Ndumbaro.

Mhandisi Ndumbaro ameongeza kuwa zoezi la malipo ya fidia kwa wanakijiji waliokuwa na uhalali wa malipo hayo lilishakwisha zamani kwa hiyo, wanaodai sasa ni wale ambao nyumba zao zilivunjwa kutokana na kujenga eneo la barabara.

Aidha, Mhandisi huyo ametoa rai kwa wananchi kufuata sheria za ardhi ili kupata uhalali wa viwanja vyao pamoja na kuepuka usumbufu na gharama za kuvunjiwa nyumba zao.

Nyumba hizo zilivunjwa ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami yenye Kilomita 54 kutoka Mkata hadi Handeni iliyojengwa na Kampuni ya Synohydro Corporation Limited ya China.


*MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0

 Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.

Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.

Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.
Eti ni kama wanakoromeana (maskhara)...

*AMBASSADOR NAIMI AZIZI ADRESSES AMGC ANNUAL MEETING

$
0
0
The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz Delivers her speech during the opening session of the African Minerals and Geosciences Centre(AMGC) 36th Annual Meeting hels at United Nations Economic Commission for Africa(UNECA), Conference Centre in Addis Ababa Ethiopia

*GARI JINGINE LANUSURIKA KUTUMBUKIA BAHARINI KIVUKONI DAR

$
0
0
 Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa kwenye kidaraja cha kuvushia magari kuingia kwenye kivuko, gari hilo kunusurika kutumbukia Baharini kwa kutofuata sheria za vivuko kwa kujaza mzigo mkubwa wa Barafu ambazo haikuweza kufahamika mara moja zilikuwa na uzito gani na zilikuwa zikipeleka wapi.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 11: 25 alasiri wakati gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami na kunasa kwenye mlango wa kivuko  hicho kutokana na gari hilo kuzidisha uzito wa mzigo mkubwa uliokuwa ndani yake na kusababisha kunasa katika mlango huo wa MV Lami.
Baada ya tukio hilo ilibidi kushushwa mabarafu yote na kisha ari hilo hilo likavutwa na gari jingine ili kulinusuru kutotumbukia majini na kupelekwa   Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini  Dar es Salaam.
Juhudi za kulinusuru gari hilo zikiendelea....
Gari hilo likisukumwa...

*TRA KUGAWA MASHINE ZA EFD BILA MALIPO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alfayo Kidata

*UZINDUZI WA MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MARA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah akizindua mradi wa Uboreshaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3 Mkoani Mara leo. Maftah alizindua mradi huo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. PS3 inatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kupitia Halamshauri 97 chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Mwakilishi wa  Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akizungumza ambapo alisema kuwa PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
 Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza.
 Baadhi ya washiriki ambao ni Wakurugenzi na watendaji wengine kutoka Mara wakifuatilia uzinduzi huo.
Mtaalam kutoka TMA, Paul Chikira ambae ni mmoja wa wawezeshaji akifuatilia tukio hilo la uzinduzi wa mradi. 
 Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Felix Lyniva akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi
 Washiriki wakipitia nyaraka wakati wa uwasilishaji mada.
 Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.
 Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
 Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
 Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mayaya Magesse akiuliza swali  kuhusiana na mradi huo wa PS3.
 Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Julius Ndyanabo akiuliza swali kuhusiana na mifumo ya mwasiliano.
 Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akijibu hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na washiriki.
 Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.
Mratibu wa Mafunzo ya muda Mfupi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambao ni moja wa wadau wa utekelezaji wa mradi huo wa PS3, Benjamin Magori akifafanua baadhi ya mambo.
 Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce Muro akifafanua na kujibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa katika idara yake katika utekelezaji wa mradi huo.
 Nyaraka mbalimbali zikipamngwa na waratibu wa mradi huo.
 Washiriki wakipewa nyenzo za mkutano huo.
 Washiriki wakisikiliza kwamakini majumuisho ya awamu ya kwanza ya maswali na majibu.
Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza na kulia ni Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PS3.
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye (wapili kulia) akifanya majumuisho. Wengine kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Musoma, Capt. Willium Gumbo, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Maftah na Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PS3.
Picha ya pamoja na washiriki
*****************
UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa naShirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Musoma mkoani Mara siku ya Jumanne na Jumatano, Mei 31-Juni 1, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Magesa Mulongo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah.
Watu takribani 200 walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Mara, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri.
Mkoa wa Mara una Halmashauri tisa, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Mji wa Tarime, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Halmashauri ya Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.
PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 
Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

