Kocha mpya wa makipa wa timu ya Yanga, Juma Pondamali (kushoto) akimfanyisha mazoezi kipa wa timu hiyo, Juma Kaseja wakati wa mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Pondamali na Boniface Mkwasa, wameteuliwa kukinoa kikosi hiho baada ya kutimuliwa aliyekuwa kocha mkuu kutimuliwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Kocha mpya wa Yanga, Charles Mkwasa (kulia) akiwafua wachezaji wakati wa mazoezi yao yanayoendelea kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama, Dar es Salaam. Kocha huyo ameteuliwa kuchukua mikoba ya kocha mkuu aliyetilimuliwa mwishoni mwa mwezi ulipoita.