Baadhi ya washiriki wa Miss Ubungo 2014 wakiwa katika pozi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Miradi wa Kampuni ya AKO Group Ltd, Honesty Minde, alisema wameamua kudhami ni shindano hilo ili kusaidia kulifanikisha.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika pozi kwenye clabu ya Ako Labamba.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CLABU ya Ako Labamba ya jijini Dar es Salaam imejitosa kudhamini shindano la Miss Ubungo litakalofanyika mwezi ujao.
Alisema wameamua kuwasaidia waandaaji wa shindano hilo ili kukuza sanaa ya urembo, wakiamini kuwa ndio dira ya maendeleo kwa Watanzania wote.
“Tuliamua kuwapa maeneo ya kufanya mazoezi pamoja na huduma nyingine muhimu kwa waandaaji na warembo wao. “Naamini kwa pamoja tutafanikisha kwa vitendo mafanikio makubwa ya Miss Ubungo mwaka huu, ukizingatia kuwa ndio lengo letu,” alisema.