Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*FAIDA NA HASARA YA KUTANUA KUKWEPA FOLENI ZA ASUBUHI

$
0
0
 Askari wa Usalama Barabarani, Mwanamama, akimsimamisha dereva wa gari ndogo aliyekuwa akitanua pembeni kukwepa foleni ya asubuhi katika Barabara ya Kinondoni karibu na Ubalozi wa India, ambapo magari yaliyokuwa kwenye foleni hiyo yalisimama kwa dakika 25 bila kuitwa. 

Askari huyo alisimama mbele ya gari hilo na kisha kumfuata dereva ambaye alijaribu kujitetea lakini wapi, askari huyu alimuamuru dereva huyu kurudi nyuma hadi alikokuwa. 

Baada ya mabishano yasiyopata muafaka dereva huyu aliamua kurudi nyuma na kugeuza gari na kutokomea zake. Haikuweza kufahamika alirudi hadi wapi kwani foleni hiyo ilikuwa ndefu kiasi cha kufika hata Kinondoni A kwa asubuhi hiyo. 

Faida ya kutanua kama hivi ni pale unapofanikiwa kuyafuka magari yote na kupata nafasi ya kuingia barabarani kabla ya kuonekana au kunaswa na askari hawa, lakini moja ya hasara zake ndiyo kama hivi, kurudishwa ulikotoka ama kuandikiwa kulipa faini asubuhi asubuhi.
 Eheee, unasemaje? Sikuelewi kwani hawa waliokaa katika foleni hawana haraka kama wewe.....
Haya geuza urudi ulikotoka kabla sijakuandikia kulipa faini asubuhi hii......

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>