Dakika 90 za Mtanange wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam Fc, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, zimemalizika kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Yanga kulazimishwa sare na kufanya timu
kugawana pointi baada ya kutoka sare kwa kufungana bao 1-1.
Bao la Yanga lilifungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza huku bao la kusawazisha la Azam Fc, likifungwa na Kelvin Friday katika dakika ya 83.
Katika dakika ya 70, Yanga walipata penati baada ya beki wa Azam, Said Morad, kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Penati hiyo ilipigwa na Hamis Kiiza na kupanguliwa na kipa Aishi Manula, na katika heka heka hizo Beki wa Azam Fc, Erasto Nyoni alizawadiwa kadi nyekundu.
Kwa matokeo hayo sasa Azam Fc inaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo ikiwa na jumla ya Pointi 44 huku Yanga ikibaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 40 lakini ikiwana na mchezo mmoja mkononi unaotarajiwa kupigwa mwishoni mwa wiki mjini Tabora na Rhyno, na mbeya city wakibaki nafasi ya tatu.