Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwenye kituo cha walemavu cha Rasibura na Ndugu Simon Mnimbo, Mkurugenzi wa Shirika la Caritas la Kanisa Katoliki Jimbo la Lindi wakati Mama Salma alipokitembelea kituo hicho tarehe 20.4.2014, siku ya Pasaka kwa ajili ya kuwapelekea zawadi za sikukuu.
Jengo linalotumika kwa makazi ya walemavu huko Rasibura, katika Mji wa Lindi likiwa katika hali mbaya ya uchakavu. Jengo hilo awali lilikuwa likitumiwa kama gereza na Jeshi la Magereza la Lindi na baadaye kukabidhiwa kwa Idara ya Ustawi wa Jamii na ndipo walipoamua kutumia kama jengo la kuwatunzia watu wenye ulemavu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi yake ya Pasaka Ndugu Theresia Thomas ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi katika kituo cha Rasibura huko Lindi. Baadaye Mama Salma anaonekana akipiga picha naye akiwa amelala kitandani kwani Theresia hawezi kukaa wala kusimama.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na baadhi ya watu wenye ulemavu wanaoishi katika Kituo cha Rasibura mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao za Pasaka tarehe 20.4.2014.