Mwakalishi wa Kampuni ya Simu ya TTCL Kanda ya Zanzibar Mohd Yussuf Mohd akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mfumo mpya wa matumizi ya mawasiliano unaotumiwa na Kampuni hiyo kwa wateja wake.
Afisa Uhusiano msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Ispector Sharif Bakar Sharif akimpatia ufafanuzi Balozi Seif juu ya mabadiliko ya pasi za kusafiria ambayo yako katika kiwango cha teknolojia ya kisasa Kimataifa.
*******************************
Maonyesho ya Biashara ya Iddi El Fitri yaliyoandaliwa na Wizara ya Baiashara Viwanda na Masoko Zanzibar kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania { Tantrade } yanaendelea katiika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Taasisi zisizopungua 67 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara zikijumuisha zile za mashirika ya Umma na Jumuiya zisizo za Kiserikali zimeshiriki maonyesho hayo ya siku nne.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seid Ali Iddi alipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo katika siku yake ya tatu na kushuhudia bidhaa mbali mbali za makampuni na wajasiri amali tofauti.
Balozi Seif akiambatana na Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Thuwaiba Kisasi,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Julian Raphael pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo alionyekana kuvutia na bidhaa hizo jambo ambalo limekuwa kivutioa kwa baadhi ya wananachi walioonekana kufurika katika eneo hilo.
Miongoni mwa mabanda ya maonyesho aliyopata fursa kuyatembelea Balozi Seif ni pamoja na Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima, Shirika la Posta, Idara ya Uhamiaji, Vigor Turky Group na Zapeta.
Nyengine ni Women Beam Light, Global Education Link, Princes Nadia Limited, Morden Natural Herbal, Busara Promotion, Trust Natural Nutrition, Shumba Cloves Foundation, Hoze Herbal Product, Ummy Vita, Zanto Food Product, Digital City Limited pamoja na Meli Nne Herbal Product.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar