Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE APOKEA TUZO YA "STAND UP FOR AFRICAN WOMEN

$
0
0
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, akizungumza na ujumbe kutoka African Medical Research Foundation (AMREF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo hapa nchini Dr. Festus  Ilako. Mama Salma  alikutana na ujumbe huo ofisi za WAMA tarehe 11.4.2014.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya kushawishi wake wa Marais wa Afrika katika kutetea haki za wanawake na watoto ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto “ Stand Up for African Mothers”. Anayekabidhi tuzo hiyo ni Mkurugenzi Mkazi wa AMREF hapa nchini Dr. Festus Ilako. Sherehe  hiyo ilifanyika kwenye ofisi za WAMA tarehe 11.4.2014.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya kushawishi wake wa Marais wa Afrika katika kutetea haki za wanawake na watoto ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto “ Stand Up for African Mothers”. Anayekabidhi tuzo hiyo ni Mkurugenzi Mkazi wa AMREF hapa nchini Dr. Festus Ilako. Sherehe  hiyo ilifanyika kwenye ofisi za WAMA tarehe 11.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kkwete akiongea na ujumbe kutoka AMREF  mara baada ya kumkabidhiwa tuzo ya “Stand up for African Mothers” tarehe 11.4.2014.
**************************************
Na Anna Nkinda – Maelezo
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya kuwa balozi wa kampeni ya Simama kwa ajili ya mwanamke wa Afrika “Stand for African Mother campaign” kwa ajili ya kujitoa kwake na kuwahamasisha wake wa Marais wa Afrika kusimama na kupigania haki za kina mama na watoto.

Hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo ambayo imetolewa na Taasisi inayoshughulika na masuala ya Afya  Afrika (AMREF) ilifanyika katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) zilizopo jijini Dar es Salaam.

Akiongea kabla ya kukabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi mkazi wa AMREF Dkt. Festus Ilako alimpongeza  Mama Kikwete kwa kazi anayoifanya ya kuhakikisha kuwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinapungua nchini. 

“Tangu kuzinduliwa kwa  kampeni hii mwaka 2012 tumefanikiwa kusomesha wakunga 250 hii ni karibu na  asilimia 10 ya wakunga ambao wanatakiwa kusomeshwa katika kampeni hii.

Changamoto kubwa inayotukabili ni kutokuwa na fedha za  kutosha za kuwasomesha wakunga hawa lakini naamini ifikapo mwaka 2016 malengo yetu yatatimia”, alisema Dkt. Ilako.

Alisema mkunga mmoja anaweza kuwahudumia wanawake 5000 kwa mwaka,  kama watu wataweza kulipia mafunzo ya wakunga idadi yao itaongezeka na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.

Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA   aliwashukuru AMREF kwa tuzo waliyompatia na kusema kuwa siyo kama yeye ni hodari sana bali ni kutokana na kujitoa kwake kushiriki na kupigania mambo mbalimbali yahusuyo wanawake. 

Mama Kikwete alisema, “Ukimwezesha mwanamke mmoja umeiwezesha familia nzima pia mwanamke akiamua kuiinua au kutoiinua familia yake anaweza kufanya hivyo jambo la muhimu ni kumsaidia ili aweze kupata elimu ambayo itamsaidia kuepukana na ujinga, maradhi na umaskini jambo ambalo litasaidia kupunguza na kufikia sifuri vifo vya wamama wajawazito na watoto”.

Mwenyekiti huyo wa WAMA pia aliwataka AMREF wajipange na kuweka maadhimio yao ili waweze kuongeza kasi zaidi ya kuwasomesha wakunga na kuweza kuvuka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 30 kwa mwaka.

Mama Kikwete aliwahimiza wake wa marais wa Afrika kuunga mkono kampeni ya AMREF ya kuwasomesha wakunga 15000  barani Afrika ili kupata wataalamu wengi zaidi ambao watawahudumia kina mama wajawazito wakati wa kujifungua na hivyo kupunguza vifo vyao na vya  watoto vinavyotokana na tatizo la uzazi katika mkutano wao uliofanyika mwezi wa tano mwaka 2013 makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.


Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa nchi mbalimbali Duniani  nchini Tanzania ilizinduliwa na Mama Kikwete mwishoni mwa mwaka 2012 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam huku ikiwa na malengo ya kusomesha wakunga 3800 hadi kufikia mwaka 2016.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>