Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akitoa huduma za vyakula katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif pamoja na watendaji wa Wizara yake hapo Nyumbani kwake Mazizini.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiwa katika futari ya pamoja Nyumbani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akitoa shukrani kwa niaba ya watendaji wa ofisi yake mara baada ya futari ya pamoja kati yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Familia yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa nasaha zake mara baada ya futari ya pamoja na watendaji wake hapo nyumbani kwake mazizini.
Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar na watendaji wa taasisi nyengine za Serikali na wakaazi jirani ya nyumba ya Balozi Seif wakipata futari ya pamoja nyumbani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.