Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*BREAKING NEEEEEWZZZZZ!!!!!!!!!,MADEREVA WA BODABODA WA BUNJU WAKAMATA GARI NDOGO LIKIWA NA MIILI YA WATU 20 LIKIELEKEA KUMWAGA PAMPO LA MPIJI

$
0
0
Habari zilizoufikia mtanda huu, usiku huu zinasema kuwa Madereva wa Bodaboda wa maeneo ya Bunju usiku huu wamefanikiwa kukamata gari aina ya Suzuki Cary, likiwa limebeba jumla ya miili ya watu 20, na wengi wao wakiwa ni wanawake wakati likielekea kumwaga katika Dampo la Mpiji. 

Aidha miili hiyo imekutwa ikiwa imegawanywa vipande vinne na ikiwa haina ngozi.

Kwa mujibu wa Reporter wetu kutoka eneo la tukio, Kituo cha Usalama kilichopo Bunju, anasema kuwa inasadikiwa kuwa miili hiyo mingi imetoka maeneo ya Interchick,huku dereva wa gari hiyo akielezwa kuwa ni mwenyeji wa Bunju.

Bado unasubiriwa uongozi wa juu wa Polisi uweze kufika eneo la tukio kwa taarifa zaidi.

Tayari Polisi wa Kituo cha Bunju na Wazo wameshafika eneo la tukio na kuanza kupiga risasi hewani ili kuwatawanya watu waliovamia kituo hicho cha polisi Bunju kwa lengo la kumuua dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo aina ya Hilux, lililokuwa limejaa viungo vya binadama vikiwa ni vibichi vikiendelea kuchuruzika damu. 

Aidha imeelezwa kuwa dereva huyo tayari alikwishafanikiwa kumwaga tripu ya kwanza eneo la Shule ya Masista ya Consolata na alipokuwa akirudi tripu ya pili ndipo akashitukiwa na madereva wa bodaboda na wananchi, waliofanikiwa kumdhibiti na kuita Polisi eneo la Tukio.

Eeeeh Mungu tunusuru na Majabari haya yanayojigeuza Mitume wa kutoa roho za watu,Wanusuru wanetu wanaotembea wenyewe huko majiani. Ameen

KAA NASI KWA HABARI ZAIDI NA MATUKIO YA PICHA ZITAKUJIA KADRI ZITAKAVYOTUFIKI.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>