Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*NCHI YA BOLIVIA 'NI KAMA TU BONGO' KASORO LUGHA TU

$
0
0
 Kijana wa Bolivia, akifuta kioo cha daladala likiwa katika foleni kwenye moja ya mtaa wa nchini humo, ambapo baada ya kumaliza kufuta kioo hicho huzunguka dirishani kwa dereva na kudai ujira wake, ambapo hulipwa pesa yao inayoitwa Boliviano kiasi cha boliviano 5 kwa kila gari. 

Tatizo la wakazi wa nchi hii ni mawasiliano kwa njia ya lugha kwani watu wote huzungumza lugha yao tu, na ni mtu mmoja kati ya 100 unayeweza kumbahatisha akizungumza angalau Kingereza cha kuibia ama akakuelewa ukizungumza Kingereza. 
Wageni wote wanaokuwa wakifika nchini hapa hupata taabu ya mawasiliano baina yao na wenyeji, jambo linalowafanya wengi wao kuzungumza na wenyeji kwa kutumia ishara za vitendo ama kuchora picha ya kitu husika huku akijitahidi kufafanua kwa vitendo. 

Mfano ukiingia hotelini na kuagiza chai hueleweki ama chakula, inabidi utoe karatasi mfukoni kwako na kuchora Kikombe cha chai inayofuka moshi ndiyo unaeleweka na kisha wakati wa malipo hivyo hivyo, inabidi umpatie karatasi ili akuandikie ni Boliviano ngapi ili ukomvate kwa dola na kisha uweze kumlipa. KAZI IPO, wengi wao hawatoki nje ya nchi yao hata kwa matembezi tu ni wachache sana hufanya hivyo.
 Kijana akiendelea kufuta kioo.
 Baadhi ya wakazi wakipata huduma ya chakula cha kikwao pembezoni mwa barabara majira ya jioni, kama ambavyo imekuwa katika baadhi ya mitaa ya Bongo mida ya jioni.
 Taka zikiwa zimetapakaa na maji machafu pembezoni mwa barabara katika moja ya mtaa.
 Hata wao hurundika taka kando ya barabara kama hivi....
 Tax za Bolivia huwezi linganisha na za Bongo hata chembe, wakifika Bongo watahisi wakazi wake ni matajiri wa kutupwa na hasa wakiona Tax zinazotumika. Hii ikiwa imechoka mbaya katika Hicee ikiwa imeshikiliwa na Kijiti.
 Huku nako mvua ikinyesha ni hatari tupu kama Bongo tu....
 Chemba ya maji machafu ikitema kama inavyokua Bongo inaponyesha mvua....
 Huu ni moja ya mtaa cheki unavyofanana ''unahisi unafanana na mtaa gani wa Bongo''???
Majengo yasiyokuwa na mpangilio si Bongo pekee hata kwao yapo mengi tu...

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>