*ZIARA YA MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE JORDAN RUGIMBANA KUKAGUA MAENDELEO YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI WILAYANI CHEMBA NA KONDOA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa, leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa pili kutoka kulia walio kalia dawati) akikagua ubora wa madawati yanayotengenezwa na wilaya ya Chemba kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Rais la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati
Mafundi wakiendelea na kazi ya utengenezaji madawati ya Wilaya za Chemba na Kondoa kama walivyokutwa Mei 30, 2016 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kukagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati.
*********************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana Mei 30, 2016 amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya kazi ya utengenezaji madawati katika Wilaya za Chemba na Kondoa.
Katika ziara yake, Mheshimiwa Rugimbana ameonesha kuridhishwa na hatua ya utengenezaji madawati iliyofikiwa na Wilaya ya Chemba na jitihada alizoziona zimempa imani kuwa kufikia mwishoni mwa mwezi Juni, 2016 Chemba watakuwa wamekamilisha agizo la Mheshimiwa Rais Magufuli la kumaliza tatizo la madawati.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mheshimiwa Ramadhan Maneno alimweleza Mkuu wa Mkoa Dodoma kuwa Wilaya hiyo ina upungufu wa madawati 9,400 na hadi kufikia Mei 30, 2016 tayari Chemba walikuwa wamekamilisha utengenezaji wa madawati 5,000. Aidha,  tayari wameisha kusanya vifaa ambavyo ni mbao na bomba za chuma (Flat Bar Pipes) vinavyotosheleza kutengeneza madawati yaliyobakia na tayari vifaa hivyo vipo kwenye karakana inayotengeneza madawati ya chemba na kazi ya utengenezaji inaendelea.
“Pamoja na kuwepo kwa changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara, Wilaya imefanya jitihada za kuongeza idadi ya mafundi ili washambulie kazi ya madawati yaliyobakia na kuhakikisha inakamilika kabla ya mwisho wa mwezi Juni” aliongeza Mhe. Maneno.
Kwa upande wa Wilaya ya Kondoa, Mheshimiwa Rugimbana amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha kazi ya kutengeneza madawati inafanyika kwenye kituo kimoja na Wilaya kuongeza nguvu ya kazi kwa kuongeza idadi ya mafundi  na vifaa ikijumuisha mbao na bomba za chuma (Flat Bar Pipes).
Aidha, ametaka kazi hiyo ifanyike hadi siku za Jumamosi na Jumapili, pia vituo vya kutengenezea madawati viwekwe taa za umeme ili kazi ya utengenezaji ifanyike usiku na mchana kwa utaratibu utakaofaa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mheshimiwa Shaban Kissu ameahidi kufikia Juni 15, 2016 Kondoa itakua inamalizia utengenezaji wa madawati yanayohitajika kwenye Wilaya hiyo kwani kwa sasa wamenunua mbao kwa bei nafuu kutoka Wilaya ya Chemba na Bomba za Chuma (Flat Bar Pipes) kutoka viwandani ambapo kwa pamoja vifaa hivyo vitatosha kutengenezea madawati yaliyobakia kulingana na mahitaji.
Taarifa ya Wilaya ya Kondoa imeonesha kuwepo kwa upungufu wa madawati 10,580 wakati yaliyokamilika kutengenezwa hadi sasa ni madawati 2,299 na yaliyo katika hatua za mwisho za matengenezo ni madawati 1,322.
Akihitimisha ziara yake ya ukaguzi, Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rugimbana amezitaka Wilaya za Dodoma kushirikiana ikiwa ni pamoja na zile Wilaya zenye misitu kuzisaidia mbao Wilaya ambazo zina uhaba wa misitu, Wilaya zilizofanikiwa utengenezaji wa madawati kama Chemba na Dodoma kuwapa uzoefu Wilaya zenye changamoto na kuahidi kuwa mwishoni mwa wiki atakamilisha kufanya ziara ya ukaguzi wa madawati kwenye Wilaya za Chamwino, Kongwa, Mpwapwa na Bahi.

Imetolewa na:
Idara ya Mawasiliano ya Serikali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
DODOMA
Mei 31, 2016

*MADAKTARI BINGWA WAPATA MAFUNZO YA KUREKEBISHA MIGUU NA MIFUPA ILIYOPINDA

$
0
0
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa Dk.Richald Gellman  kutoka Califonia - San Fransisco Marekani (kushoto), akiwaonesha kifaa Chuma kinacho tumika kufanya marekebisho ya mifupa iliyo pinda baada ya kuunga vibaya au kutounga kabisa,   madaktari  mbalimbali kutoka nchi mbalimbali za Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia, DRC Congo, Nigeri, Zimbabwe na wenyeji wao Madaktari wa Taasisi hiyo  waliohudhuria Mkutano huo utakaomalizika Juni 3, 2016, katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mifupa ya Fahamu Muhimbili (MOI)  Dar es Salaam leo. 
 Baadhi ni vifaa vya kufanyia kazi hiyo
Mafunzo yakiendelea.....
 Madaktari Bingwa wakiwa katika chumba cha mikutano katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Moi, leo...
Umakini wa mafunzo.....
Madaktari Bingwa wa Taasisi hiyo wakifuatilia mafunzo hayo.

*TASWA WAMTEUA MHADHIRI WA SJMC KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA TUZO ZA WANAMICHEZO BORA WA 2015/16

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
A;KAMATI YA TUZO
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Makamu Mwenyekiti wa TASWA, ambaye pia Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania mwaka 2015/2016.
 
Pia TASWA imeteua wajumbe tisa wa kamati hiyo. Majina yao na vyombo vyao katika mabano ni Mahmoud Zubeiry (Bin Zubeiry Sports- Online), Jane John (TBC), Baruani Muhuza (Azam Media), Limonga Justine (Redio Uhuru), Maulid Kitenge (E-FM Redio), Deogratias Rweyunga (Redio One/ITV), Shaffih Dauda (Clouds Media), Asha Muhaji (Bingwa) na Nelly Mtema (Daily News).
 
Kamati inaweza kuongeza wajumbe wengine au kupunguza kwa kadri itakavyoona inafaa. Utaratibu wa kuizindua kamati hiyo unaandaliwa na sekreterieti ya TASWA. Jukumu la kamati itakuwa ni kuandaa utaratibu wa kuwapata wanamichezo watakaowania tuzo hiyo na pia kuteua washindi kwa kila mchezo.
 
Tuzo za Wanamichezo Bora zinazotolewa kila mwaka na TASWA zimepangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu, Dar es Salaam zikihusisha michezo mbalimbali.
 
 
B; ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
 
TASWA kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha program ya ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili, ikiwa katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine la waandishi wa habari chipukizi.
 
Kwa kuanzia wahariri wa habari za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi usiopungua miaka kumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi kwa ziara ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
 
Tunaamini wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata fursa kama hiyo siku za usoni.
 
Ahsanteni,
 
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
01/06/2016

*SERIKALI KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA TING KUBORESHA MAPATO YA UWANJA WA TAIFA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo pichani) kuhusu kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo katika kikao kati ya kampuni yake na Serikali kilicholenga kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. william Challe akichangia hoja katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
 Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo. miaka minne katika miundombinu na wataalam.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael kichangia hoja akichangia hoja katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
 Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo. 
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo. Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM
******************************************
Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.
Akizungumza hapo jana wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.

“Ndugu zetu TING wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.
Aidha, Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.
Kampuni ya TING imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika miundombinu na wataalam.

*WAAMUZI WA TAIFA STARS V MISRI HAWA HAPA

$
0
0

Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.
Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

*KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI, AZINDUA MATUKIO YA SIKU YA MSANII 2016 JIJINI DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wasanii wakati wa uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
 Mwanamziki mkongwe wa miondoko ya rhumba Stara Thomas akizungumza na wasanii wenzake (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa serikali na wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam. 
 Viongozi wa serikali na wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam. 
 Viongozi wa serikali na wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam. 
Viongozi wa serikali na wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa matukio ya siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francaise Jijini Dar es Salaam. 
 Picha na WHUSM

*MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NCHINI PAPUA NEW GUINEA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mzungumzaji Mkuu wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP, akihutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo wakati Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Mhe. Natumbo Nandi Ndaitwah.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo Baada ya Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati katibu wa Makamu wa Rais Ndugu Waziri Rajab Salum. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandaaji wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific  ACP baada ya kuhutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo. Picha na OMR
Viewing all 13053 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>