Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, Jana amefanya ziara fupi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza.
Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinu uliotokea baada ya Mvua kubwa.
Mradi huo unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.
Pesa za Ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Mstahiki Meya, Ilala Jerry Silaa (kushoto) akiwa na Mhandisi wa Barabara (mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano (katikati) (wa kwanza Kulia) ni Mhandisi wa Manispaa,Muhinda Kassimu wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa kwa kiwango cha changarawe.
Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.