Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*KILIMANJARO STARS HOI KWA ZAMBIA YASHINDWA KUCHUKUA NAFASI YA TATU, MABOMU YARINDIMA UWANJANI, WAKENYA WAKIFOSI KUZAMA BURE, HARAMBEE BINGWA WA MICHUANO HIYO

$
0
0
Mshambuliaji wa Tanzania Bara, 'Kilimanjaro Stars', Mbwana Samatta akienda chini bada ya kukwatuliwa na wachezaji wa Zambia katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge jioni ya leo Uwanja wa  Nyayo, Nairobi, Kenya. Zambia ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. 

Mbwana Samatta akichuana na Nahodha wa Zambia, Bronson Chama kulia
Mrisho Ngassa akimpiga tobo beki wa Zambia, Rodrick Kabwe
Felix Katongo wa Zambia akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Stars, Athumani Iddi 'Chuji'
Haikuwa riziki; Kipa Ivo Mapunda na beki wake Said Mourad wakitoka uwanjani baada ya mechi
Walikosekana; Kiungo Frank Domayo kushoto akiwa na mshambuliaji Thomas Ulimwengu wakifuatilia mechi hiyo jukwani.
Haroun Chanongo kulia akimtoka Kabaso Chongo
Wachezaji wa Stars wakinawa maji baada ya mchezo kusimama kutokana na kulipuliwa kwa mabomu ya machozi na Polisi dakika ya 88 wakipambana na mashabiki wa Kenya waliotaka kuingia uwanjani bure.
Kujiokoa dhidi ya mabomu

Mrisho Ngassa kulia na Amri Kiemba kushoto wakikimbia mabomu. Mchezo ulisimama dakika ya 88 hadi baada ya dakika sita ukaendelea. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry
****************************************
timu ya Kenya ‘Harambee Stars’ leo wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya usiku huu kuifunga Sudan ‘Mwewe wa Jangwani’ mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Shukrani kwake, Nahodha wa timu hiyo, Alan Wanga aliyefunga mabao yote hayo katika mchezo wa leo uliokwenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Kenya.


Wanga alifunga bao la kwanza dakika ya 35 kwa kichwa akiunganisha krosi ya David Ochieng Owino kutoka kushoto na la pili dakika ya 69 akiunganisha kwa guu la kulia krosi ya chini ya James Situma kutoka kulia pia.
Hilo linakuwa taji la sita la Challenge kwa Kenya, baada ya awali kutwaa katika miaka ya 1975, 1981, 1982, 1983 na 2002.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>