Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said ‘Sharapova’ , Otilia na wengineo watanogesha na kuacha historia siku hiyo .
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solutions (LIMSO), Khadija Kalili ambaye pia ndiyo Mratibu wa shindano hilo.
Pia anawaahidi wakazi wa mkoa wa Pwani na wilaya zake zote kwa jumla kupata burudani ya aina yake siku hiyo hivyo amewaomba wajitokeze kwa wingi.
Alisema katika shindano hilo warembo kumi ndiyo watakaopanda jukwaani ikiwa ni katika kumsaka malkia wa Pwani ambaye atauwakilisha Mkoa katika shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2014.
Kalili aliongeza kwa kusema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea ambapo pia anawataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni wadhamini wakuu Redd’s Premium Cold, DIRA Media Group, Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa, Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept, Bongoweekend.blogspot.com, Maisha Plus (Police Mess) , Montage (Teddzzzzz), Filbert Bayi Foundation (FBF).Kiingilio ni sh. 10,000.