Mwenyekiti wa Kamati namba tano(5) ya Bunge Maalum la Katiba Hamad Rashid Mohamed (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kamati namba kumi(10) ya Bunge Maalum la Katiba Paul Kimiti (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kamati namba kumi(10) ya Bunge Maalum la Katiba Paul Kimiti (katikati) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Machano Othman Said akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kuhusu muundo wa muungano unaofaa wakati wa kikao cha Kamati namba nne (4) kilichokuwa kinapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya
Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba Dr. Sira Ubwa Maboya (kushoto) akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kulia) akisamiliana na wajumbe wenzake leo mjini Dodoma mara baada ya kikao cha asubuhi cha Kamati namba kumi (10) cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Kamati namba tatu (3) ya Bunge Maalum la Katiba Shamsi Vuai Nahodha akiongoza mjadala wa Kamati hiyo leo mjini Dodoma wakati wanapitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ,Kamati namba nne (4) wakiwa katika kikao leo mjini Dodoma cha kupitia vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba kwa ajili ya kuiboresha. Picha na Magreth Kinabo-MAELEZO
***************************************
Na Magreth Kinabo – Dodoma
Kamati 12 za Bunge Maalum zimeaanza kazi vizuri ya kuchambua Rasimu ya Katiba, huku baadhi ya wenyeviti wakisema kuwa muda wa siku mbili wa kujadili sura ya kwanza na ya sita hautoshi.
Hayo yamebainika katika mahojiano ya Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya Bunge hilo, Anne Kilango Malecela, yayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
“ Tatizo lililojitokeza ni kwamba muda wa siku mbili hautoshelezi , leo tumejadili sura ya kwanza sehemu ya kwanza kesho tutajadili sehemu ya pili ya sura ya kwanza hivyo tunaweza tusiiguse sura ya sita.
“ Wenzetu walikakataa Kanuni zisirekebishwe. Lakini wenzetu wapinzani wameliona hilo wameanza kusema muda hautoshi,” alisema Anna .
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo atamweleza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitaa (leo jioni ) kuwa muda hautoshi.
Mwenyekiti huyo tatizo lingine lililojitokeza katika kamati yake ni baadhi ya wajumbe kutokuwa na uelewa wa tofauti ya dola na nchi, hali iliyomfanya kutumia kanuni namba 56(7) kumwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo ikiwezekana kumleta mtaalamu wa sheria ili kuweza kutoa elimu hiyo leo (jioni) juu ya masula hayo.
Akizungumzia kuhusu mjadala alisema wajumbe wote walijitayarisha vizuri na walishindana kwa hoja hivyo hakuna aliyetoa maneneo makali.
Akizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo, kwa sababu alikuwa katika Mwenyekiti wa Kamati namba moja ,Ummy Ali Mwalimu alisema wajumbe walichangia kwa utulivu.
Ummy alisema kilichojitokeza katika kamati yake ni kuwa muda hautoshi kama ilivyodaiwa na baadhiya wajumbe kutoka upinzani, chama tawala na kutoka 201.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya namba tano ya Bunge hilo ,Hamad Rashid alisema kamati yake mjadala unaendelea vizuri na ulikuwa wa kistaarabu.