Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

KAMERA YA SUFIANIMAFOTO MITAANI

$
0
0
 Jamaa ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, akipata kifungua kinywa Supu na chai kwa Mama Ntilie pembezoni mwa Barabara eneo la Msamvu mjini Morogoro kama alivyonaswa na kamera ya Mafoto hivi karibuni.
 Mkazi wa vijiji vya Morogoro akisafirisha mkaa kuelekea kufanya biashara maeneo ya katikati ya mji wa Morogoro.
 Mfanyabiashara wa Nyanya eneo la Mikese, akiandaa biashara yake ya nyanya, viazi na vitunguu, tayari kwa kusubiri wateja ambao wengi wao ni wasafiri wanaotumia barabara hiyo, kutoka Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam.
 Askari wa usalama barabarani, wakipozi pembezoni mwa barabara hiyo, wakijipoza kwa kujisomea magazeti baada ya kazi kubwa ya kuongoza magari katika eneo hilo.
 Kitoweo eneo la Ruvu darajani.......
 ''Baba Karudi'', hata katapila kama hubeba mzigo japo halina mahala maalumu pa kubebea mzigo, hapa mkaa unasonga tuuuu.....
Baada ya kazi ngumu na jua kali askari hawa walikutwa wakiwa wamepumzika eneo la Kibaha... Ila huyu wa kulia aliyeshika kichwa sijui alikuwa akiadhibiwa nini.......

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>