↧
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MUASISI WA ASP MZEE ALI MACHANO
↧
*DKT. JOSE CHAMELEONE ATUA JIJI LA MWANZA KUANGUSHA SHOO LA UKWELI LEO CCM KIRUMBA
![]() |
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na ndugu zake wasanii wa Tanzania waliofika leo kuzungumza na waandishi wa habari katika Hotel Gold Crest Mwanza. |
![]() |
Jose Chameleone akiwa na wasanii wa Tanzania kutoka kushoto ni Bob Haisa, King Houston, Chemeleone (mwenyewe) Dogo Dee, Chuse, na Jambo Squard team. |
![]() |
Jose Chameleone akiwa na wadhamini waliosimamia mzigo ukasimama. |
![]() |
Take two na wadhamini. |
![]() |
Jose akiwa na wanahabari wa Mwanza. |
![]() |
Uskose usiku wa leo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba. |
↧
↧
*MSONDO, SIKINDE KAMA YANGA NA SIMBA MTANI JEMBE KESHO TCC CLUB
Na Mwandishi Wetu, Dar
Mabingwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra “Sikinde” kesho mchana zitachuana vikali katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la kufunga mwaka 2013 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa dansi nchini mwaka huu.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano huo litanzaza saa nane alasiri hadi majogoo.
Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa muda wote.
Mratibu huyo alisema kila bendi litapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa hujuma.Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga jukwaani kabla ya kumpisha nyingine.
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaibuka kidedea.
Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na 'Suluhu'.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Athumani Kambi, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge, Zahoro Bangwe, Ibrahim Kandaya, James Mawilla, Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roman Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.
Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’, 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.
Sikinde inaundwa na wanamuziki kama Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka, Mbaraka Othman, Hamisi Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard, Ramadhani Mapesa na Habibu Jeff.
Pambano umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Nipashe, CXC Africa na Saluti5.
↧
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZURU KABURI LA NA KUIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU SHEIKH SULEIMAN AMOUR JENDELE ZANZIBAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) kwenye Makaburi alipozikwa kijijini kwake Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) aliyefariki Dunia hivi karibuni wakati alipofika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo.
↧
*RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA NEW YORK JANA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani jana (24/12/2013) .Viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake. Picha na Freddy Maro
Wakikwa katika mazungumzo.
Wakiagana baada ya mazungumzo.
↧
↧
*WAZIRI MWAKYEMBE AFANYA UKAGUZI WA BEI ZA TIKEKETI ALFAFJIRI MAENEO YA VISIGA
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisoni Mwakembe akifanya ukakuguzi wa tiketi ili kubaini mabasi yaliyo toza gharama kubwa za nauli za kusafiria katika kipindi cha Sikukuu ya Christimass na mwaka mpya, ambapo katika ukaguzi huo badhi ya mabasi yalikamatywa na kuamuliwa kurudisha nauli zilizozidi. Zoezi hilo limefanyika majira ya alfajiri Visiga mkoani pwani na kila basi lilozidisha nauli lilitozwa faini ya shilingi 250,000/=
Mwakyembe akikagua ndani ya basi.
↧
*TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA JAMES KISAKA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.
Akiwa mwanafunzi Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam aliwahi kuchezea timu za Oysterbay Stars, Eleven Stars ya Msasani, Sigara wakati ikicheza Ligi ya Temeke na Nyota Nyekundu kabla ya kutua Simba.
Pia alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana iliyokwenda Zimbabwe kwenye sherehe za uhuru wan chi hiyo mwaka 1980. Vilevile alikuwa mmoja wa wachezaji waliounda kombaini ya Tanzania ya UMISSETA akiwa na akina Said George, Nico Njohole, George Kulagwa na wengine. Hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Benny Kisaka, James alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kufa ganzi na matatizo ya kutoona vizuri.
Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Mwisho (Kwa Yusuf), na anatarajia kuzikwa nyumbani kwao Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kisaka, klabu ya Simba na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Marehemu Kisaka ameacha mjane na watoto wanne. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
↧
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA CCM DMV KUJIUZULU KWA KATIBU MKUU, JACOB KINYEMI
↧
*MSIKILIZE RAY C KATIKA MKASI
↧
↧
*MOHAMED MATUMLA AMCHAPA NASIBU RAMADHAN KWA POINTI
Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akitangazwa kuwa mshindi baada ya kumchapa mpinzani wake Nasibu Ramadhan katika pambano lao lililokuwa la kugombea Pikipiki, la raundi 10 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Friends Corner Manzese usiku huu. Katika pambano hilo Matumla alishinda kwa pointi. VIDEO YA PAMBANO HILI ITAWAJIA BAADAYE USIKOSE KUJIONEA MAWE.
