BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA
Yah:- RATIBA YA MABONDIA WA TANZANIA WANAOWAKILISHA TAIFA
KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA SCOTLAND (NDONDI).
Hatimaye ratiba ya mchezo wa ngumi kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola imetolewa jana tarehe 24/07/14 baada ya zoezi la kupima uzito na afya lililofanyika kuanzia saa 2.00 hadi saa 4.00 Asubuhi kwa saa za Scotland, kwa mabondia na waamuzi wote wanaotegemea kushiriki mashindano hayo`1.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa mashindanoo yataanza tarehe 25/07/14 na yatamalizika tarehe 02/08/14.katika ukumbi wa Secc (Hall 4A) na inaonyesha kuwa captain wa timu ya Tanzania Selemani kidunda ndiye atayeanza kupeperusha bendera ya taifa na hatiaye kufatiwa na mabondia wengine kama ifuatavyo:-
⦁Tarehe 25/07/14 saa 1.45 Jioni (69) kg
Kehinde Ademuyiyiwa (Nigeria) v/s Selemani Kidunda (Tanzania)
⦁Tarehe 26/07/14 saa 7.20 Mchana (60) kg
Jessie Lartey (Ghana) v/s Nasser Maffuru ( Tanzania)
Saa 1.00 Jioni (64) kg
Stevin Thanki (Malawi) v/s Fabian Gaudensi (Tanzania)
⦁Tarehe 27/07/14 saa 12.45 Jioni( 52) kg
Bye v/s Ezra Paul ( Tanzania)
Saa 1.40 Jioni (8I)kg
Mohamed Hakimu (Tanzania) v/s Sumit Sangwan (India)
⦁ Tarehe 28/07/14 saa 7.25 Mchana) (56)kg
Bashiri Nasir (Uganda) v/s Emilian Patrick (Tanzania)
Saa 1.35 jioni (49) kg
Paddy Barnes( Northern Ireland) v/s Hamed Furahisha (Tanzania)
Taarifa hizi zimeletwa na
Makore mashaga
KATIBU MKUU.