Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga mpira kama ishara ya uzinduzi rasmi wa tamasha la Matumaini lililofanyika Ijumaa ya wiki iliyopita Agosti 8, 2014 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
MTANANGE WA YANGA NA SIMBA- WABUNGE
Mshambuliaji wa timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete, akiruka kukwepa kwanja la beki wa timu ya wabunge mashabiki wa Simba, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, wakati wa mtanange wao wa kuhitimisha Tamasha la matumaini, lililofanyika Ijumaa ya wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Wabunge wa Yanga walishinda mabao 3-2.
Yanga wakipata bao la tatu kwa mpira wa kona.... KUCHEKI MATUKIO ZAIDI BOFYA READ MORE
Mbunge Mwigulu Nchema (kushoto) akiwatoka mabeki wa timu pinzani wa Simba
Ridhiwani (kushoto) akijiandaa kumtoka beki wa Simba ambapo alipigwa tobo na kuamua kucheza faulo iliyosababisha penati iliyozaa bao la tatu.
Kipa wa Simba Wabunge, Iddi Azan, akiruka kujaribu kupangua mpira wa penati bila mafanikio.....
Aliyekuwa mwiba mchungu kwa ukuta wa Wabunge wa Simba, Ridhiwan Kikwete (kulia) akimtoka beki wa Wabunge wa Simba.
Ridhiwan, wakishangilia kwa kurusha jezi yake kwa mashabiki wa Yanga.
MENGINEYO UWANJANI HAPO
Baadhi ya waratibu wa tamasha hilo wakijadiliana jambo.
Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo, akizungumza wakati wa tamasha hilo.
Kina dada waliopangwa kusimamia na kukaribisha wageni jukwaa kuu la VIP....
Wimbo wa Taifa ukiimbwa,........
UKAGUZI WA TIMU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wachezaji wa Wabunge wa Yanga, wakati akikagua timu hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wachezaji wa Wabunge wa Yanga, wakati akikagua timu hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wachezaji wa Wabunge wa Simba, wakati akikagua timu hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wachezaji wa Wabunge wa Simba, wakati akikagua timu hizo.
Jukwaa Kuu wakifuatilia tamasha hilo....
MAPAMBANO YA NGUMI, ZA WASANII HADI MABONDIA KAMILI CLOUDE vs JB
Bondia Cloude akiingia uwanjani kupanda ulingoni kuzichapa na JB.
Bondia JB, akiingia uwanjani kuzichapa na Cloude...

Mabondia ambao ni wasanii wa Filam nchini, Cloude (kushoto na JB,wakichapana wakati wa pambano lao katika Tamasha la Matumani. Katika pambano hilo JB alishinda kwa pointi.
Chukua hiyoooo......
Cloude akimgalagaza JB..........kwa sumbwi zito......
Kichapo kikiendelea........
Cloude akitimua mbio baada ya kuona mambo yamebadilika akishambuliwa mfululizo na JB.....
Cloude, akiwa chini huku akihesabiwa na mwamuzi baada ya kuchapwa konde na JB....
NGUMI CHOKORAA vs MEMBA
Mwanamuziki wa bendi ya Mapacha wa3, ambaye pia ni bondia, Khalid Chokoraa, akiingia uwanjani na wapambe wake ili kupanda ulingoni kuzichapa na Memba.....

Khalid Chokoraa (kulia) akichapana na mpinzani wake, Said Memba, wakati wa tamasha la Matumaini, ambapo Chokoraa alishinda pambano hilo kwa pointi.
Kichapo kwa zamu......
Khalid Chokoraa (kushoto) akimchapa mpinzani wake Memba katika pambano hilo......
Khalid Chokoraa akibebwa juu kwa furaha na mashabiki wake baada ya kutangazwa kushinda pambano lake kwa pointi.....
Bondia Thomas Mashali, akiingia uwanjani akiongozana na wapambe wake kwa ajili ya kupanda ulingoni kuzichapa na Mada Maugo......
NGUMI MADA MAUGO vs MASHALI....

Bondia Mada Maugo, akiingia uwanjani kupanda ulingoni kuzichapa na Mashali......
Bondia Thomas Mashali (kulia) akichapana na mpinzani wake Mada Maugo,wakati wa pambano lao la raundi sita. Katika pambano hilo Maugo aliibuka kidedea kwa kulipiza kisasi alipomchapa kwa pointi Mashali.
Kichapo kwa zamu kikiendelea.....
Hadi apatikane mbabe......
Holaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa................
Chukua Hiyoooooooooooooooooooooooo........................
Chaliiiiiiiii................Bondia Mashali akiwa chini baada ya konde zito la Maugo.....
Hapa hata mimi sikuelewa ilikuwa ni mieleka au ngumi.............
Mashali akikwepa konde la Maugo........
Mashali akienda chini.............
Chiniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...........................
Hapa huingizi ngumi.............................
Chukua hiyooooooooooooooooooooooooooooooooo
Maugo, akiwa chini baada ya konde zito la Mashali...............
Maugo akibebwa juu na mashabiki wake baada ya kutangazwa mshindi kwa Pointi alipomgalagaza mpinzani wake Mashali......
BURUDANI....

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature, akiimba na kuwapagawisha mashabiki kwa nyimbo zake za zamani kama Mgambo,Sonia na nyinginezo.......

Sehemu ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo wakipagawa na ngoma za Nature....