''Nimeacha Unga na Bangi, sasa mashabiki watakoma na mavitu yangu, Bendi ya Super Star imenibadilisha, hivi sasa mimi ni mwingine kabisa na mwili wangu si unauona???, nanenepa sasa''. alisema Diouf. CHEKI VIDEO YA WIMBO WA AFRICAN UNITY HAPA CHINI
MWANAMUZIKI na Rapa mahiri wa muziki wa dansi nchini, alitua nchini akitokea nchini kenya kupiga kazi miaka ya 2003 na kujiunga na bendi ya Twanga Pepeta baada ya kufanya kazi nzuri katika albam ya Special Remix ya Ally Choki na Gurumo, Msafiri Diouf, amesema kuwa hivi sasa ameamua kuacha kula unga na kuvuta bangi.

Alipotua Twanga pia alionyesha uwezo mkubwa wa kuimba na kurap na kuibuka na baadhi ya nyimbo zilizopata umaarufu na kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya redio na Televisheni kama wimbo wa Afrcan Unity, Safari 2005 uliobeba jina la Albam na Shafii uliokuwa katika albam ya Mtu Pesa.
Kadri siku zilivyozidi kwenda Rapa huyo mahiri alizidi kupotea kwa kuanza kutumia madawa, jambo ambalo lilianza kumpotezea umaarufu kwa kudharaulika huku akianza kushindwa kufanya kazi vizuri jukwaani ikiwa ni pamoja na kukata sauti, kushindwa kuimba kwa kiwango kilichozoeleka, kutokaa jukwaani kwa muda mwingi na hata kuchelewa kazini ama kutokuwepo wakati wimbo anaotakiwa kuimba unapopigwa na kuimbwa na mwanamuziki mwingine.
Diouf, alikili kuwa ni kweli akikuwa ameshapotea katika Anga za Muziki, na kusema kuwa anaishukuru sana bendi ya Super Star na uongozi wake kwa kumbadilisha na kujikuta akimudu kuacha kuendelea na kutumia madawa hayo na badala yake akibadilika na kupiga kazi zaidi.
Bendi ya Super Star, imeundwa na baadhi ya wanamuziki aliokuwa nao katika bendi ya Twanga Pepeta, kama mpiga Kinanda, Victor Mkambi, mwimbaji Amigolasi, mwimbaji mwingine aliyekuwa na bendi ya Extra Bongo, Rogat Hegga 'Katapila' na wengineo.