
Watu Sita wamepoteza maisha katika ajali ya gari (daladala) iliyogongana na Lori eneo la Makongo jijini Dar es Salaam, mchcna wa leo na wengine 14 kujeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Lugalo kwa matibabu ya awali na kisha kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili. Mashuhuda wa ajali hito awameeleza kuwa chanzi cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa daladala hilo lililokuwa likitokea Tegeta kuelekea Mwenge baada ya kumshinda dereva na kuhamia upande wa pili wa barabara na kugongana na Lori hilo na gari la Raia wa China lililokwenda kuwakanyaga majeruhi wengine katika eneo hilo. ![]()

Ajali ya Lori aina ya Fuso iliyotokea eneo la Kongowe nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Katika ajali hiyo hakuna mtu alyejeruhiwa. Picha na Yvonne Mhando.