Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*ZIARA YA KINANA KATIKA WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA

$
0
0
Kijana Ramadhani Ali wa Kijiji cha Kasanga kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa akitoka ziwani na samaki wake aina ya migebuka.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya mpya ya Kalambo, Aprili 2, 2014, Ofisi hiyo ipo mji mdogo wa Matai mkoani Rukwa jana. Kinana yupo katika mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama, Utekelezaji wa ilani ya chama na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzipatia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanga matofali baada ya kushshiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya mpya ya Kalambo,  Ofisi hiyo ipo mji mdogo wa Matai mkoani Rukwa Aprili 2, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiondoka kwenye Ofisi ya CCM wilaya mpya ya Mkalamo baada ya kushiriki ufyatuaji matofali kwa ajili ya kuboresha jengo la ofisi hiyo. Watatu kulia ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume ambaye amefuatana na Kinana katika ziara ya mkoa wa Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa shina namba moja, Apolinary Kibiko, alipofika kwenye shina hilo, katika kijiji cha Matai, wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye shina namba mbili la mjumbe, Daudi Nkaisi (kushoto), katika mji mdogo wa Matai, wilaya mpya ya Kalambo mkoani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>