MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi (pichani chini kulia) amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha mbwa mwizi leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe jijini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amedaiwa kuwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani katika nyumba ya mkazi wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho. Picha zote na Bashir Nkoromo
Mmoja wa kijana wa mtaa huo akiinua tofali kumtwanga kibaka huyo, ambapo alimtwanga nalo kichwani.
Kibaka huyo akila kipondo huku akiburutwa kupelekwa Kituo cha Polisi.
Safari ya kuelekea Kituo cha Polisi.
Ghafla njiani Kibaka huyo alianguka chini na kuzimika baada ya kuonekana kuishiwa nguvu jambo lililowafanya wananchi hao wenye hasira waliokuwa wakimpeleka Kituoni, kutawanyika kila mmoja na njia yake.