Mshambuliaji wa timu ya New Ukonga Veterans, Samuel Temi (kushoto) akiwatoka mabeki wa timu ya Burundi VeteransIssa Olivyee (kulia) na Shahibu Abulaa, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Leaders Club Kinondoni jana.
Katika mchezo huo Burundi walishinda kwa mabao 4-3, baada ya kutangulia kufungwa mabao yote matatu katika kipindi cha kwanza na wao kusawazisha yote katika kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko yaliyowasaidia kubadili mchezo huo. Timu hiyo imekuja nchini kwa mwaliko wa timu ya Tanzania Stars wa kusherehekea Sikukuu ya mwaka mpya, ambapo leo itashuka dimbani tena kumenyana na Tanzania Stars.
Beki wa Burundi Stars, Issa Olivyee, akiondosha hatari katika eneo lake.
Kipa wa Burundi Veterans, Shadrack Shanda, akiruka kujaribu kuokoa mchomo uliomshinda na kutinga wavuni wakati wa mchezo huo.
Kikosi cha New Ukonga Veterans.
Samuel Temi, akinyanyasa mabeki wa Burundi.....
Benchi la Burundi Veterans.
Benchi la New Ukonga Veterans.