Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*MABASI YENYE UWEZO WA KUTEMBEA MAJINI NA NCHI KAVU KUZINDULIWA NCHINI MWAKANI NA KAMPUNI YA TRANSEVENTS LTD

$
0
0

Kampuni ya Transevents Marketing Ltd ya nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport (DAT) inayotengeneza mabasi kutoka Uholanzi  yenye uwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayo anzia Tanzania kuwa na aina hiyo ya mabasi, inatarajia kuzindua mabasi hayo mapema mwakani.

Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania, pamoja na mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha suala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu.
Mchakato huo umekwisha anza kufanyiwa kazi pia kwa ushirikiano na SUMATRA.
Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu na kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Tazama juu Video ya Basi hilo wakati likiwa katika matengenezo hadi majaribio majini.
Tazama video ya Basi hilo Likiwa linafanya safari zake Nchi kavu na Baharini pamoja na abiria ndani. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>