Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*PSPF KUFANYA MKUTANO NA WATANZANIA WAISHIO NEW YORK

$
0
0
Mfuko wa Umma wa Pensheni wa Tanzania (The Public Service Pensions Fund au PSPF) unaandaa mkutano na Watanzania waishio New York , New Jersey , Connecticut , Pennsylvania na Springfield siku ya ijumaa ya tarehe 13 Desemba 2013 kuanzia saa kumi na moja jioni kule Brooklyn . 

Anwani kamili ya mkutano utakapofanyika ni 1103 Fulton Street , Brooklyn , NY 11238 . Kila mmoja wenu anakaribishwa na kutakuwa na vinywaji na chakula kitakachotolewa na waandaaji wa shughuli hiyo ambao ni PSPF. Wote mnaombwa kuhudhuria. Kama kutakuwa na badiliko la anwani basi wote mtafahamishwa mapema iwezekanavyo.
 
Mada ya mkutano huo ni;
  • Kuwafahamisha Watanzania shughuli za mfuko huo;
  • Kuwafahamisha Watanzania jinsi ya kupata huduma za shirika hilo ikwemo namna ya Watanzania wa diaspora wanavyoweza kuweka pension zao kwenye mfuko huo na namna watakavyopata faida kwa kuweka pesa zao kwenye mfuko huo wa pensheni.

  • Kuwafahamisha Watanzania huduma zinazotolewa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa nyumba  kwa bei nafuu huko Tanzania kwa wanachama wa mfuko huo wa Pensheni.

  • Kuwafahamisha Watanzania kuwa kila mtu anaweza kujiunga na mfuko huo kwa kuanzia malipo madogo tu ya dola 6 kwa mwezi au zaidi kulingana na kipato cha mwekezaji katika mfuko huo.
  • Kuwafahamisha Watanzania shughuli nyingine zaidi za mfuko huo.
Jinsi ya kufika eneo la mkutano: Chukua treni C hadi Franklin Avenue . Na anwani iliyotajwa hapo juu ipo kati ya Franklin na Classon Avenues.
 
Ili uujue zaidi mfuko huu wa Pension unaweza kwenda kwenye website yao : www.pspf-tz.org
 
Wote Mnakaribishwa. Kumbukeni hakuna kiingilio kwenye mkutano huu na soft drinks na chakula vitatolewa. Asanteni.

Deogratius Mhella
The Executive Secretary
New York Tanzanian Community
c/o Tanzania Mission to the UN
201 East 42nd. Suite # 425
New York, NY 10017
Tel: 201-252-7220


Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>