DODOMA,Tanzania
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Kada wa CCM, Ridhiwani Kikwete kuwa mgombea wake wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, marehemu Said Bwanamdogo.
Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya CCM kupitia Idara ya Itikadi na uenezi CCM, imesema wakati uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi huo utafanywa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kampeni zitaongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa baada ya mchakamchaka mkali, kampeni za CCM zitafungwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhwan Kikwete akijaza fomu ya kugombea jimbo hilo.
Ifuatayo chini ni Taarifa Rasmi ya CCM