
Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania, Juma Boma (wa pili kulia) akipanda ndege mpya aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda uwanja wa ndege wakimataifa wa Songwe. Shirika hilo limeanza safari zake kwenda Mbeya ambapo itaruka mara nne kwa wiki.

Kaimu mkurugenzi wa biashara na masoko wa shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Juma Boma akipokea maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo, muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege yao mpya aina ya CRJ-200 iliyotumika kuzindua safari za kati ya Dar es Salaam na Songwe. Nyuma yake ni kaimu mkurugenzi wa ufundi, Patrick Itule. Shirika hilo litakuwa linaruka mara nne kwa wiki kwenda Mbeya.