Mabondia Jafet Kaseba wa jijini Dar es salaam na Alibaba Ramadhan wa Arusha, wanatarajia kupima afya na uzito kesho jumamosi ya tarehe 21 decemba 2013 saa nne asubuhi katika ukumbi wa Friends Corner Hotelkwa ajili ya pambano lap litakalofanyika keshokutwa Desemba 22.
Pambano hilo lililoandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya Karage Suba na bondia mkali anayechipukia kwa nguvu Fadhili Awadh 'tiger' katika uzito wa wealter (66kgs) pambano la raundi kumi, ambao nao pia wanategemea kupima hiyo kesho.
kizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa mabondia wanaotegemea kupima ni mbaruk heri mabae atapima kwa ajili ya kuzipiga na lusekelo daudi ,Issa omar nampepeche na Hassan kiwale’moro best’, Zumba kukwe na Jacob maganga, Adam Yahaya na Harman shekivuli, jocky hamis na mbena rajab, Ernest Bujiku na Shah kasim, shaban bodykitongoji na mwinyi mzengela, shaban manjoly na kasim chuma.
Nae Mtanzania aishie Canada kareem kutch atapima na Tata boy kwa ajili ya pambano la kimataifa la mchezo wa kickboxing la raund tano, Mabondia wote wameshawasili Dar es salaam, wakati Alibaba Ramadhan wa Arusha na Jacob maganga wa Tanga wamefikia katika hotel ya valley view wakati kareem kutch yupo Durban hotel kariakoo wapo vema na wenye furaha kwa mapambano yao