Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*TANZANIA YAPOKEA MKOPO WA BILIONI 87 ZA UJENZI WA VITUO VYA KUHIFADHIA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (kushoto) akimpa mkono wa shukrani Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya  kusaini  mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha(Sera), Saada Salum(wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira A.Silima wakipiga makofi ya shukrani Baada ya Waziri wa Fedha kusaini mkataba wa mkopo wa kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa kutoka  Export and Import Benki ya Korea,jijini Dar Es Salaam.
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa kushoto akiwa na Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za  kitanzania,waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dickson Maimu (wa tatu kushoto ) na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import Korea  Yong Hwan Kim(wa pili kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo baada ya halfa ya kusaini Mkataba wa Mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa, leo jijini Dar Es Salaam.
 Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (wa pili kushoto),Balozi wa Korea nchini Chung Il(wa kwanza kulia),Mwenyekiti na Raisi wa Benki ya Export and Import Korea Yong Hwan Kim(wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Saada Salum(kushoto), wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kusaini mkataba wa mkopo wa Kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa kutoka Benki ya Export and Import Korea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea baada ya hafla ya kusaini iliyofanyika Wizara ya Fedha leo jijini Dar Es Salaam. Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>