Quantcast
Channel: SUFIANIMAFOTO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

*SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU WANAJESHI WASTAAFU KUDAI SH. MILIONI 3

$
0
0
Gazeti la Kiingereza la The East African, Toleo Na. 1030 lililochapishwa mwishoni mwa wiki, Jumamosi, Julai 26, 2014, limeandika habari yenye kichwa cha habari “Ex-soldiers want $3m for covert Congo operation”, ikiwa na maana kuwa wanajeshi wastaafu wanadai kulipwa dola za Marekani milioni tatu kwa kushiriki operesheni ya siri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Inadaiwa katika habari hiyo kwa zaidi ya wanajeshi 400 wastaafu wa Tanzania, wametishia kuishitaki mahakamani Serikali ya Tanzania, wakidai posho ya zaidi ya dola za Marekani milioni tatu (sawa na karibu sh. Bilioni sita) kwa kushiriki operesheni ya kivita ya siri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya 2000 na 2003.

Inadaiwa na gazeti hilo kuwa askari hao wastaafu walipelekwa Congo ili kutoa mafunzo kwa Jeshi la Congo lakini baada ya kuwasili walisambazwa katika maeneo ya Majimbo ya Katanga na Kivu Kusini kukabiliana na wapinzani wa Serikali ya Rwanda wa Interahamwe na waasi wa Burundi – FDD.

Habari hiyo siyo ya kweli, kwa hakika ni upuuzi mtupu na inalenga kupotosha ukweli na kuwapotosha wananchi.  Serikali inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao ili kuwawezesha wananchi kujua ukweli.

·        Siyo kweli kuwa Serikali ama Jeshi la Wananchi wa Tanzania lilihusika kwa namna yoyote kuwapeleka Congo Askari hao wastaafu kwa sababu kimsingi walikwishakustaafu na hawakuwa tena Jeshini.

·        Askari hao walijipeleka wenyewe Congo, kinyemela na kwa mipango yao wenyewe ambayo waliifanya na watu wanaowajua wenyewe.

·        Hivyo, kama askari hao kweli hawakulipwa, kama inavyodaiwa katika gazeti hilo basi wao wenyewe wanamjua nani wa kumdai.

·        Walichofanya askari hao wastaafu ni kinyume cha sheria na Serikali ya Tanzania iliitahadharisha Serikali ya DRC kuhusu suala hilo.

·        Serikali ya Tanzania isingependa kuhusishwa, kwa namna yoyote, katika suala hili kwa sababu haikuhusika nalo hata kama washiriki walikuwa raia wa Tanzania.

Serikali inapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa hakuna askari wake halali ambaye amepata kwenda Congo ama nchi nyingine yoyote kushiriki opereshini ya kivita na mapigano kinyemela. 

 Askari wote wa Tanzania walioshiriki ama wanaoshiriki operesheni mbalimbali duniani wamefanya na wanafanya hivyo chini ya miavuli halali ya kimataifa.
IMETOLEWA NA 
MKURUGENZI IDARA YA HABARI (MAELEZO)
2/08/2014

Viewing all articles
Browse latest Browse all 13053

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>