Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Pichani), anatarajiwa kutua mjini Sumbawanga, leo saa tano asubuhi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Rukwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka Ofisi ya CCM mkoa wa Rukwa zilizopo mjini Sumbawanga zimesema, baada ya kuwasili Kinana atakwenda katika Ofisi ya CCM ya mkoa ambako atapewa taarifa ya Chama ya utekelezaji wa Ilani mkoani Rukwa na baadaye kufuatiwa na taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa ilani hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kupata taarifa za Chama na Serikali kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM, Kinana anaondoka mjini Sumbawanga na kwenda Wilaya ya Nkasi ambako ataanza rasmi ziara yake kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishuka kwenye Ndege, Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga baada ya kuwasili leo kwa ajili ya kuanza ziara ya siku 21, katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimlaki Kinana (kulia) Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, leo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa, Lahel Ndegeleke
Chipukizi wa CCM, Sharifa Tamim akimvisha skavu Kinana Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Kinana akipita katika paredi la Chipukizi baada ya kulakiwa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Kinana akiwasalimia viongozi mbalimbali Uwanja wa Ndege wa Sumbawanja, anayesalimia (kushoto) ni Mjumbe wa NEC, Ali Karume
Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM Sumbawanga mjini, Emmanuel Kilindu, baada ya kuwasili Uwanja wa Sumbawanga, Kati ni Mzee wa Chama, Clisant Msindakaya
Kinana akisalimia wananchi Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Kinana na Karume wakiaga wananchi katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Kinana na Karume wakifurahia ngoma, Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga
Kinana akiwaaga wananchi waliompokea Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga

Kinana akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Rukwa kuzungumza na Kamati ya Siasa ya mkoa.