Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*DIDIER DROGBA KUREJEA CHELSEA?????

$
0
0
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast, anayekipigi nchini Uturuki na Chama la Galatasaray, Didier Drogba, huenda akarejea Jiji la England kuitumikia timu yake ya zamani ya Chelsea, katika msimu wa majira ya kiangazi.

Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho, amesema kuwa yupo mbioni kumrejesha mpachika mabao huyo kikosini ili kuimarisha na kuongeza kasi katika safu ya ushambuliaji.

Aidha imeelezwa kuwa mmiliki wa Klabu hiyo,  Roman Abramovich, anamapenzi ya dhati na mshambulizi huyo na ameonyesha nia ya kumsajili tena ili arejee kuitumikia timu Klabu yake ya zamani.

Akiwa na Klabu ya Chelsea, Drogba anayetarajia kutimiza miaka 36 mwezi Machi, aliweza kuwika na kucheza kwa mafanikio makubwa na hasa kwa ufundi wa kupachika mabao na kuwa kinara wa ufungaji mabao katika michuano mbalimbali pamoja na ile ya Ulaya.

Galatasaray, itakutana na Chelsea ikiwa mwenyeji katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora inayotarajia kupigwa keshokutwa. 

Hata hivyo, Uongozi wa Klabu ya Chelsea, haujaweka wazi kuhusu kuanza mazungumzo na mwanasoka huyo juu ya kumrejesha England.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>