Bondia Nasib Ramadhan (kulia) akikwepa konde la mpinzani wake, Mohamed Matumla wakati wa pambano lao la raunsi 10, lililofanyika kwenye ukumbi huo usiku huu.
Matumla (kulia) akiendelea kuchapana na Nasibu.
Hili lilikuwa ni moja kati ya mapambano ya utangulizi kati ya Juma Fundi (kulia) na Sadiki Abdulazizi, katika pambano hilo, Juma Fundi alishinda kwa pointi katika pambano lao la Raundi Sita.
Fundi (kushoto) akiendelea kuchapana na Abdulazizi.
Mashabiki wa Juma Fundi wakimshangilia kwa ukali wa ulingoni.
Bondia Francis Miyeyusho, akitambulisha pambano lake na Mkenya linalotarajia kufanyika Jumanne ijayo kwenye Ukumbi wa New Msasani.
Hili pia lilikuwa ni pambano la utangulizi kati ya Cosmas Cheka (kulia) na Hamis Ajali, Katika pambano hilo lililokuwa la raundi sita, Cheka alishinda kwa pointi.
Cheka (kushoto) na Ajali, wakiendelea kuchapana.
↧
*WENGI WAJITOKEZA KUUGAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA JANA
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika leo.
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
↧
*BALOZI IDDI APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA MICHEZO YA KOMBAINI YA WANAFUNZI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea vifaa mbali mbali vya michezo kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan and Sons kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake Mohd Raza kusaidia mashindano ya Kombaini za wanafunzi wa Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imedhamiria kufufua upya vugu vugu la michezo Nchini ili kuirejeshea hadhi yake Zanzibar katika Nyanja za Michezo Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya michezo pamoja na vyakula kwa ajili ya washiriki wa mashindano ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliyofanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema heshima ya Zanzibar kimichezo lazima iwepo kwa kuhakikisha Vijana wanaandaliwa vyema Maskulini ambako ndiko kunakopatikana vipaji vya michezo mbali mbali vinavyoweza kuirejeshea heshima yake Zanzibar.
Alifahamisha kwamba jamii popote pale hapa Nchini inahitajika kuongeza ari ya kuwaamsha vijana kwenye mitaa yao katika kupenda na hatimae kushiriki kwenye michezo tofauti kulingana na uwezo wa vijana wenyewe.
“ Zanzibar inaweza kurejea tena katika hadhi yake ya kimichezo Kimataifa kama mpango utakaoandaliwa wa kuamsha vugu vgugu la michezo utapokelewa vyema katika maskuli mbali mbali hapa nchini “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kampuni ya Hassan and Son’s, Zat pamoja na ule wa Zanzibar Ocean View kwa uwamuzi wao wa kuchangia sekta ya michezo nchini mbali ya kudumisha ushirikiano lakini pia husaidia kutoa ajira kwa wanamichezo nchini.
Akitoa Taarifa ya mashindano hayo ya Kombaini za wanafunzi za Wilaya 10 za Zanzibar kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mkuu wa kitengo cha michezo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mussa Abdullrabi Fadhil alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vya vijana maskulini.
Abdullrabi Fadhil alisema tafiti zinaonyesha kwamba vipaji vingi katika sekta za michezo mara nyingi hupatikana miongoni mwa wanafunzi katika skuli mbali mbali hapa nchini.
Alieleza kwamba mashindano hayo yataoshirikisha michezo tofauti ikiwemo soka, Wavu, mchezo wa Bao, Pete pamoja na Table Tennis kwa kujumuisha wanafunzi wa unguja na pemba yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Tarehe 29 Disemba mwaka huu wa 2013 katika uwanja wa michezo wa Uzini Wilaya ya Kati na kumalizika tarehe 5 Januri mwaka 2014.
Mapema Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Hassan And Sons Mohd Raza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake waliochangia vifaa hivyo vya michezo pamoja na vyakula alisema Serikal lazima iungwe mkono na wafanyabiashara pamoja na wananachi katika kusaidia kupunguza au kuondoa kabisa kero zinazoikabili jamii.
Alisema utaratibu huo kwa njia moja utaiwezesha Zanzibar kurejea katika heshima yake kimichezo iliyokuwa ikitambulikana katika sehemu mbali mbali ulimwenguni.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amepokea vifaa vya michezo kwa ajili ya kuchangia maandalizi ya mashindano ya kombe la mapinduzi linalotarajiwa kushirikisha Timu 12 za soka za kitaifa na kimataifa pamoja na timu 27 za michezo mengine ya ndani.
