Meneja wa Yanga, Afidh Ally, akimsainisha Fomu za usajili za TFF, kiungo mpya aliyejiunga na timu hiyo akitokea Ruvu Shooting, ambaye anatarajia kukipiga kwa mkataba wa miaka miwili na Klabu ya wanajangwani.
Mshambuliaji wa KMKM ya Zanzibar, Ali Shoboli (kushoto) akijikunja kupiga shuti huku beki wa Yanga, Mbuyu Twite, akimdhibiti wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Yanga imeshinda mabao 3-2, bao la kwanza likifungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 43, bao la pili lilifungwa na Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 47 na la tatu likifungwa na Hamis Thabit, katika dakika ya 83.
Mabao ya KMKM, yalifungwa na Ali Shiboli, katika dakika ya 71 na Haji Simba dakika ya 69. Timu hiyo ya KMKM itashuka dimbani tena kesho kukipiga na Simba katika mchezo wa kirafiki katika uwanja huo huo wa Taifa.
Beki wa Yanga, Oscar Joshua, akimdhibiti winga wa KMKM, Mudrik Muhib, wakati wa mchezo huo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Yanga, Nadir Haroub Canavaro (kushoto) akimdhibiti, mshambuliaji wa KMKM, Ali Shiboli.
Kipa wa Yanga, aliyejiunga na wanajangwani katika msimu huu wa dirisha dogo, Juma Kaseja, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
Didier Kavumbagu wa Yanga, akijiandaa kupiga mpira uliomtoka kipa wa KMKM, Mudathr Khamis (chini) wakati wa mchezo huo.
Kiungo wa Yanga, Reliant Lusajo, akiwania mpira na mabeki wa KMKM, wakati wa mchezo huo.
Kocha mpya wa Simba Mcoratia, Logarusic (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', wakifuatilia mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.