Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akisalimiana na Viongozi walioongozana na timu kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland wakati walipokuwa wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda akiwaelekeza jambo baadhi ya Wanamichezo walioiwakirisha Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akifurahia jambo na baadhi ya wanamichezo waliotoka kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola, huko mjini Glasgow Scotland baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko, akizungumza na wanamichezo hao kwa niaba ya Serikali wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi.
Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akizungumza na wanamichezo. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda na Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Rish Urio.
Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Nahodha wa Timu ya Taifa.
Baadhi ya wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland, wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini.
Baadhi ya wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland, wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali (hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya mapokezi na kuwakaribisha iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA.