Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*VIONGOZI WAPYA WA IKULU SACCOS WAJITAMBULISHA KWA KATIBU MKUU KIONGOZI NA KUKABIDHI RIPOTI YA UTENDAJI.

$
0
0
 Na Freddy Maro. Ikulu.
Uongozi Mpya wa ikulu SACCOS leo umejitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, ikulu jijini Dar es Salaam na kukabidhi ripoti ya utendaji ya SACCOS hiyo.

Waliojitambulkisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS Bwana Theofrid Kikombele,Makamu Mwenyekiti Bwana David Kivembele na Mshauri Mkuu Bwana Joseph Sanga.

Akizungumza mara baada ya kujitambulkisha, Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid Kikombele alisema uongozi huo umepanga mikakati madhubuti ya kuiendesha SACCOS hiyo kwa uwazi na ufanisi zaidi ikizingatia kutenda kazi kwa weledi na kuwahamasisha wafanayakazi wengi zaidi kujiunga.

Mkakati mwingine, alisema Bwana Kikombele ni kwa SACCOS hiyo kuanzisha vitega uchumi mbalimbali kwa lengo la kupanua mtaji ili kuweza kuwahudumia vyema wanachama wa SACCOS hiyo kwa  kuwawezesha kukopa zaidi kwaajili ya shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Wakati wa mkutano huo kati ya Katibu Mkuu na Uongozi wa Saccos hiyo Viongozi hao walikabidhi ripoti ya utendaji wa SACCOS hiyo na walimuomba Katibu Mkuu Kiongozi kujiunga na SACCOS hiyo, ombi ambalo aliliafiki na kuahidi kutoa ushirikiano kuboresha SACOSS hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>