Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo na familia zao wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam, jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC na familia zao wakipata mlo wa asubuhi wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa NBC wakichuana katika mchezo wa soka ili kumpata mshindi katika hafla hiyo.
Hapa wakionyesha umahiri wa kucheza mpira wa kikapu katika sherehe hizo.
aadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara wakifurahia kuogelea ndani ya bwawa la kuogelea katika hoteli hjiyo jijini Dar es Salaam.
Kulikuwa na aina mbalimbali za vyakula kukidhi haja ya kila mmoja aliyehudhuria sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam.
Manahodha’ wa timu za michezo za benki hiyo wakionyesha umahiri wao kusakata rumba katika hafla iliyowakutanisha wafanyakazi na familia zao jijini Dar es Salaam.