Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*WAZIRI WA MAJI AZINDUA MRADI WA MAJI WA SHILINGI MILIONI 300 KIJIJI CHA MVUMI MAKULU MKOANI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma,Fatma Ally, wakizindua kisima cha maji, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo mchana wilaya ya Chamwino. Mradi huo mkubwa wa maji wenye uwezo wa kuwahudumia wakazi zaidi ya 13,000,  umegharimu kiasi cha fedha Sh. Milioni 300.
 Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,Fatma Ally  kwa pamoja wakifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi rasmi na matumizi ya maji salama ya bomba hilo.
 Muonekano wa kisima hicho baada yakuzinduliwa.
 Waziri wa Maji,  Profesa.Jumanne Maghembe, akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvumi makulu Mkoani Dodoma, baada ya kuzindua rasmi kisima hicho.
 Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akipanda mtiwa kumbukumbu baada ya uzinduzi huo.
 Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Mvumi wakishuhudia uzinduzi huo.
 Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akizungumza na wanakijiji wa Mvumi makulu Mkoani Dodoma.
 Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,Fatma Ally (kushoto) na Ofisa Tarafa
wa Chamwino, Mohamed Mfaki, wakielekea kuzindua Bomba la maji.
Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Adrian Jungu.baada ya uzinduzi huo. Picha na Solomon Philemon

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>