Mwili wa Marehemu George Tyson (pichani) utapelekwa nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach (eneo la Makonde) jijini Dar es salaam leo Jumanne Juni 3, 2014 kuanzia majira ya saa kumi jioni kwa ajili ya kuaga.
Mwili utakuwepo nyumbani hapo mpaka siku ya Jumatano Juni 4, 2014 ambapo mwili utapelekwa kwenye viwanya vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es salaam, kwa ajili ya shughuli ya kuaga mwili na ibada fupi.
Baadae mwili utapelekwa kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere tayari kwa kusafirishwa kwenye jijini Nairobi nchini Kenya kwa mazishi.
Tutaendelea kuwaletea taarifa
kadri zitakavyokuwa zikitufikia.