Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM kwa mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha Chadenje aliyehama kutoka Chama Cha Wananchi,CUF wakati wa sherehe za uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka 37 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa huko Kiwalala, wilayani Lindi Vijijini.
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete akimpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Mkoa wa Lindi Bwana Ali Omar Chitanda, ambaye amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Mama Salma baada ya kumpongeza alimtambulisha kwa wananchi akiwa pamoja na Bi. Asha Chadenje wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka y37 ya CCM mkoani Lindi.
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimnadi Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kiwalala kupitia CCM, Bwana Shineni Hamis Zahoro wakati wa sherehe za miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Kiwalala terehe 1.2.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wanachama wa CCM na wananchi wa Lindi Vijijini wakati akizindua rasmi sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi katika mkoa wa Lindi. Shughuli hiyo ilifanyika katika kata ya Kiwalala iliyoko Lindi Vijijini. Sherehe hiyo ilienda sambamba na kumnadi mgombea wa udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi katika kata hiyo Bwana Shineni Hamis Zahoro katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 9.2.2014.
Ngoma ya Tambiko inayochezwa na wananchi wa kabila la wamakonde nayo ilikuwa ni kivutio tosha wakati wa sherehe za uzinduzi wa miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa kwenye kata ya Kiwalala, Lindi Vijijini tarehe 1.2.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI