Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*MASOGANGE NA MWENZAKE KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA MARA YA PILI AGOSTI 13

$
0
0
Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa nchini Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.

Aidha alisema kuwa kutokana na ushahidi kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani tena tarehe 13 ya mwezi ujao.
Kamanda Nzowa alisema kuwa baada ya tukio hili, nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo.
"Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi," alisema Nzowa.
Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakitokea Tanzania, walikutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazina matumizi nchini, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles