Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*SIKU YA MSANII YAZINDULIWA JIJINI DAR SASA KUANZA KUADHIMISHWA OKTOBA 25 KILA MWAKA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipiga Gitaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msanii itakayokuwa ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production (T) Limited Bw. Emmanuel Mahendeka wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Msanii itakayoadhimishwa tarehe 25 Oktoba,Siku ya Msanii inaratibiwa kwa ushirikiano baina ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA na Kampuni hii ya Haak Neel Production. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA  Bw. Godfrey Mungereza.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production (T) Limited Bw. Emmanuel Mahendeka wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Msanii,mapema wikiendi hii, jijini, katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko na Kaimu Katibu wa BASATA Bw. Godfrey Lubejo Mungereza.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akishiriki kuwakumbuka  Wasanii waliotangulia mbeleza za haki, kabla ya kuendelea na hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaanii itakayokuwa inaadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Bibi. Sihaba Nkinga, Mkurugenzi Mkuu wa Haak Neel Production Bw. Emmanuel Mahendeka na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akielezea kwa ufupi histori ya Siku ya Msanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku hiyo itakayokuwa ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Haak Neel Production (T) Ltd Bw. Emmanuel Mahendeka  akizungumza na wadau wa sanaa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaanii iliyozinduliwa mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa India hapa nchini Bibi. Chitra Suresh (wapili kutoka kulia) akifuatilia baadhi ya kazi za wasanii wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msanii mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
 Mwanamitindo mkongwe Asiah Idarius wa kwanza akiwa na baadhi ya wanamitindo wake wakati wa hafla ya uzinduzi wa hafla Siku ya Msanii mapema wikiendi hii.
 Wasanii wa Kikundi cha Ngoma kutoka Dodoma wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipokea zawadi ya gauni kutoka kwa mbunifu  wa mavazi na Mwanamitindo Asiah Idarius(katikati) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaonyesha wadau wa Sanaa zawadi ya gauni aliyozawadiwa na Mbunifu  wa Mavazi na Mwanamitindo Asiah Idarius wakati wa hafla ya uzinduzi wa Siku ya Msaani mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (mwenye koti jeupe) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga  wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa wakati wa hafla uzinduzi wa Siku ya Msanii iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>