Vifaa hivyo vilivyojumuisha vikombe vitatu kwa washindi wa mwanzo, medani, T. Shirts, Redio maalum kwa Mchezaji, mfungaji na Kipa bora wa mashindano hayo vimetolewa kwa pamoja na Kampuni ya Hassan and Sons, Zat pamoja na Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Akipokea vifaa hivyo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza uongozi wa Makampuni hayo kwa michango yao hiyo itayosaidia kufanikisha vyema mashindano hayo.
Balozi Seif alisema michango ya uongozi wa Kampuni hiyo italeta changamoto kubwa kwa wanamichezo kuweza kujikita zaidi katika hamasa ya kuendeleza vyema mashindano hayo ya kimataifa kwa mwaka huu.
Mapema Mwakilishi wa makampuni hayo ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza aliahidi kwamba yupo tayari wakati wowote kutoa mkopo wa dharura endapo yatajitokeza mapungufu wakati wa maandalizi ya sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Nusu Karne.
Alisema yeye kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake wakati wowote wataendelea kuiunga mkono Serikali kuu katika kutoa michango na misaada itayosaidia kupunguza matatizo yanayowasumbua wananchi.
Akipokea vifaa hivyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kutafuta fedha kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Sharifa Khamis aliwakumbusha wafanyabiashara nchini kuiangalia pia michezo ya ndani katika misaada wanayotoa ili kwenda sambamba na ule mchezo uliozoelewa wa soka.
Timu kadhaa za mchezo wa zimeshathibitisha kushiriki mashindano hayo miongoni mwao zikiwemo timu za soka za Yanga , Simba na Azam za Tanzania Bara, timu za Nchi jirani za Afrika Mashariki, Ikiwemo Sudan ya Kusini, China pamoja na Vietnam.
↧
*KALAMA NYILAWILA AJIFUA KUMSINDIKIZA MIYEYUSHO DESEMBA 31
Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
Makaburini, Bernald Lumbila (kulia) akimfanyisha mazoezi bondia Kalama Nyilawila wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na pambano lale dhidi ya Ibrahim Maokola, litakalofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani Club.![]()
Kalama Nyilawila akijifua.
Pambano hilo litaanza kabla ya bondia Fransic Miyeyusho kupanda ulingoni kuvaana na David Chalanga kutoka Kenya katika mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi.
Pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi kati ya Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde, Cosmas Cheka na Iddy Mnyeke, Anthony Mathias na Fadhili Majiha, ambapo mapambano yote ya utangulizi yatakuwa ni ya raundi sita sita.
↧
↧
*WATOTO 15 WATINGA FAINALI ZA SHINDANO LA "MO KIDS GOT TALENT 2013", FAINALI KUFANYIKA LEO
Lango kuu la kuingilia kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar panapofanyika shindano kali la kusaka kipaji cha SUPA STAA wa watoto na vijana! la "MO Kids Got Talent 2013"
.Wazazi wahamasishwa kujitokeza kwa wingi, kuona vipaji vya watoto wao.
.Fainali kuanza saa kumi na moja jioni
Chief Judge wa Shindano la vipaji vya watoto na vijana wadogo la “MO Kids Got Talent”, Salma Mziray, akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki walioingia semi finals za shindano hilo linalofanyika kwenye hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Neema Theobald na kushoto ni msanii wa filamu nchini Hidaya Njaidi wakiwa meza kuu.
Sehemu ya zawadi zilizotolewa kwa watoto walioshiriki kwenye usaili wa shindalo la "MO Kids Got Talent 2013" ambapo fainali zake zinafanyika leo kuanzia saa Kumi na moja jioni ndani ya Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
Pichani juu na chini ni baadhi ya kati ya watoto 15 wakionyesha vipaji vyao kwenye semi finals za shindano la kusaka vipaji kwa watoto na vijana la "MO Kids Got Talent" lililoandaliwa na Kampuni ya Frost Africa na kudhaminiwa na kampuni ya MeTL Group, ambapo leo jioni kutafanyika fainali za mashindano hayo kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar na mshindi kujinyakulia fedha taslim shilingi Milioni 5 za Kitanzania.
Mambo ya Sugua Gaga hayo...... Wapi Shaa....??? Kipaji hicho...!!!
Sehemu ya watoto wakionyesha vipaji vyao vya aina mbalimbali ikiwemo kucheza, kuimba na vingine kibao.
Kipaji cha mchezo wa Karate pia kilikuwepo.
Sehemu ya watoto wakisubiria kuingia kwenye chumba maalum kuonyesha vipaji vyao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko akigawa zawadi zilizotolewa na MeTL Group pamoja na kupata picha ya kumbukumbu kwa washiriki waliojitokeza kwenye usaili wa shindano la "MO Kids Got Talent" ambapo fainali za shindano hilo zitafanyika leo kuanzia saa kumi na moja jioni kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa ambao ndio waandaji wa shindano la "MO Kids Got Talent" Bw. Peter Sekasiko, katika picha ya pamoja na Operations Manager wa MOblog, Zainul Mzige na Mwandishi wa Gazeti la Nipashe, Enles Mbegalo.
↧
*TAARIFA YA MSIBA
Mtanzania mwenzetu Amne Shaaban Salim wa Brooklyn New York amefiwa na mama yake Fatma Muhsin Zahran. Mama Fatma alifariki huko Pemba, Tanzania jana Alhamisi. Amne na Mmewe Fuad wanapatikana Brooklyn: 223 Richmond Street, Brooklyn 11208. Watanzania na watu wote wenye mapenzi mema mnaweza kufika nyumbani kwao kuwapa pole na simu yao ni 718-348-0203. Kwa wale mnaotumia usafiri wa treni kituo ni Norwood unafika na J train.
Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo yetu. Tunamwomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amen.
Kwa niaba ya Amne na Fuad,
↧
*RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AENDA MUHIMBILI KUWAFARIJI WAGONJWA
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali. Picha na Freddy Maro
Juu na chini ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba (15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo.
Rais akizungumza na mtoto huyo.
↧
*ASHANTI, JKT RUVU KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI JAN 1
Timu za Ligi Kuu za Ashanti United na JKT Ruvu Stars zinapambana Januari Mosi mwakani kati moja ya mechi za kujaribu matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamzi, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kitakapomalizika.
Mawakala 18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora, Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.
Ghomme Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni, K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo.
Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo, S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko.
Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kwa njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapata namba atakayoitumia kufanya malipo kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya malipo kwa TFF ambayo ndiyo mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi (business number) ni 888800. Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao anaweza kufanya malipo kupitia CRDB simbanking.
Baada ya kufanya maombi kupitia njia yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari Huduma na CRDB simbanking, mshabiki atapata namba ambayo ataitumia ku-print tiketi yake kupitia mashine maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF zilizo katika ATM za CRDB kwenye maeneo yafuatayo;
Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la Holland House ambapo kuna mashine mbili, tawi la Vijana, tawi la Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo ambapo kuna mashine mbili na ATM ya CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.
↧
↧
*ETI DAKTARI HUYU ANATIBU UMASKINI
↧
*MSICHANA WA KITANZANIA ALIYENASWA NA MADAWA YA KULEVYA MACAO YADAIWA NI JACK PATRICK
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni.
**********************************************IMEELEZWA kuwa mwanadada wa Kitanzania aliyekamatwa na kete 66 za madawa ya kulevya akiwa Macao, kuwa ni Mwanamitindo maarufu nchini, Jacqueline Patrick Cliff, aliyedaiwa kukamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko nchini China. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na pipi hizo zenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720 sawa na shilingi milioni 215.5 za Kitanzania.
Inadaiwa kuwa Jack alikamatwa wakati akiwa safarini kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne ya Desemba 19, 2013. Baada ya kuhojiwa aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Jack alipata ni mmoja wa zao la warembo walioibukia katika shindano la Miss Tanzania ambapo aliibuka mshindi wa tatu katika shindano la Miss Ilala na kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005/06. Pia alishiriki katika kurekodi video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marehemu Albert Magwea ‘Ngwair’ iliyokwenda kwa jina la She Got A Gwain.
Ni katika kipindi hicho cha umaarufu akaolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Abdallah Fundikira, Abdulatif kabla ya jamaa huyo kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha mihadarati.
Mwanamitindo Jack Patrick, akiwa katika pozi tofauti.
Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick akipelekwa katika chumba maalum kwa ajili ya mkutano na wanahabari Jumanne Desemba 19, 2013 huko Macao China.
↧
*NJEMBA YAGOMA KUSHUKA KUTOKA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO JIJINI DAR AKIHITAJI KUONANA NA RAIS
Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo
Hapa akishushwa na askari wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokoaji
Hapa Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akiwa amemuweka begani na Kushuka nae chini Mara baada ya kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya kumteremsha chini bila kupata madhara
Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji muda mfupi uliopita Ubungo jijini Dar
Tukio likiendelea huku wakazi wa jiji la Dar Wakiendelea kushuhudia.
Raia wakishuhudia tukio hilo
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar leo
Gari la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji likiwa limetia timu eneo la tukio kwaajili ya Kuokoa
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia gari la Polisi likiondoka na Kijana Hassan ambaye alipanda juu ya Mnara leo Ubungo jijini Dar Es Salaam.
↧