Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*TAIFA STARS YAKUBALI KICHAPO CHA NYUMBANI BAO 1-0 DHIDI YA UGANDA

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars),John Boko (14) akimiliki mpira mbele ya Beki wa timu ya Uganda ( The Cranes) wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya (CHAN) mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu ya Taifa Stars imekubali kipigo cha bao 1-0.
 John Boko (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Uganda.
 Haruna Chanongo (kushoto) akijaribu kupambana na beki wa Uganda, kuwahi mpira.
 Mrisho Ngassa, akijaribu kuwatoka Mabeki wa Uganda wakati wa mchezo huo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
*************************
Taifa Stars imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya leo (Julai 13 mwaka huu) kufungwa bao 1-0 na Uganda (The Cranes) katika mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Denis Iguma ndiye aliyefunga bao hilo pekee kwa Uganda dakika moja baada ya mwamuzi Thierry Nkurunziza kutoka Burundi kupuliza filimbi kuanzisha kipindi cha pili cha mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumzia matokeo hayo, Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema mpira wa miguu ni mchezo wa kufunga mabao ambapo timu ilipata nafasi nzuri katika dakika ya kwanza tu lakini ilishindwa kuibadili kuwa bao.

“Uganda walitengeneza nafasi moja tu katika kipindi cha kwanza wakati sisi tulikuwa nazo kadhaa. Kipindi cha pili tuliwapa nafasi wakafunga bao lao. Lakini kwa kifupi kama wao wameweza kufunga hapa (Dar es Salaam), hata sisi tunaweza kufunga Kampala,” amesema Kim akizungumzia nafasi ya timu yake kusonga mbele.

Timu hizo zitarudiana jijini Kampala kati ya Julai 26 na 27 mwaka huu ambapo mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kwenda kwenye fainali za tatu za CHAN zitakazofanyika Afrika Kusini. Stars ilicheza fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>