Baadhi ya nyumba za wananchi zilizoachwa na wananchi waliokimbia mapigano hayo.
Mpiga picha Ton Koene alizuru Jamuhuri ya Afrika ya kati kwa mara ya kwanza miaka minane iliyopita, lakini mapema mwaka huu alirejea katika nchi hiyo ambapo aliwapiga picha raia ambao wamekwama katika vita vya kidini vinavyotokota.
CAR imekumbwa na vita vya kidini kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa hasa kati ya waisilamu wa Seleka na wakristo.
Maelfu wameuawa huku mamia wakitoroka vita hivyo
Mjini Bangui, karibu nusu ya wale wanaoishi mjini humo wameondoka tangu mwezi Disemba , wengi wakiishi katika makao ya muda kambini katika uwanja wa ndege.
Waisilamu wachache sana wamesalia katika mji mkuu wengi wakitoroka na kuelekea katika eneo la Kaskazini.
Katika miezi ya kwanza mitatu mwaka huu waliwatibu zaidi ya wagonjwa 3,250, wengi wakiwa na majeraha ya kivita.